View attachment 2300525Huu ni UPUMBAVU na haupaswi kukaliwa kimya na mtu yeyote mwenye akili timamu. Sensa ni zoezi linalowahusu watanzania wote si wana CCM peke yao. Sensa ni kwa maendeleo ya taifa na sio maendeleo ya CCM. Wote tutahesabiwa. Na fursa za ajira zinapaswa zitolewe kwa USAWA kwa watanzania wenye sifa na uwezo, bila kuwabagua kwa jinsia zao, dini zao, makabila yao au vyama vyao vya siasa.
Ni aibu huko Mbeya nafasi za kazi za sensa zinatolewa kwa misingi ya kisiasa. Yani kama wewe sio mwanaCCM hupati. Eti Katibu wa UVCCM anamtumia WEO majina ya wanaCCM walioomba nafasi za kazi ya sensa. Ujinga gani huu? Kwahiyo wasio wanaCCM wakiomba wanajisumbua sio?
Kila siku mnatusisitiza tukubali kuhesabiwa, halafu leo mnapeana nafasi kwa ubaguzi wa kisiasa? Mnataka tususie sensa? Tuwaachie hiyo sensa wanaCCM mjihesabu wenyewe? Mazwazwa kabisa.
Kwani mtu akiomba nafasi bila kupewa endorsement na chama chake cha siasa kuna shida gani? Kama ana sifa si atapata tu. Kitendo cha kupigiwa debe na chama cha siasa ni kielelezo kuwa watu hao wamepungukiwa sifa. Wangekua na sifa za kutosha wasingehaha kuomba endorsement ya chama chakavu cha CCM.
Awamu ya tano ilijaa ubaguzi. Watu walibaguliwa kwa vyama vyao vya siasa, wengine wakabaguliwa hadi kwa makabila yao. Bahati nzuri Mungu akaingilia kati na kuamua ugomvi (kwa sauti ya Nape).
Awamu ya sita angalau vitendo vya KIBAGUZI vikapungua sana. Watu wakaanza kuishi kwa amani na kuifurahia nchi yao. Sasa mmeanza tena kutuletea ubaguzi wenu wa kiwaki? Endeleeni, matokeo mtayaona.!
Cc. Malisa GJ