khamis lyaheja
New Member
- Feb 5, 2017
- 3
- 9
Mungu awalaze mahala pema
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu pole sana kwa kuyajua maumivu hayo,maelezo yako yamenitoa machozi kwa kweli,tunahangaika sana na hawa watoto wao hawajui tu,wakienda trip huna amani wala furaha hadi watakaporudi salama,natamani kuwakataza wakiniambiaga,lakini huzuni wanayokuwa wanananionyesha na wanajua ninauwezo wakuwalipia,huwa naumia sana,nikiwaruhusu hawajui maumivu ninayokuwa nayo mm hadi warudidah ndio maana mimi watoto wakinambiaga maswala ya kwenda ziara nawakataliaga kwa sabab ya vitu kama hivi ila kwakuwa wao hawajui waniita mkoloni yan inafikia hatua wakiwa wananiulizia wanasema"mama,mzee mkuda yupo ndani au bado hajaludi"........dah maumiv ya kupoteza mtoto ni mazito jaman mi yashanikuta !
yan mimi watoto wakinambiaga haya mambo ya ziara nawauliza mchango ni tsh ngap wakishanambia nawapa hiyo pesa nawawambia nendeni mkatembee kuna siku mtoto alijibu jibu flan sitasahau,alinijibu"baba wewe sio mzee ila mbona una mambo ya kikoloni hivo,ungekuwa unatukataza bila kutupa hizi pesa ambazo zingekuwa ghalama ya trip tungehisi m'bahili"
Wakuu habari za leo,
Muda huu kuna ajali mbaya imetokea maeneo ya karatu basi la shule limeanguka kabla ya kuingia karatu mjini na kuua watoto wengi ambao idadi yake bado haijafahamika. Wanafunzi hao wanaokadiriwa kuwa wa darasa la 7 inasemekana ni wa shule inayoitwa Lucky Vicent ya Arusha ambao walikua wanaenda karatu kufanya mitihani ya mashindano na shule za karatu. Kwa mujibu wa shuhuda basi hilo lilikua limebeba watoto zaidi ya 40 na wengi wao (zaidi ya nusu) inasemekana wamepoteza maisha akiwemo dereva na walimu.
Ntawapa updates soon nipo jirani na eneo la tukio na mvua inanyesha sana nimeshindwa kutoka kufika eneo la tukio.
Tuendelee kuwaombea
Hata private, ikifika imefika japo public ni kizunguzunguHabari mbaya sana, poleni wazazi mm ni mmoja wa wazazi ambaye sipendi kabisa vi trip vya pamoja iwe ni kwa watu wazima au watoto i prefer private transport
Inasikitisha sana .. Hili ni janga la taifa, vifo zaid ya 50 ni vingi sana. tena mbaya zaid ni vya watoto wadogo.Tbc wanaonesha Bongo muvi! Polen sana wafiwa
Ni nadra binadam wooote wakafariki lazima wawili watatu Mungu anaweza kuwanusuru.Nimepata habari isiyo na shaka kuwa gari aina ya coaster limeua watoto karibu wote waliokuwa wanaelekea mjini Karatu kwa ziara ya kimasomo, taarifa zinasema wamebaki watoto wawili tu wengine wamefariki, shule inaitwa Lucky Vincent Nursery & Primary School ipo Arusha ni medium schools,kwa wenye updates tunaomba mtupe
Picha: Soon ntaziapload ni ajali ya mda huu
Mungu awalaze mahali pema peponi
----------------------
UPDATE: Coaster ina jumla ya abiria 58 na wote wanasadikiwa wamefariki,maiti zimepelekwa hospitalini na watu wameondoka eneo la tukio,mvua inanyesha
UPDATE: Picha zinakuja soon ripota yuko eneo la tukio..
![]()
.........................
UPDATES:Magari ya polisi yametanda kila kona na maiti zimebebwa na magari ya polisi
Tayari kuhifadhiwa
...................
UPDATES:Ni watoto wanne(4) wanasadikiwa wako hai ila wako mahututi kabisa na kuna wasi wasi vifo vikaongezeka
UPDATES:Lucky vincent nursery school bus![]()
UPDATES:Shughuli za uokozi
![]()