KERO Responded Ajira Mpya (Walimu) Temeke tuliwekewa Laki 9, tukaambiwa ni nauli, sasa hivi wanatuambia turudishe

KERO Responded Ajira Mpya (Walimu) Temeke tuliwekewa Laki 9, tukaambiwa ni nauli, sasa hivi wanatuambia turudishe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ndio mkuu. Hayo ni mazingira ya upigaji yani hao wakubwa wanatumia hizo account za walimu ku laundry pesa
Mhh! Akaunti za watu wote hao zitatumikaje kufanya upigaji wa wazi kama huo mkuu? Upigaji hauwekwi wazi kiasi hicho. Haya ni makosa tu yamefanyika kama makosa mengine lakini kwa sababu CAG kila mwaka anaibua upigaji ndio maana watu wanadhani huenda wamepigwa. Hakuna upigaji wa namna hiyo mkuu.
 
Mkigoma kuiludisha hiyo hela itaondoka na nyinyi pia na Accounting officer wenu..bora muiludishe mambo yasiwe mengi..
 
Usirudishe hata 100 mbovu wakitaka waambieni waende Mahakamani shenzi zao pumbavu mnachukuliwajwe kinyonge namna hio halafu mnaogopa nini wakati hela hizo ni sehemu ya kodi zenu? Acheni ufala hakuna kurudisha hata 100 mbovu
Wajaze wenzako upepo, liwakute jambo.
 
Hao wanao dai kurudishiwa hizo pesa hawana ubavu wowote wa kwenda kwenye mamlaka yoyote maana wanazidai kwa maslahi yao binafsi.
wanajua wamekosea lungu litawaangukia, ndo maana wanafanya hvo, lakini haiondoi uhalali wa kuchunguzwa kiundani...unaposema maslai yao binafsi unamaanisha hzo pesa wanazokatwa walimu kurejesha zinaingia kwenye akaunti za hao maafisa? Au umaanisha nini..Kama zinaludi kwenye akaunti ya serikali sioni kama kunatatizo.
 
Mimi ni mwajiriwa Mpya Manispaa ya TEMEKE, Dar es Salaam, March 6, 2026 tuliwekewa fedha kwenye account zetu waajiriwa wapya Idara ya Msingi, jumla ya Walimu 77 tuliwekewa fedha kwa wastani kila mmoja alipata laki tisa na point.

Hatukujua nini, kuna baadhi ya wenzetu walijaribu kupiga simu wakaambiwa ni nauli, imekaa hivyo sasa tunaitwa tunaambiwa turudishe, tunafokewa, tunaitwa wezi, kana kwamba sisi tulienda kutaka hizo hela.

Wanasema walikosea kuweka, basi kama walikosea watuwekee utaratibu mzuri wa kurudisha lakini tunafokewa, tunatukanwa ukizingatia sisi ni ajira mpya.

Sijui walikosea kweli au waliwekeza kwetu ili baadaye wachukue, tunapewa maelezo hayo kwa mdomo tu na hela tulipewa kimyakimya bila nyaraka yoyote, ni Ajira Mpya Mwaka 2025.

Tunafanya kazi bila uhuru, tusaidieni ujumbe huu ufike kwa Wakubwa wajue tunachopitia.

Ufafanuzi wa Manispaa ~ Temeke DC yafafanua Watumishi kuingiziwa fedha kisha kuambiwa wazirudishe, yaelezwa ziliingizwa kimakosa
Auditors wakija wanaoneshwa documentation ya malipo kwa walimu. Hiyo ya kuzirejesha ni story nyingine.

Mkizirudisha kienyeji kienyeji, msishangae kama zikiishia kwenye mifuko ya wajanja!
 
wanajua wamekosea lungu litawaangukia, ndo maana wanafanya hvo, lakini haiondoi uhalali wa kuchunguzwa kiundani...unaposema maslai yao binafsi unamaanisha hzo pesa wanazokatwa walimu kurejesha zinaingia kwenye akaunti za hao maafisa? Au umaanisha nini..Kama zinaludi kwenye akaunti ya serikali sioni kama kunatatizo.
Kuna ushahidi gani kuwa zinarudi kwenye akaunti ya serikali?
 
Kuna ushahidi gani tofauti na hisia zako kuwa zinarudishwa kwenye akaunti binafsi za hao watumishi ?
Swali la kipumbavu hili.

Hela zimeingia kwa njia gani na wanatakiwa kurudisha kwa njia gani?

Hemu jifunze kuuliza maswali kwa akili.
 
Swali la kipumbavu hili.

Hela zimeingia kwa njia gani na wanatakiwa kurudisha kwa njia gani?

Hemu jifunze kuuliza maswali kwa akili.
Na wewe ni mmoja ya hao walimu waliopokea hizo pesa kinyemera. Waambiwe wenzako msiporudisha kwa hiyari mtarudisha kwa nguvu.
 
Hawakukosea, ndio zinapigwa hivyo. Na wanajua walimu ndio wanawamudu kiwapelekesha wanavyojisikia, maana wengi ni waoga.
Kama mshahara wako haitoshi kulipia Safari ya Ndege Kwenda Zanzibar, mzee pambana sana upate kujikwamua
 
Back
Top Bottom