Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Mwenyezi Mungu azilaze mahala Pema roho za wanafunzi na walimu waliopata ajali hiyo na awatie nguvu wazazi/walezi katika kipindi kigumu cha msiba.
Amin
 
Pole kwa wafiwa, ni msiba mzito kwa taifa, changamoto kwa kamanda Mpinga, kamanda elewa kuwa vijana wako wanaruhusu magari mabovu kutembea. Kama Mh rais ametumbua watumishi wasio na sifa, wewe unashindwa nini kuzuia magari yasiyo na sifa?
Shida sidhani kama ni ubora wa gari....uzoefu wa dereva na eneo husika ndo tatizo. Lile eneo alitaki mwendo kasi....pamoja na ule mteremko kua mkali pia kulikua na mvua.... kama sio mzoefu na idadi kuzidi shida ndo ipo hapo.
 
Aliyepost aache ukuda na upumbavu unaweka siasa kwene mambo ya misiba jinga kabisa kaa bashite akipima akili yako
 
Mods mtarekebisha baada ya Vilio vingi heading ya Mwananchi ni hii hapa chini


"Lowassa awalilia wanafunzi, maiti 32 zapelekwa mochwari''
Ww kijana ni mpumbavu sana,hata kama ni uvyama huu unaofanya ni upumbavu,acha kua mpumbavu kiasi hiki kweny mambo yasiyohitaji siasa,jielewe,mjinga sana ww
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward
Lowassa ametuma salamu za rambi
rambi kutokana na tukio la watu 32
kufariki dunia katika ajali ya basi.
Waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Karatu, ni wanafunzi 29, walimu wawili, pamoja na dereva wa gari hilo.


“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo, ni ajali mbaya ambayo inaifanya siku hii kuwa mbaya katika
historia ya nchi yetu,”alisema Miongoni mwa wanafunzi waliofariki ni pamoja na wanaume 11 na wasichana 18.

Kadhalika maiti 32 zikiwamo za walimu wawili, dereva mmoja na wanafunzi 29 zimepokelewa sasa hivi katika Hospitali ya Lutheran Karatu.

Chanzo: Mwananchi.
We mngese nn heading gani hii?
 
Asee ni mbaya sana hii, yawezekana hao ndio wengi wao walikua vichwa darasani asee Mungu awape pumziko la amani.
 
Dunia inajua na Chadema wanajua huwezi Kutenganisha Ufisadi na Lowassa.
Hiyo heading imenifanya nicheke! Ingawa nilikuwa nawalilia ndugu zangu! Haki ya Mola!
 
Yule bwana aliyejinywea uji wa wagonjwa hajawalilia hawa wanafunzi?
 
Back
Top Bottom