KERO Responded Ajira Mpya (Walimu) Temeke tuliwekewa Laki 9, tukaambiwa ni nauli, sasa hivi wanatuambia turudishe

KERO Responded Ajira Mpya (Walimu) Temeke tuliwekewa Laki 9, tukaambiwa ni nauli, sasa hivi wanatuambia turudishe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mwajiriwa Mpya Manispaa ya TEMEKE, Dar es Salaam, March 6, 2026 tuliwekewa fedha kwenye account zetu waajiriwa wapya Idara ya Msingi, jumla ya Walimu 77 tuliwekewa fedha kwa wastani kila mmoja alipata laki tisa na point.

Hatukujua nini, kuna baadhi ya wenzetu walijaribu kupiga simu wakaambiwa ni nauli, imekaa hivyo sasa tunaitwa tunaambiwa turudishe, tunafokewa, tunaitwa wezi, kana kwamba sisi tulienda kutaka hizo hela.

Wanasema walikosea kuweka, basi kama walikosea watuwekee utaratibu mzuri wa kurudisha lakini tunafokewa, tunatukanwa ukizingatia sisi ni ajira mpya.

Sijui walikosea kweli au waliwekeza kwetu ili baadaye wachukue, tunapewa maelezo hayo kwa mdomo tu na hela tulipewa kimyakimya bila nyaraka yoyote, ni Ajira Mpya Mwaka 2025.

Tunafanya kazi bila uhuru, tusaidieni ujumbe huu ufike kwa Wakubwa wajue tunachopitia.

Ufafanuzi wa Manispaa ~ Temeke DC yafafanua Watumishi kuingiziwa fedha kisha kuambiwa wazirudishe, yaelezwa ziliingizwa kimakosa
 
Watumishi kada ya ualimu ni wapuuzi kabisa
Kwani hamzijui haki zenu???!
 
Mi nisharudisha mkuu mana ajira yenyew nimeipata kwa tabu wasiniletee mbilinge na mizengwe nikarudi mtaani
 
Ulishawahi kutumiwa pesa na mtu unayemfahamu halafu muda huohuo wale wahuni wa "tuma kwa namba hii" wakakupigia kwamba urudishe pesa na kwamba imekuja kwako kimakosa?
 
Mimi ni mwajiriwa Mpya Manispaa ya TEMEKE, Dar es Salaam, March 6, 2026 tuliwekewa fedha kwenye account zetu waajiriwa wapya Idara ya Msingi, jumla ya Walimu 77 tuliwekewa fedha kwa wastani kila mmoja alipata laki tisa na point.

Hatukujua nini, kuna baadhi ya wenzetu walijaribu kupiga simu wakaambiwa ni nauli, imekaa hivyo sasa tunaitwa tunaambiwa turudishe, tunafokewa, tunaitwa wezi, kana kwamba sisi tulienda kutaka hizo hela.

Wanasema walikosea kuweka, basi kama walikosea watuwekee utaratibu mzuri wa kurudisha lakini tunafokewa, tunatukanwa ukizingatia sisi ni ajira mpya.

Sijui walikosea kweli au waliwekeza kwetu ili baadaye wachukue, tunapewa maelezo hayo kwa mdomo tu na hela tulipewa kimyakimya bila nyaraka yoyote, ni Ajira Mpya Mwaka 2025.

Tunafanya kazi bila uhuru, tusaidieni ujumbe huu ufike kwa Wakubwa wajue tunachopitia.
Msirudishe.Mbona Yanga hawajarudisha walizozidishiwa?Acheni ufala!Mkirudisha tu muhame mrudi vijijini kwenu.Hamkuiba.
 
Tofauti na hyo laki tisa je mlilipwa hela ya kujikimu?

Kama waliwahi kuwapa hela ya kujikimu nje na hyo laki tisa bc rudishen hela yao ila kama hela ya kujikimu hawakuwapa jueni kwamba hy mnaenda kupigwa

Kuna muhuni ofisin alichepusha hela za serikali na sasa ashagundua ufuatiliaji wake umeisha sasa anataka imrudie aende kufanya yake
 
Kama walikosea waambieni wazichukue nyie hamkuziona!!

Tena wafokeeni na nyie ili wasiwazoee!!😀

Hizo Halmashauri zinavyozungusha wazabuni malipo yao hadi wanafilisiwa na bank ila zenyewe makosa yao wanataka warejeshewe leoleo.
 
Kabisa mnaruhusu Hadi watu wanakuja kuwafokea?
Watu wote 77 mnafokewa?
Acheni uzembe.
 
Sisi ajira mpya kada ya afya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga hatujapewa pesa ya kujikimu tunateseka sana viongozi wamekaa kimya hakuna anayeongelea hili jambo. Maafisa utumishi wanayo lugha chafu Kuna mmoja anaitwa Sarah
 
Back
Top Bottom