KERO Responded Ajira Mpya (Walimu) Temeke tuliwekewa Laki 9, tukaambiwa ni nauli, sasa hivi wanatuambia turudishe

KERO Responded Ajira Mpya (Walimu) Temeke tuliwekewa Laki 9, tukaambiwa ni nauli, sasa hivi wanatuambia turudishe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kama ni kweli inabidi hiyo pesa ikatwe kidogo kidogo, sio urudishe zote kwa mpigo
 
Maoga makubwa nyie
Pesa ya serikali unairudishaje?
Umepewa utaratibu wa kuirudisha?
Takukuru wanafahamu?
Piga simu uwaombe control namba ya serikali uone kama watakupa
 
Sisi ajira mpya kada ya afya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga hatujapewa pesa ya kujikimu tunateseka sana viongozi wamekaa kimya hakuna anayeongelea hili jambo. Maafisa utumishi wanayo lugha chafu Kuna mmoja anaitwa Sarah
Mfikishie DAS hilo swala.
 
Majizi serikalini sahivi yamepata mpaka ujasiri wa kudai hela zilizolipwa kwa watumishi? Ama kweli awamu ya kula kwa urefu wa kamba
 
Wanasema walikosea kuweka, basi kama walikosea watuwekee utaratibu mzuri wa kurudisha lakini tunafokewa, tunatukanwa ukizingatia sisi ni ajira mpya.
Usirudishe hata 100 mbovu wakitaka waambieni waende Mahakamani shenzi zao pumbavu mnachukuliwajwe kinyonge namna hio halafu mnaogopa nini wakati hela hizo ni sehemu ya kodi zenu? Acheni ufala hakuna kurudisha hata 100 mbovu
 
Urudishee!!! Si bora uache kazi sasa.. unarudishaje sasa
 
Nimepiga hesabu hapo ,ujumla ni Tsh 69.3m. Mkirudisha hizo pesa bila kupewa maelezo yaliyo nyoka ndiyo nitathibitisha Leo kuwa walimu ni wajinga na hamstahili kufundisha wanetu kwani mtakuwa mnawaambukiza ujinga wenu. Na hata wakiwapa maelezo yaliyonyooka ni lazima wawape control namba ya serikali ili mzirudishe serikalini siyo mikononi mwa mtu binafsi.
 
Yaani kumbe ndo mambo ya ajira yalivyo, hapo kama ni Mimi sirudishi na kama wanaweza wanifukuze kazi kama huo ubavu wanao...Wawafuate Benki wawaambie watoe hizo pesa Mimi sihusiki...hapo lazima tutafutana ubaya Tu maana hela ya kuanzia kazi umesema hujapewa, ndo hiyo hiyo, mijitu halmashauri ina roho mbaya Sana ndo maana maisha Yao yanakuwa ya dhiki Sana.
 
Mimi ni mwajiriwa Mpya Manispaa ya TEMEKE, Dar es Salaam, March 6, 2026 tuliwekewa fedha kwenye account zetu waajiriwa wapya Idara ya Msingi, jumla ya Walimu 77 tuliwekewa fedha kwa wastani kila mmoja alipata laki tisa na point.

Hatukujua nini, kuna baadhi ya wenzetu walijaribu kupiga simu wakaambiwa ni nauli, imekaa hivyo sasa tunaitwa tunaambiwa turudishe, tunafokewa, tunaitwa wezi, kana kwamba sisi tulienda kutaka hizo hela.

Wanasema walikosea kuweka, basi kama walikosea watuwekee utaratibu mzuri wa kurudisha lakini tunafokewa, tunatukanwa ukizingatia sisi ni ajira mpya.

Sijui walikosea kweli au waliwekeza kwetu ili baadaye wachukue, tunapewa maelezo hayo kwa mdomo tu na hela tulipewa kimyakimya bila nyaraka yoyote, ni Ajira Mpya Mwaka 2025.

Tunafanya kazi bila uhuru, tusaidieni ujumbe huu ufike kwa Wakubwa wajue tunachopitia.
Walimu malalamiko yetu kama watoto. 😅😅😅😅
 
Walimu nao wanamatatizo gani tu?Umelipwa hela halafu unaanza kupiga simu kwa mkurugenzi kuuliza hii hela ni ya nini?Mwisho wa siku wameona wawanyang'anye.
 
Maoga makubwa nyie
Pesa ya serikali unairudishaje?
Umepewa utaratibu wa kuirudisha?
Takukuru wanafahamu?
Piga simu uwaombe control namba ya serikali uone kama watakupa

Pesa iingie kwenye acc ila utaratibu wa kurudisha, unapewa kwa mdomo 😁.

Wawaandikie barua na control no. mrudishe pesa za serikali nje ya hapo.

Tulieni kama hampo, hawana cha kuwafanya
 
Back
Top Bottom