Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Ndugu zangu kuna taarifa nimezipat muda sio mrefu ajali imetokea rotia, basi la wanafunzi wa lucky vincent school kwa morombo. wanafunzi walikuwa wanakwenda kufanya mtihani wa ujirani mwema sasa kama kuna mtu anamwanafunzi pale afuatilie kwasasa ili kupata habari za uwakika.

 
Maskini vitoto vizuri vidogo,vilivyokuwa vikipendeza,vimepotezwa maisha yao,na dereva asifuata sheria za barabarani.Mlale salama watoto wazuri.Poleni sana wafiwa wrote.Huu ni msiba wa wapenda watoto wote duniani.
 
Poleni Sana waliofikwa na msiba huu mkubwa.

Wote waliofariki, Roho zao zipumzike kwa amani!
 
Nilivyosoma kichwa cha habari tuu kidogo nipoteze fahamu watoto wangu wanasoma hapo ila bado hawajafika la saba.

Siwezi kuamini kuwa huyo ni Mungu ndio kawachukua haoo watoto kwa style hiyo nooo that's the devil's work, Mungu atusaidie na Hawa watoa makafara jamani very sad
 
Asante sana ndugu yangu. Acha tu ni Kama ndoto ambayo tunaomba tuamke usingizini tukute sio kweli. Kaka Presha imepanda kaanguka yuko hospital hajaamka mpaka sasa. Amezika MKE wake mwezi wa pili mwaka huu.
Aisee inapain sana kk!! Yaani habari mbaya kama hizi sisikie tu, lakini ikikukuta!! Mungu ndio anajua! Niseme tu kuwa Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina
 
Habari mbaya sana, poleni wazazi mm ni mmoja wa wazazi ambaye sipendi kabisa vi trip vya pamoja iwe ni kwa watu wazima au watoto i prefer private transport
Mkuu ajali inatokea muda wowote kwa mtu yeyote unaweza ukawa na gari lako binafsi ukasafiri nalo kama imepangwa kutokea itatokea tu cha muhimu mungu aweke roho zao mahali pema.
 
Unayajua maumivu ya Kupoteza mtoto?ukipoteza mtoto unafikiria mengi anapokuaga japo huwezi kumkinga na chochote,huwa unahisi unamuepusha,mshikaji sio mkoloni,tahadhari tu kama mzazi amewahi kupoteza mtoto hujui kwa mazingira gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…