Akili gani hii mtu ananunua costa milion 100 kwa ajili ya kupewa laki 1 kwa siku

Akili gani hii mtu ananunua costa milion 100 kwa ajili ya kupewa laki 1 kwa siku

Hii ni biashara nyingine kichaa yaani unawekeza milion 100 Kwa ajili ya laki 1 Kwa siku na hiyo pesa unalipata kkwa mbinde na siku nyingine utaletewa mpaka elfu 50 aisee huyu mtu anaakili timamu kweli yaani mwaka unaisha hata nusu ya Bei alionunulia kicosta chake haijarudi yaani hapo bado hata ajali haijapata ambapo inaweza kupata mzinga ukaambulia skrepa aisee mtu mweusi anasafari ndefu Sana ya utajiri duniani
Hizi ni hesabu za karatasi, ingia ground
 
Mfano: Papaa fololo
Idadi ya Costa: 50
Makadirio ya manunuzi Mil 100@ Costa.
Hesabu ya Boss: Tsh 100,000 kwa siku.
Tutumie siku 360 ( 1 year).

Jumla ya Manunuzi ya Costa Tsh 100,000,000 * 50 = 5,000,000,000/= ( Billion 5)

Hesabu ya Boss

1 Costa Tsh 100,000 * 360 = 36,000,000

36,000,000 * 50( idadi ya Costa)
= Tsh 1,800,000,000 ( 1.8 B) per year kwa 50 Costa

Kila kitu kina plan, let use 5 year plan

1,800,000,000 * 5 = 9,000,000,000 ( Billion 9)

Billion 9 Toa Manunuzi ya Billion 5

Faida ni 4,000,000,000/=
Gawanya kwa miaaka 5, inamaana kila mwaka anaingiza faida ya Mill 800 ambapo kwa siku anaingiza Faida ya million 2. 22

Hapo sijaweka matengenezo makubwa na madogo. Nime assume hakukuwa na matengenezo makubwa kwa miaka 5.

Hesabu ngumu sana, hapo nahisi nimeboronga. Mnisamehe tu.
 
We umefanya hiyo biashara tuanzie hapo naona unarahisisha tu
Siongelea maneno ya vichochoroni naongelea fact na evidence kwenye transportation and logistics..

Binafsi nimeanza na biashara hii nimeanza na Bajaj na nachokuambia nimekifanya.

Nilinunua bajaj nikakata bima kubwa nikapata ajali nikalipwa 4m nikarepair asaivi nakula pesa

Nakutumia Picha
 
Attachments

  • Screenshot_20241028-092645.png
    Screenshot_20241028-092645.png
    1.2 MB · Views: 5
Mfano: Papaa fololo
Idadi ya Costa: 50
Makadirio ya manunuzi Mil 100@ Costa.
Hesabu ya Boss: Tsh 100,000 kwa siku.
Tutumie siku 360 ( 1 year).

Jumla ya Manunuzi ya Costa Tsh 100,000,000 * 50 = 5,000,000,000/= ( Billion 5)

Hesabu ya Boss

1 Costa Tsh 100,000 * 360 = 36,000,000

36,000,000 * 50( idadi ya Costa)
= Tsh 1,800,000,000 ( 1.8 B) per year kwa 50 Costa

Kila kitu kina plan, let use 5 year plan

1,800,000,000 * 5 = 9,000,000,000 ( Billion 9)

Billion 9 Toa Manunuzi ya Billion 5

Faida ni 4,000,000,000/=
Gawanya kwa miaaka 5, inamaana kila mwaka anaingiza faida ya Mill 800 ambapo kwa siku anaingiza Faida ya million 2. 22

Hapo sijaweka matengenezo makubwa na madogo. Nime assume hakukuwa na matengenezo makubwa kwa miaka 5.

Hesabu ngumu sana, hapo nahisi nimeboronga. Mnisamehe tu.
Hahahaha 🤣🤣🤣
 
Huyo dogo ni jobless ambaye kasoma elimu ya dumu fagio.

Anajiita Chief God love Ana I'd kibao zote ni miaka ya 2024 na 2023

Nimeona hapo haelewi kuhusu bima
So kichwa kimejaa matusi
Hasira za nini mkuu Mimi sijakusababishia umasikini ulionao 🤣🤣🤣🤣
 
ni uwekezaji mgumu. Itachukua miaka miwili kurudisha pesa. Mwaka wa 3 ndo faida itaanza.
hakuna uwekezaji mwepesi. Dangote bilionea na anawashauri wa biashara lakini kwenye cement akakutana na za uso.

hii ni biashara ambayo ina high risk, but ukiweza kumanage inafaida nzuri. gari nyingi zinarudisha mtaju mwaka na nusu. then baada ya hapo uza. utakachouza ndo faida yako.

kuweka utt 70M na kuweka gari road. after 1year na nusu kwenye gari ukiuza umekosa sana 40 inategemea na utunzwaji wa gari. nambie utt kama inafika hyo.
 
Wacha nitoe niliyokutana nayo kiuhalisia kabisa ana kwa ana mbivu na mbichi kutoka jikoni.

1. Taasisi niliyokuwa natumika, kulikuwa na mbaba anabiashara ya malori ya kubeba mizigo kwenda mikoani. Muda wa kuanzia saa nne asubuhi, muda wa lanchi mchana na kuanzia saa kumi muda wa kurudi nyumbani... huyo baba alikuwa anaongea na simu za madereva na mafundi yaani alikuwa mkali kwenye simu hadi unahisi nikipita karibu yake atanisweka kibao au mbata. Utamsikia, nakwambia wewe na huyo utingo wako ntawaweka ndani na kabla sijawaweka ndani nawakata mapanga kwanza halafu linafuata tusi.

Wafanyakazi wenzie tulimzoea hasa kinamama, tukawa tunaambizana, biashara hizi za kufanya upande presa waachie wanaume wenyewe misiwezi, mali yako halafu kupata hela/malipo hadi ugombe/uwe mkali.

2. Huyu dada aka mshangazi, alizaliwa pekeyake na alilelewa na mama yake tuu hakuwahi kumjua baba yake wala ndugu upande wa baba. Mama yake alipofariki alimuachia nyumba hapo Sinza, akaja kuipiga bei ili apate mtaji afanye biashara......!!!🙄🙄🙄
Alianza kuuza mkaa anaagiza mkoani aulete Dar auze kwa jumla, akatapeliwa kaletewa magunia 10 yote chenga na unga wa mkaa... sehemu ya mtaji ukalala hapo. Akashauriwa anunue daladala DCM ya ruti ya Mbagala Kawe hiyo hela ya mauzo ya wiki anatoboa maisha. Kaingia wanguwangu sijui aliuziwa milioni ngapi ile daladala ila ilikuwa used na inafanya ruti hiyohiyo Mbagala Kawe, aliletewa hesabu ya wiki moja tuu ambayo nayo alilipia matengenezo ambayo hayakuisha baada ya hapo gari ikawa juu ya mawe haitengenezeki.
Pesa iliyobakia akajenga huko ukanda wa Tegeta nyumba haikuisha iko kwenye lenta haina milango wala madirisha akahamia...
Maisha yanatisha acha tuu.

3. Miaka 4 kabla sijastaafu nilimfata baba mmoja hapo kazini nikamwambia nataka nianzishe biashara ya uber ninunue ist moja used nitafute dereva niwe naingiza hela ya thupu. Akaniambia dada yangu Kasinde, biashara ya magari ni kichaa, sikushauri dada yangu hiyo biashara inataka ujitoe ufahamu kwelikweli. Kwanini usifungue duka la vyakula au madawa. Nikaachana na habari ya kununua it for uber, saa hii uongo maisha alhamulilah 🙏, can't complain.
 
Back
Top Bottom