Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Wewe nawe kumbe ni **** kabisa.
Kama mtu hana uhakika na habari kwanini atunge mara wamekufa wote 30, Mara aseme kuna majeruhi 3, Mara 4.

Kwanini usiseme tu idadi kamili ya vifo na majeruhi siijui.

Logic! funga safari nenda eneo la tukio ukajue hali na idadi halisi. Hizi habari zilizo'vunjika' ziache kama zilivyo.
 
2fb23bb2252b031205d611c151f8ddc0.jpg
591ad809f403c64e13cfbf47baad90cc.jpg
Guga ni karatu sehemu gani?
 
Niko njiani kuelekea Arusha. Nimefiwa na watoto wa kaka yangu wawili katika hiyo ajali. Mungu atupatie wepesi.
Aisee poleni sana, nashindwa ku imagine hali za hao wazazi Mungu awasaidie katika hiki kipindi kigumu
napafahamu mahali pale ni kona kali na korongo baya upande kushoto. overspeeding kwa kona hiyo ni ajali. nilishapoteza Baba mdogo hapo kwa style hiyo hiyo. madereva wa tours wanapajua sana.
 
ukitaka kugombana na mtoto mkataze kwenda hizo tour sijui walimu wanawapaga nini watoto?
Poleni sana wafiwa mdau hata wewe ulipitia huko kwa hiyo tusianze kunyoosheana vidole na wale wanaopigwa na radi huko kigoma nao wasiende shule
 
Kwa muonekano wa hiyo gari, haikupaswa kuuwa watu wote hao..... maana nyuma ni nzima kabisa.

R.I.P wanafunzi......pole kwa wazazi ndugu Jamaa na marafiki na Taifa kwa ujumla.
 
Asante sana mkuu. Ndio maana nimesafiri mara tu nilipopata taarifa. Ndugu zangu wengine bado hawaamini na hawataki kuamini. Kaka alikuwa na watoto hao hao ndio walikuwa wanampa faraja baada ya mke wake kuitwa na Mungu mwezi wa pili mwaka huu.
Jamani mbona hili ni zaidi ya jaribu kwake mke kapoteza leo na watoto wawili... Mungu mtazame huyu baba mateso anayopitia ni mazito
 
Back
Top Bottom