KERO Responded Ajira Mpya (Walimu) Temeke tuliwekewa Laki 9, tukaambiwa ni nauli, sasa hivi wanatuambia turudishe

KERO Responded Ajira Mpya (Walimu) Temeke tuliwekewa Laki 9, tukaambiwa ni nauli, sasa hivi wanatuambia turudishe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mimi ni mwajiriwa Mpya Manispaa ya TEMEKE, Dar es Salaam, March 6, 2026 tuliwekewa fedha kwenye account zetu waajiriwa wapya Idara ya Msingi, jumla ya Walimu 77 tuliwekewa fedha kwa wastani kila mmoja alipata laki tisa na point.

Hatukujua nini, kuna baadhi ya wenzetu walijaribu kupiga simu wakaambiwa ni nauli, imekaa hivyo sasa tunaitwa tunaambiwa turudishe, tunafokewa, tunaitwa wezi, kana kwamba sisi tulienda kutaka hizo hela.

Wanasema walikosea kuweka, basi kama walikosea watuwekee utaratibu mzuri wa kurudisha lakini tunafokewa, tunatukanwa ukizingatia sisi ni ajira mpya.

Sijui walikosea kweli au waliwekeza kwetu ili baadaye wachukue, tunapewa maelezo hayo kwa mdomo tu na hela tulipewa kimyakimya bila nyaraka yoyote, ni Ajira Mpya Mwaka 2025.

Tunafanya kazi bila uhuru, tusaidieni ujumbe huu ufike kwa Wakubwa wajue tunachopitia.
Cha bure ni kifo tu. Nahata ukifa bado ndugu zako watalipia.
 
Msirudishe! Watakatishaji hao! hawajawapa account binafsi kwamba mrudishe huko? Sasa pesa mshakula mtarudishaje , washenzi hao.
 
Hizo ni hela Zinapigwa.Nyie tulieni.Wakigusa Mshahara wenu mumtafuta Samia.Msiwe na wasiwasi.Hio ni michezo ya Kawaida serikalini.
 
Kuna mshkaji wangu aliajiriwa Babati kwenye orientation kulikua na walimu. Afisa Elimu Kata akasimama akasema walimu wote wasimame akapita kuwakagua kisha kila aliyevaa raba au jeans akamtoa akamuambia akavaen inavyotakiwa mwalimu kuvaa.

Na wale walimu walitoka kwenda kubadili nguo. Tena ni jeans na raba.

HIi kada inanyanyaswa sana ndiyo sababu mtu ataenda kusoma akirudi anapambania recategorization. Sasa mtu anakufokea ili iweje? Pesa mmeweka wenyewe ni kivipi mnaanza kufokea watu badala ya kuwaelewesha?

Mambo ya kimiyeyusho
 
Hiyo ni lazima ulipe pesa za watu, hizo ni pesa ambazo unakopeshwa kuanzia maisha kabla ya kupata salary.

Wengine huwa wanapewa magodoro, Unga ,Mahindi na mchele, mafuta ya kupikia, N.k
 
Sisi ajira mpya kada ya afya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga hatujapewa pesa ya kujikimu tunateseka sana viongozi wamekaa kimya hakuna anayeongelea hili jambo. Maafisa utumishi wanayo lugha chafu Kuna mmoja anaitwa Sarah
Inaonekana huyo Sarah ndio kiboko yenu 😂😂🔥
 
Back
Top Bottom