Matumizi mabaya sana ya fedha na rasilimali za Umma.
Magari ya Serikali yanafanya nini katika msafara wa Chama? Nani anaidhinisha haya kutokea.
Kuna vituo vya afya havina vitanda vya akina mama kujifungulia.
Kuna vituo vya Afya havina Solar
Kuna maeneo Wazazi hawawezi kununua vifurushi vya kujifungulia.
Kuna shule zimesimama kwa miti hata kuziita shule ulimi unasita. Kuna matatizo mengi sana kwa Wananchi.
Msafara wa DAB unatumia mafuta kiasi gani! kuna Watu hawana pesa za kutoa miili ya Wapendwa ' pasimoto'
Leo magari zaidi ya 10 yanakuwa '' written off'' kesho tunaagiza mengine.
DAB anafaida gani katika Taifa hili kiasi cha kuruhusiwa kufuja mali za Umma kiasi hicho.
Miaka 60 ya CCM sisi ni masikini duniani! hapana si masikini wa rasilimali, ni masikini wa akili
JokaKuu Pascal Mayalla