Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ametuma salamu za rambi rambi kutokana na tukio la watu 32 kufariki dunia katika ajali ya basi.

Waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Karatu, ni wanafunzi 29, walimu wawili, pamoja na dereva wa gari hilo.


“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo, ni ajali mbaya ambayo inaifanya siku hii kuwa mbaya katika historia ya nchi yetu,”alisema Miongoni mwa wanafunzi waliofariki ni pamoja na wanaume 11 na wasichana 18.

Kadhalika maiti 32 zikiwamo za walimu wawili, dereva mmoja na wanafunzi 29 zimepokelewa sasa hivi katika Hospitali ya Lutheran Karatu.

Chanzo: Mwananchi.
 
Safi sana kwa uwepesi wake wa kutoa pole . Uungwana ni vitendo.
 
Badilisha heading mkuu ila habari ibaki hivyohivyo
 
b4553912f67830f44b764c8c198a7b2d.jpg
 
Huyu ni moja ya majeruhi, haamini na wala hawezi kuongea chochote
 
Oooh God... I know the place..... Hali ya kule ya ukungu itakua imesababisha... Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi
 
Back
Top Bottom