Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Maskini vitoto vizuri vidogo,vilivyokuwa vikipendeza,vimepotezwa maisha yao,na dereva asifuata sheria za barabarani.Mlale salama watoto wazuri.Poleni sana wafiwa wrote.Huu ni msiba wa wapenda watoto wote duniani.
Poleni sana wazazi na ndugu,taifa limepoteza nguvu kazi ya kesho. RIP watoto wetu.
 
Sometimes unakosa hata cha kusema.so sad,inawezekana hakukua na kosa lolote kutoka kwa dereva wala yeyote.vitu vingine hutokea tu,for his will,Almighty God.RiP watoto na wazazi garini...
 
Nimepata habari isiyo na shaka kuwa gari aina ya coaster limeua watoto karibu wote waliokuwa wanaelekea mjini Karatu kwa ziara ya kimasomo including(joint examinations), taarifa zinasema wamebaki watoto(3) tu wengine wamefariki,

shule inaitwa Lucky Vincent Nursery & Primary School ipo Arusha ni medium schools,kwa wenye updates tunaomba mtupe

Picha: Soon nitaziapload ni ajali ya muda huu
Mungu awalaze mahali pema peponi
----------------------

UPDATE: Coaster inasadikiwa kuwa na zaidi ya abiria 30 na wote wanasadikiwa wamefariki,maiti zimepelekwa hospitalini na watu wameondoka eneo la tukio,mvua inanyesha

UPDATE: Picha zinakuja soon ripota yuko eneo la tukio..

19a4fcd1c935e4c031670cd880a46bc5.jpg

.........................
UPDATES:Magari ya polisi yametanda kila kona na maiti zimebebwa na magari ya polisi
Tayari kuhifadhiwa
...................
UPDATES:Ni watoto watatu (3) wanasadikiwa wako hai ila wako mahututi kabisa na kuna wasiwasi vifo vikaongezeka
UPDATES:Lucky vincent nursery school bus
62d62ef75dec257e496254f5cfb2808e.jpg

UPDATES:Shughuli za uokozi
a198eaa3cab45eec73b51943888b0a63.jpg

UPDATES:Gari lilikuwa na zaidi ya abiria 30 wanafunzi 25,waalimu (4) wote wa kiume na dereva 1
................
UPDATES:Kati ya majeruhi watoto watatu(3) wawili wako mahututi kabisa na mmoja amepasuka kichwa
................
UPDATES:Maajabu ya ajali hakuna damu zozote zilizotapakaa licha ya watu wengi sana kufa!
..................
UPDATES:Majeruhi mmoja kati ya( 3) amefariki kabla ya kufikishwa hospitali,kwa hiyo taarifa zinasema wamebaki majeruhi wawili walioko ICU
...............
UPDATES:Kuna mkanganyiko mwingi kuhusu chanzo cha ajali ila nature ya eneo la ajali ni mteremko mkali na kuna daraja,ni eneo ambalo dereva anatakiwa kuwa makini kabisa,kwa dareva asiyemwangalifu inaweza tokea lolote,hebu angalia hapo gari lilipotumbukia na haikuwa ina over take ,u can diagnose the nature of an accident
efc42e9814d84a123b6aa5a8a92fed7c.jpg

UPDATES:Mwonekano wa gari kwa mbele baada ya kupata ajali
1b9b2ef92a5648b20c71d3e04a5e5f65.jpg

UPDATES:RPC Wa arusha amethibitisha jumla ya vifo 31 vya waalimu na wanafunzi


R.I.P all

Client:Jf member
Ajali imetokea eneo gani?
 
Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi marehemu hao,Awaswamehe madhambi yao makubwa kwa madogo,
 
walikuwa darasa la saba nasikia wanaenda kwa mitihani ya interschool
 
Hilo gari imekuwaje hadi wa nyuma wamekufa wakati linaonesha nyuma pako vizuri sana?
 
Innallillah wainaIllah Raji'un. Duh! speechless. Allah Awatie nguvu wazazi/walezi wa marehemu. Kipindi kigumu sana ktk maisha ya kiuzazi!!
 
Hilo gari imekuwaje hadi wa nyuma wamekufa wakati linaonesha nyuma pako vizuri sana?
Mkuu hayo ni madhara ya kutokufunga mikanda pia kama ajali ikitokea na ikacrush kwa impact kubwa hata siti za nyuma hungoka
 
Kwa muonekano wa hiyo gari, haikupaswa kuuwa watu wote hao..... maana nyuma ni nzima kabisa.

R.I.P wanafunzi......pole kwa wazazi ndugu Jamaa na marafiki na Taifa kwa ujumla.
Kwa hiyo inawezekana hawakufunga mikanda, gari ilipojibamiza kwa mbele, backbenchers woote wakarushwa kwenda mbele!!
Ila ndo yameshatokea
 
HIVI MAANA YA KUTOA MAPICHAPICHA YA MAREHEMU NI NINI??? HAKUNA HAJA YA KUTOA HAYO MAPICHA, TUMESHAJUA KUNA AJALI YA WATOTO WA SHULE FULANI, TUMESHAJUA IDADI INATOSHA.
 
Kazi ya shetani katika jina la Yesu Kristo ikashindwe kwa Majeruhi.
 
Back
Top Bottom