Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

*Habar za hivi punde kutoka Hospital ya Lutheran Karatu maiti zilizopokelewa hapo hospitali ni maiti 32 miongoni mwao waalimu ni 2 dereva 1 na wanafunzi 29 ambapo wanafunzi wa kiume 11 na wasichana 18 nakufanya jumla hiyo ya maiti 32*
 
Poleni sana wafiwa na marehemu wapumzike kwa amani.
 
Madereva hawa wa school bus ni majanga wengine huwa wanawanajisi/wabaka watoto.
 
Asante sana ndugu yangu. Acha tu ni Kama ndoto ambayo tunaomba tuamke usingizini tukute sio kweli. Kaka Presha imepanda kaanguka yuko hospital hajaamka mpaka sasa. Amezika MKE wake mwezi wa pili mwaka huu.
Pole sana mdau....
 
Asante sana mkuu. Ndio maana nimesafiri mara tu nilipopata taarifa. Ndugu zangu wengine bado hawaamini na hawataki kuamini. Kaka alikuwa na watoto hao hao ndio walikuwa wanampa faraja baada ya mke wake kuitwa na Mungu mwezi wa pili mwaka huu.
Unakuja arsh sehemu gani? Tunaweza kua ni majirani
 
Hiyo gari ilivyo sio ya kuuwa wote hao... Kuna ushetani tu hapo
Masomo ya sayansi hapa ndio umuhimu wake hujitokeza.
Impact ya gari ilisababisha movement ya objects zilizokuwa ndani ya gari (ambao ndio wapendwa watoto wetu) ambao nao walikuwa impacted kwenye gari kwa speed ya escaping velocity.

Tubuni kwa maana hamuijui siku wala saa.
 
Dah kweli inauma sana. Hadi machozi yamenitoka. Inauma sana. Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema. Amen
 
Mimi anani changanya anaposema wamekufa wote....
Mara aseme kuna majeruhi 3.
Mara abadilishe aseme majeruhi ni 4.
Yaani kaandika habari kwa mihemko ya kipumbavu.

Wewe ndio unahemka. Hii ni breaking news... sio habari kamili. Kwa habari kamili subiri official statement kuhusiana na ajali kutoka polisi, shuleni au mamlaka nyingine zinazohusika.
 
Asante sana ndugu yangu. Acha tu ni Kama ndoto ambayo tunaomba tuamke usingizini tukute sio kweli. Kaka Presha imepanda kaanguka yuko hospital hajaamka mpaka sasa. Amezika MKE wake mwezi wa pili mwaka huu.
Pole sana mkuu Mungu pekee ndio faraja yetu anayajua mawazo yetu,anaijua kesho yetu pia ni yeye pekee anayejua kwanini kaka anapitia ktk mapito magumu kiasi hichi, basi yeye akawe faraja kwenu hasa ktk kipindi hiki kigumu na akamfute kaka machozi na kumuwezesha kusimama tena na pia ampe dogo pumziko jema la milele "Amina"
 
Mungu awatie nguvu sana maana!!!!... Mungu atupe ulinzi kwakweli.....R.I.P kwa wote waliokatishwa safari ya kuishi duniani
 
Masomo ya sayansi hapa ndio umuhimu wake hujitokeza.
Impact ya gari ilisababisha movement ya objects zilizokuwa ndani ya gari (ambao ndio wapendwa watoto wetu) ambao nao walikuwa impacted kwenye gari kwa speed ya escaping velocity.

Tubuni kwa maana hamuijui siku wala saa.
kwa jinsi ilivyokita haponi mtu, tatizo school bus zinahesabika kama private transport na madereva wake wanakuwa na leseni za chini sana,
 
Pole wazazi jamanii Poleni shule husikaa Poleni watoto mmekwenda wadogooo kifo wee kifoo huna hurumaaa
 
Back
Top Bottom