Waziri Mkuu Mstaafu, Edward
Lowassa ametuma salamu za rambi
rambi kutokana na tukio la watu 32
kufariki dunia katika ajali ya basi.
Waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Karatu, ni wanafunzi 29, walimu wawili, pamoja na dereva wa gari hilo.
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo, ni ajali mbaya ambayo inaifanya siku hii kuwa mbaya katika
historia ya nchi yetu,”alisema Miongoni mwa wanafunzi waliofariki ni pamoja na wanaume 11 na wasichana 18.
Kadhalika maiti 32 zikiwamo za walimu wawili, dereva mmoja na wanafunzi 29 zimepokelewa sasa hivi katika Hospitali ya Lutheran Karatu.
Chanzo: Mwananchi.