Akili gani hii mtu ananunua costa milion 100 kwa ajili ya kupewa laki 1 kwa siku

Costa Japan ni milioni 40 hadi 50, ikiwa nzuri zaidi ni 60M. Hiyo ya 100 jko wapi?
 

Mkuu kwani ukiwa na akili wewe tu si inatosha?
 
Hatuangalii Biashara inatoa shingapi tunaangalia tunabiashara ngapi ambazo zinatoa faida kidogo kidogo Ila tukijumlisha tunapata Hela nyingi na biashara hizo zinajiendesha na kuna kuwa na uhakika wa mtaji wetu kuwa safe
Deep.
 
Ni upuuzi
 
PIa wenye kufanya hizi biashara hawawezi kuwa na gari moja kuwa moyo wake wote ameweka kwenye hiyo gari.
 
Mbona mabasi yanagharamiwa mil 400 mengine lakini hayaleti mil zaidi ya mil 10 kwa mwezi?

Mbona nyumba zinajenga kwa mil 350 lakini hazileti mil zaidi ya mil 24 kwa mwaka?

Waache watupe huduma ,kwa fikra hizo akuna ambaye angewekeza huko na tusingepata usafiri nafuu.

Biashara ambayo inakupa Gawio la 20% kwa mwaka sio mbaya,mbaya ni inayokupa chini ya asilimia 11% na haidumu kwa miaka zaidi ya 10
 
Kuna mshua ana malori anaweza kuwa kijiweni na wenzie mara dereva wake anatokea kwa mbali kwa miguu mzee anaanza kutukana 'we ms@@@@nge mwanaharamu k@@@@@@yo ishia huko huko usiniletee balaa! Ha ha ha ha. Lakini kuna watu wanaimudu hii biashara acha tu. Kuna majirani zangu Wapemba huwa nawaoana nje ya nyumba yao yenye uwanja mkuuuuuubwa wanacheza draft huwa najiuliza na kihererehere changu hawa vipi hawachoki kukaa. siku moja jumapili napita hapo kwao geti liko wazi niliona Nissan Civilian 8, yes nane zinafanyiwa service, daladala na zote ziko kwenye hali nzuri. Sasa wacha sisi tuendelee kusema hii biashra haifai. Hata mimi hii biashara sitaki hata kuiskia.
 
Je
Na wale wanaonunua nyumba 250m alafu anapangisha kwa 250k kwa mwezi au 300k?
 
Hii naifananisha na hadithi moja ya msomi na mkulima.

Msomi alitumia usomi wake kupima hali ya hewa na akapata jibu la mvua inaweza kunyesha au hapana.

Akaanza kufikiria kwamba, akilima mvua inaweza isinyeshe. Akaacha kulima.

Lakini yule mkulima hakujali mvua itanyesha au hapana, yeye alilima tu.

Baadaye mvua ikanyesha, zao la mkulima likastawi na akavuna mazao mengi na baadaye kumuuzia msomi. 🤗
 
Binadamu tuna akiri ya ajabu sana, na hiyo hela una kuta haijatokana na Costa. Sasa badala kuimarisha biashara iliyo mpa hiyo 100m, mtu anaenda kununua au kuingia kwenye biashara nyingine
 
watu wanapiga pesa wanatajirika inategemea na approach zako ulizoingia nazo.
1. gari gani
2. route gani
3. dereva gani
4. fundi
Mkuu achana naye uyo kiazi. Kwanza sidhani kama ana hata leseni ya udereva. Fala mmoja anakuja na hoja za kindezi kila cku, kazi kukandia biashara za usafirishaji. Hatoi maoni mengine kama, iyo 100m mtu aifanyie nn tofauti na kuwekeza kwny iyo costa. Kazi kunanga tu biashara za watu.
 
Mkuu costa gani million 100 mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…