Ajiua kwa kujinyonga siku chache kabla ya harusi yake

Ajiua kwa kujinyonga siku chache kabla ya harusi yake

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
2,968
Reaction score
8,139
Joseph Patrick Ngonyani mkazi wa Kijiji cha Makuyni kilichopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro amejiua kwa kujinyonga ikiwa zimebaki siku 29 afunge ndoa.

Uchunguzi wa chanzo cha kifo chake bado unaendelea.

Godlisten Malisa ameandika haya katika ukurasa wake wa Facebook kuhusu kifo cha Joseph Ngonyani (rafiki yake):
Mwezi August mwaka huu ulimvalisha pete mchumba wako na ukatuomba support marafiki zako kwa ajili ya ndoa yenu uliyopanga kuifunga mwezi December mwaka huu. Tulikutakia heri na kuahidi ushirikiano. Lakini leo nimeshtushwa na taarifa ya kifo chako cha ghafla. Nimeambiwa umejinyonga. What a shocking news.!

Rafiki na mdogo wangu #JosephNgonyani nini kimekusukuma kufanya uamuzi huu mgumu namna hii? Zilibaki siku chache tu kuelekea ndoa yako. Itakuaje sasa kwa mchumba wako? Je mipango yote mliyopanga ndio imeishia hapa? Kwanini hukutishirikisha ikiwa kuna jambo gumu uliloshindwa kulimudu? Daah. Just rest in peace bro. Nimeishiwa maneno.!

Wanaume tunapitia mengi sana. Baada ya kuweka taarifa ya dogo #JosephNgonyani kujinyonga, ndugu Mathew Mfinanga ameamua kushare sehemu ya mapito yake. Ni magumu sana, lakini jambo la muhimu tusiache kuongea. Kama unapitia changamoto ukaongea na watu 100 wasipokuelewa, basi kuna mmoja atakuelewa. Na Mungu atamtumia huyo mmoja kubadili story ya maisha yako.

Wanaume wengi hufikia hatua ya kujiua kwa kutokuongea, au kuona wakiongea watakua wamejidhalilisha. Please talk to save ur life. Taarifa ya taasisi ya afya ya akili nchini Marekani (National Institute of Mental Health) inaonesha kuwa 77% ya watu wote wanaojiua ni wanaume. Hizi takwimu zinatisha. Moja ya sababu ya wanaume "kukimbilia" kujiua ni kushindwa kuongea wanapopitia magumu.

Wanawake hawajiui kirahisi kwa sababu wanaongea sana. Katika kuongea kwao wanaweza kupuuzwa au kusaidika, lakini la muhimu wameongea. Kuongea kunapunguza mzigo, kunakupa nafasi ya kufikiria tena, kunakuwezesha kupata mawazo mapya, kunasaidia kujipanga upya. Kujiua ni ubinafsi. Ni kuacha mzigo mkubwa kwa wale waliokua wanakutegemea. Ni kuacha alama ya maumivu yasiyokoma kwa wanao, mke na ndugu zako. Kujiua sio suluhisho. Wanaume tuongee, tuongee, tuongee.!

Mchangiaji mmoja pia ametoa ushuhuda wake kuhusu alivyopitia hali ya sonona (See atached image) :
IMG-20221128-WA0045.jpg
 
Apumzike kwa Amani..kila nafsi itaonja mauti.
 
Sasa Wabongo kabla hujaongea wanakulisha Maneno, Sasa ukiongea si ndio wanakusambaza kabisa.

Kwa Mimi hapana kwakweli nitakabiliana na hali zote na hakuna kujinyonga.
Hahahahahaha...!! Hilo nalo neno aisee.
Ila ni vizuri kuwa na mtu wako angalau mmoja ambae unajua piga ua huyo lako ni lake na lake ni lako, hivyo hawezi kutoa nje ndio wa kuongea nae huyo.
Ila una point ya msingi sana pia!!
 
Mwingine huyu.

#HABARI Askari wa Kampuni ya ulinzi ya Suma JKT, Osea Kashililika (21), amejiua kwa kujipiga risasi shingoni kwa kutumia silaha aina ya shot gun pump action yenye namba 00715V mali ya Suma JKT akiwa lindo la Benki ya Azania iliyopo jijini Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Polisi ambaye ni Mkuu wa Oparesheni Mkoa wa Mbeya, Abdi Issango amesema tukio hilo limetoa majira ya saa tano asubuhi eneo la eneo la Benki ya Azania na sababu za kutoa uhai wake Kashililika bado hazijafahamika.

Kamanda Issango amesema tayari mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na kwamba vielelezo kama vile bunduki na risasi vimehifadhiwa kituo cha Polisi kwa ajili ya uchunguzi. #EastAfricaTV
 
Tena sio jambo dogo. Lazima kutakua na jambo kubwa lililomsukuma bwana Ngonyani katika dimbwia maamuzi haya
Yupo jamaa mmoja alikuwa rafiki yangu nilisoma nae chuo na nishawai kukaa group moja japo mi nilikuwa chairman ila alikuwa mtu yuko active sana nilimkubali ila ishu zake anaficha mpaka ilipobuma .

Ilikuwa ivi jamaa alikuwa na demu wake wanapendana sana na hapo chuo kusema la ukweli kasoma mpaka third year hakuwai hata kutongoza kwa maelezo yake alimpenda demu sana ila mshkaji kwao life la kawaida sana ,kama tegemezi basi kipind tukiwa chuo alikuwa na hustling Sana kila dili yye hata dalali yupo anamake money anatuma kwa bi mother wake na kumuhudumia demu..basi miaka kadhaa mbele baada ya chuo zilitokea ajira akasema hatoenda alikuwa kashaanza biashara na alipiga mwaka mmoja awe kashamuoa demu wake anajulikana mpaka home kwa huyo demu yaani kama kwao maana wote Wana asili moja ni watu wa mbeya ...

Basi jamaa ule mwaka aliyumba kiasi cha kuingia madeni kibao mpaka biashara ikafa ndani ya mwaka mmoja kingine akasema hapo hapo demu alianza kuleta nyodo ,bahati mbaya demu kashaanzisha mahusiano na jamaa mwingine..

Basi washkaji wake wakamsanua kwamba demu kashachumbiwa yeye akajipa moyo labda masnitch ..kumbe kweli mpaka demu kaolewa na jamaa hapa dar harusi kubwa kabisa .,jamaa kaenda home kwa kina demu wakawambia eti kwa nn alikuwa anamchezea na sio kumuoa jamaa akawaeleza zile ishu bado wakamtolea nje maana demu kashaolewa na kweny simu kablockiwa na demu.

No way jamaa alifanya attempt ya kunywa sumu watu wakamuwahi haswa washkaji na ishu wakasema iwe kimya hata mwenyekitu asijue basi jamaa tangu hapo Kawa kama kapumbaa yaani kama kachizisha kimtindo ,kapooza ila demu kashaolewa Kuna kipind vilitulia akawa anapiga dili coz chuo alikuwa na performance nzuri tu sasa akiwa mishe posta ile kashapoteza kama mwaka na kitu tangu ya tukio ,bahati mbaya akakutana na demu yule akiwa na jamaa na demu akiwa na mimba jamaa ilikuwa siku mbaya kwake Tena ile hali ikaanza kumrudia Tena..

Akaona arudi kwao mbeya ila yupo town sasa yuko fresh anapiga ishu zake tu za maana namkubali ni hustler .
 
Duuuuh poleeee yake aseeeeeh. Nimeogopaaaaa!!!!
 
Back
Top Bottom