Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Asante sana ndugu yangu. Acha tu ni Kama ndoto ambayo tunaomba tuamke usingizini tukute sio kweli. Kaka Presha imepanda kaanguka yuko hospital hajaamka mpaka sasa. Amezika MKE wake mwezi wa pili mwaka huu.
Durtete, pole sana. Hebu kuwa jasiri umfariji kaka yako. Ajali hii imenihuzunisha sana. Pole, pole sana.
 
Acha kuleta fikra shirikishi.
Watoto wetu wapumzike kwa amani wakiutazamia ufufuo.
Hata Mimi nilijiuliza nilipoona bus ilivyo haikuumia sana haswa kuanzia kati kurudi nyuma utaona kabisa kuwa idadi kubwa ya vifo imechangiwa na abiria kutokufunga mikanda nadhani idadi ilikuwa kubwa compared to idadi ya seat (hiyo ni kawaida kwa trip za watoto) unaweza kuta seat Moja was shared.
 
Asante sana ndugu yangu. Acha tu ni Kama ndoto ambayo tunaomba tuamke usingizini tukute sio kweli. Kaka Presha imepanda kaanguka yuko hospital hajaamka mpaka sasa. Amezika MKE wake mwezi wa pili mwaka huu.
So sad! Mwenyezi Mungu awape uvumilivu ktk kipindi hiki kigumu!
 
Mkuu yaani acha tu, kuna ajali nyingine ilitokea mbeya sehemu inaitwa songwe, watu walipitiwa na train walikuwa wamekaa kwenye mkutono wa dini maspeaker yalikuwa makubwa hawakusukia!! Cha ajabu hakukuwa na damu
 
Haya maeneo yana kona Kali sana... Na hii mvua sio rafiki sana maeneo yenye kona kali... Looh! Inasikitisha saana. Wazazi poleni sana, maana najua maumivu haya, na sio kwa wazazi wa watoto hawa tu, bali maumivu haya ni kwa wazazi wote Tanzania na Dunia nzma... Roho za marehemu wapumzike kwa amani na wapate rehema kwa Mungu... Amen.
Ingawa sio mwenyeji lakini naona kama watu wamesimama kwenye lami, au nakosea
 
Mungu awape nguvu familia za hawa watoto. inaumiza sana kupoteza kizazi kijacho wengi mamna hii.

Imeniuma hadi machozi yamenitoka.

Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema peponi.
 
Durtete, pole sana. Hebu kuwa jasiri umfariji kaka yako. Ajali hii imenihuzunisha sana. Pole, pole sana.
Asante sana mkuu. Ndio maana nimesafiri mara tu nilipopata taarifa. Ndugu zangu wengine bado hawaamini na hawataki kuamini. Kaka alikuwa na watoto hao hao ndio walikuwa wanampa faraja baada ya mke wake kuitwa na Mungu mwezi wa pili mwaka huu.
 
Back
Top Bottom