Mimi ni mwajiriwa Mpya Manispaa ya TEMEKE, Dar es Salaam, March 6, 2026 tuliwekewa fedha kwenye account zetu waajiriwa wapya Idara ya Msingi, jumla ya Walimu 77 tuliwekewa fedha kwa wastani kila mmoja alipata laki tisa na point.
Hatukujua nini, kuna baadhi ya wenzetu walijaribu kupiga simu wakaambiwa ni nauli, imekaa hivyo sasa tunaitwa tunaambiwa turudishe, tunafokewa, tunaitwa wezi, kana kwamba sisi tulienda kutaka hizo hela.
Wanasema walikosea kuweka, basi kama walikosea watuwekee utaratibu mzuri wa kurudisha lakini tunafokewa, tunatukanwa ukizingatia sisi ni ajira mpya.
Sijui walikosea kweli au waliwekeza kwetu ili baadaye wachukue, tunapewa maelezo hayo kwa mdomo tu na hela tulipewa kimyakimya bila nyaraka yoyote, ni Ajira Mpya Mwaka 2025.
Tunafanya kazi bila uhuru, tusaidieni ujumbe huu ufike kwa Wakubwa wajue tunachopitia.
Ufafanuzi wa Manispaa ~ Temeke DC yafafanua Watumishi kuingiziwa fedha kisha kuambiwa wazirudishe, yaelezwa ziliingizwa kimakosa