Ajali: Tuambiane ukweli dhahama hili lituepuke

Ajali: Tuambiane ukweli dhahama hili lituepuke

Hatuna 1m kitu gani
Usisome kama kasuku. Soma Kwa kuelewa. Sweden nchi ndogo mno kuliko sisi yenye watu 10m ina takribani magari 5m. Sisi hapa hatuna 1m na nchi kubwa zaidi.

Uendashaji wetu usioakisi miundo mbinu yetu kwa sababu zozote zile ni lazima ubadilike.

Ya mipango ya Mungu hayatusaidii.
 
You're right!!!!!
Nakumbuka rafiki zangu Fulani walikuwa hawana uzoefu na kuendesha magari safari ndefu wakawa wanatembea mwendo sawa na mabus kwenye vibao vya speed 50 chakushangaza walikuwa wanakamatwa na traffic lkn mabus yanaenda Tu,kitu ambacho walikuwa hawajui ni kuwa speed 50 ya bus Kwa wewe mwenye gari ndogo unafikisha Hadi speed 80
Speed zote Ni sawa 40kph ya Bajaj, is equal to 40kph ya lambo or Lori nk
 
Kwa haraka haraka ajali nyingi kubwa ni za kugongana uso kwa uso zikifuatiwa na kugonga kwa nyuma na kupinduka, hii ni kwa vyombo vya abiria. Vyombo vya mizigo ni kufeli kwa breki na mengineyo.

Ushauri mzuri hadi sasa ni utanuzi wa barabara. Na sio lazima kutanua barabara zote kwa urefu wake. Inawekezana kutanua barabara kwenye maeneo korofi au kutanua barabara kwa interval ya kilometer kadhaa ili kutoa nafasi kwa overtaking.

Spidi ya sasa Km 80 kwa saa sio sahihi na hasa kwa mabasi... inaleta uchovu kwa abiria na dereva. Mabasi yawe yanakwenda kwa spidi ya 100km/h malori 80km/h na magari mengine kati ya 80 na 120km/h.

Muda wa kuendesha mabasi na malori uwe kati ya masaa 6 hadi nane. Na iwapo safari ni ya zaidi km 700, basi gari ya abiria iwe na madereva wawili na upande wa malori baada ya safari ya masaa nane dereva asimame na kulala kwa masaa 8 kabla ya kuanza tena safari yake.
 
Udereva Tanzania sio professional job.

Kwanza wanafanya kazi kama vibarua tu hawwezi kuwa na umakini na utulivu sababu ya stress.

Waajiriwe na kupewa mikataba ya ajira kama fani nyingine hawa wanabeba watu wengi.

Halafu wawe na elimu sio mtu kashindwa huko kakata tamaa ya maisha anakimbilia udereva yaniinakua kama bodaboda ambapo wengi ni wahuni tu au walikuwa vibaka huko sasa ni bodaboda ajali hazitoisha.
Udereva ni proffesional kama kazi zingine tu ,sema madereva wengi tanzania wanaifanya kazi yao unprofessional

Ova
 
Madereva wengi tz ni vichaaaa

Syo wa magari makubwa wala madogo,wote vichaa

Ova
 
Unajua herufi Moja kukamilisha Ni magari laki tano na 47 na tuko no E sasa

Tembelea takwimu za Mwigulu. Takwimu zote ziko hadharani.

Kisha zingatia msingi wa hoja.

Sweden ni ndogo kuliko Morogoro Ina magari mengi kuliko Tanzania na pia ajali kidogo kuliko Tanzania.

Kinachogomba hapa siyo kuhesabu magari 1, 2, 3 .. kama mtoto wa darasa la 4.
 
Tembelea takwimu za Mwigulu. Takwimu ziko hadharani.

Kisha zingatia msingi wa hoja.

Sweden ni ndogo kuliko Morogoro Ina magari mengi kuliko Tanzania.

Kinachogomba hapa siyo kuhesabu magari 1, 2, 3 .. kama mtoto wa darasa la 4.
Bali Ni kuhesabuje? Na hio milion mmepata wewe na mwigulu
 
Bali Ni kuhesabuje? Na hio milion mmepata wewe na mwigulu

Idadi ya watu wote duniani au nyota zote zilizopo haipatikani kutoka kwa grade IV wanaojua kuhesabu 1, 2, 3, ...
 
Hii nchi wenye elimu wanabezwa Sana , Ila ujinga ndo tatizo kubwa , umaskini pia , huwez kusafr more than 800 km Kwa basi , dunia za wenzetu hapo ni tren za umeme au aircraft , miundo mbinu mibovu na isiyokidhi , two lanes Kwa highway ni graveyard
Huu ndio ukweli hususani hiyo Dodoma road, na madereva wanakimbia sana yaani hawajali kabisa.
 
Mmeambiwa mabasi yapaki kwanza usiku yatembee malori pekee,mnaleta siasa.

Wanaowatia ujinga wao wanatumia ndege na magari binafsi yanayotembea mchana tu.
 
Ukweli n mchungu lakini tufike mahali tuuseme hata kama unauma.

Mengi yamesemwa kuhusu ajali miaka nenda rudi, lakini ajali ziko pale pale.

Bahati mbaya mzizi wa tatizo umekuwa hausemwi kwa kujua au kutokujua.

"Tatizo letu kuu kimsingi ni ujinga ndugu zangu."

1. Kulikoni dereva kuendesha gari akiwa haoni waziwazi anakokwenda?

2. Kulikoni dereva kuendesha gari bila kujali hali ya miundo mbinu alipo?

Pana haja ya kurekebisha viwango vya elimu angalau kwa kuanzia, madereva wa mabasi na malori.

Kwanini kutokuwatumia wahitimu wa vyuo vikuu kuendesha mabasi?

Kwanini kama ilivyo kwingine kama kiwango cha juu cha mwendo ni 80km/h, isiiwe hivyo kwa vyombo vyote vya moto barabarani?

Kwa kuzingatia haya tu, ajali zitakwisha.

Serikali inao wajibu.
Hakuna suggestive solutions za kumaliza au kupunguza ajali kwenye hizi hoja hapa.
 
Mtoa mada anataka iwepo tuition ya ku overtake tena ifundishwe na graduates.
Mkuu tuition wala haisaidii. Imekuwa miaka mingi mno. Bora graduates wakamate usukani wenyewe kabisa.
 
Umenena vyema lakini umetoa majawabu mengine yasiyo sahihi!

Halafu,haiwezekani ajali kwisha. Lengo la kifanyia kazi ni kuzipunguza kabisa.

Siku za nyuma ajali zilikuwa zinaonekana chache kwa kuwa magari yalikuwa machache na movement ya watu ilikuwa ndogo kutokana na vipato duni na kukosekana shughuli nyingi za kiuchumi. Siku hizi magari na vyombo vingine vya moto vimeongezeka mno barabani!
Ni kweli magari yamekuwa mengi lakini sio kwamba ndio sababu ya ajali kuwa nyingi !! Swali langu ni moja tu-: Je madereva kugongana uso kwa uso huwa inasababishwa na magari kuwa mengi barabarani au ni uzembe tu wa madereva husika ?! Dereva wa gari A ana macho na anakutana na dereva wa gari B naye pia ana macho ni kitu gani kinachosababisha gari wanazoziendesha zigongane uso kwa uso ??!! Jibu nililonalo mimi ni kwamba mmoja wao au wote Wawili huwa hawazitumii akili zao inavyotakiwa wanapoendesha magari yao !! Na hiyo mara nyingi husababishwa na kuamini ulevi fulani fulani unampa ujasiri na nguvu awapo barabarani huyo dereva !!
 
Back
Top Bottom