Ajali ya Magari 13 Msafara wa Makonda; Tusome Alama za Nyakati

"Initial assessment" ni kwamba hayo magari yote yalikuwa kwenye mwendo mkali.

Njia yenyewe ni mabonde na si lami hivyo gari ya kwanza kugota au kusimama ghafla likazua balaa nyuma yake.

Kutokana na wingi wa vumbi kuu magari mengine yalokuwa nyuma ya gari ya kwanza yote ikabidi yagongane na kwa kuwa yalikuwa katika mwendo mkali hakukuwa na muda wa kusimama.

Tusilaumu uchawi wala ulozi bali ujinga wa baadhi ya watanzania wenzetu ambao wameamua kuweka maarifa pembeni.

Njia na barabara hazina lami bali mabonde kwanini kuwepo mashindano kama tupo kwenye jangwa la Sahara?
 
Haya anayofanya Zerobrain Bashite hayana baraka za Mwenyezi Mungu. Kama kuna wanaojua alama za nyakati, kuna ujumbe kwenye ajali hii...!!!

Ujumbe ni mmoja tuu ziara yote imeharibikia hapo zile post za kumsifu zimekoma sasa ni mjadala wa ajali



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndie kichwani hamna kitu yeye anafuatilia utekelezaji wa ilani ya chama
 
Katika video hiyo nacho kuona ni uzembe wa madereva kuendesha kwa kasi bila kujali speed au stopping distance na kutokuwa na awareness wakati wa uendeshaji ndio maana wa nyuma akamgonga wa mbele na kuendelea…bima ndio itakula hasara hapo…polisi pia iwachukulie hatua hao madereva kwa kutofuata speed limits ktk barabara za aina hiyo…
 
Hii mikoa ya kusini ndo maana hainaga maendeleo sababu ya uchawi! Alienda Magufuli wakampulizia moshi msafara wake, baada ya hapo afya yake ikadolola mpaka akafariki!
Great thinker huyo tayari ameshakimbilia kwenye uchawi kisa msururu wa magari zaidi ya ishirini unaokimbia kasi katika barabara yenye vumbi kupata ajali........TAIFA HILI KAZI IPO!!!

Great thinker huyo amekariri stori za miaka ya 70 na 80 huko (enzi za ujinga kwa watz) kuhusu watu wa kusini. Yaani kweli tz hii kuna mtu mwenye ujasiri kabsaaa wa kuzizodoa sehemu zilizoendelea na zisizoendelea?!!!! Hv ni wapo huko kumeendelea tukimbilie wadau?!!! Nipo chalinze hapa hali si hali
 
Kwani Mwenezi wa CCM ni nani katika nchi hii hadi afuatane na msafara wa magari kiasi hicho.

Huu ni UJINGA tunaulea, na tusipochukua hatua basi kuna damu nyingi zitamwagika kwa ajili tu ya kumshabikia huyu BAZAZI Makonda
 
Awajibishwe Paulo Makonda:

 
Awajibishwe Paulo Makonda:

View attachment 2901386
Gari la Serikali kwenye msafara wa Bashite???
Niko wilaya ya Kinondoni ambapo last months alitangaza hdharani kuwa atamkabidhi Mbunge Gwajima wa jimbo la kawe makatapila 20. Nimetembea na kuuliza kila mtaa, hakuna katapila lolote limepokelewa.

Kama kuna wafanyakazi wanatetemeka ujio wa Makonda basi ujuwe wafanyakazi hao ni MBURURA, yaani hawajitambui

Bashite ni Zerobrain, hakuna lolote atakisaidia CCM kwa hizo ziara zake
 
Mkuu, hii inasikitisha na kutia hasira sana, yaani unashindwa kuelewa anayeyabariki haya yote ana nia gani haswa.
 

Awajibishwe Paulo Makonda Kwa uharibifu huu:

 
Hamnaga hoja upinzani sijui mnashida ipi?...Ziara hazina tija mbona wew ndio zero brain sas.Mtu kabaini utendaji mmbovu wa DED huko tanga unakuja kusema ziara haina tija
 
Kwani hizo garama ni za kwako ama za chama waswahili mbona mnajiaibisha hivi..akina mbowe wakifanya ziara na mahelkopta wanatumiaga makaratasi sio.

Mbali na CCM kuwa ndio chama chenye serikali hivyo kinayo mamlaka ya kwenda mahali popote na watendaji wa serikali ili kutatua kero mbona uulizi gari za umma zinafata nin kweny misafara ya akina mbowe ama hizo gari za polisi ni gari zako
 
Anachoma fedha za serikali, halafu akifika mikutanoni analia kwamba yeye ni wa masikini na wanyonge. Bilions za serikali zinateketea katika msafara wake, akifika mkutanoni anampiga mkwara Mkurugenzi wa Halmashauri kwa nini hajamlipa mkandarasi milioni tano!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…