Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

M/Mungu awajaalie moyo wa subira na uvumilivu wazazi wote waliopoteza watoto na watoto waliopoteza wazazi (walimu waliofariki) ni Kipindi kigumu sana hiki lakini hili nalo litapita Allah awajaalie uvumilivu Amin
 
[emoji24] [emoji24] R.I.P teachers and pupils
 
Ni kweli aseee.
Pole kwa majeruhi pole kwa familia zao
Na kama wapo waliopoteza maisha Mungu azilaze mahali pema roho za marehem kwan bado n wadogo na hawana dhambi.
Inauma sn jaman.
 
Inasikitisha sana..

Ingawa ajali haina kinga... Na kifo hakina hakina hodi... Ni ni shida sana kusafiria magari mabovu...

Shule nyingi kwenye ziara za kusafiri eneo moja kwenda jingine, wanakodisha magari ambayo yapo tayari kwa safari za mbali...


Cc: mahondaw

May their souls rest in peace. AMEN
 
Ajali haina kinga ila MWENDOKASI nao majanga
Tuwaombee wazazi wote wawe wavumilivu kipindi hili kigumu poleni sana Ameen
Hapo sio mwendo kas n miundo mbinu ya barabara na mvua hizi ndio balaa kabisa..Mungu tuepushie zimwi hili la ajali
 
Dah RIP na pole kwa wafiwa wote .

Habari mbaya sana, mpaka sasa hakuna chombo cha habari chochote kilicholipa jambo hili uzito .[HASHTAG]#OnlyInTanzania[/HASHTAG]

Acha uongo. JF ni chombo cha nini? ITV wameripoti tena kistaarabu - hawajaonyesha picha wala kuzusha idadi ya majeruhi na wafu wala sababu ya ajali.
 
Hizi shule ziache ubahili, we Costa gani ina uwezo wa kubeba abiria 58, hapo hata ikitokea ajali ndogo lazima mfe tu kwanza mnabanana, hewa yenyewe inakuwa hamna hapa shule inabidi iwajibike. Mimi mwaka juzi nilisafirisha msiba kwenye Costa tulikuwa 28, sasa wao wamewabana watoto mpaka wamefikia 58, ili wapige ela. RIP
 
Hii ajali ni mbaya sana na inasikitisha Sana.

Majira haya ya Mvua kuwasafirisha Watoto si busara hata kidogo.
 
Acha uongo. JF ni chombo cha nini? ITV wameripoti tena kistaarabu - hawajaonyesha picha wala kuzusha idadi ya majeruhi na wafu wala sababu ya ajali.
Nimesema hakuna chombo cha habari kilicholipa hili jambo uzito sio kwamba hawajaripoti, jaribu kuelewa kabla ya kukurupuka.. JF haiwezi kufika kwa watu wengi kama radio na TV

Anyways hakuna haja ya kubishana mkuu, tuko msibani. [HASHTAG]#Pamoja[/HASHTAG]
 
Sasa safari hiyo ukute hawana kibali. Shule itakuwa matatani. Vijipesa hivi walimu tuangalie coster ni watu 25.unaweka zaidi YA 30 shídaa
Kama ni watoto wadogo wanaweza kukaa wa4 katika siti ya watu wawili kwa hyo 25*2 mkuu!Tuombe subra kwa walimu na wazazi mkuu sio mda wa lawama huu,walimu wameumia sana pia maana mda mwingi sana wanakaa na watoto wetu,siku 5 sisi siku moja kwa ajili ya kuhangaika,mtoto aliyezowea kumuona kila siku kwa mwezi siku kama 22 asimuone tena milele,poleni walimu wa shule tajwa,na hongereni kwa jukumu kubwa LA kutuangalizia,kulea,kuwashape watoto wetu wakati sisi tunahangaika!
 
napafahamu mahali pale ni kona kali na korongo baya upande kushoto. overspeeding kwa kona hiyo ni ajali. nilishapoteza Baba mdogo hapo kwa style hiyo hiyo. madereva wa tours wanapajua sana.
 
Wapumzike kwa amani..


Kuna kona flani zipo kwenye kilima ukiwa unatoka Mto wa mbu kwenda Karatu...Dereva akikosea tuu pale haponagi mtu..
 
Back
Top Bottom