Seran
JF-Expert Member
- Feb 7, 2025
- 36,315
- 104,500
Nyooh!😆Believe it or don't! It's done!
Nyooh!😆Believe it or don't! It's done!
Naapa hakyanane tena!Nyooh!😆
Tapeli😁Naapa hakyanane tena!
Si kweli.Unanionea.Tapeli😁
Kuna nyakati uzinzi ulifanyika kwa siri na tahadhari mno hata kama mwanamke aliolewa tayari akiwa na mtoto. Nafasi ya mume ilikuwa ya heshima na upekee. Sasa hivi ni kuburuzana kama fuso bovu.WAZAZI HAWAACHANI KAMWE BALI HUTENGANA TU,KWENYE SHIDA KUBWA HUWASILIANA NA KUJULIANA MALI,HAPA NDIPO UGUMU ULIPO!...
Anakasirika nini na ni maongezi ya kifamilia? Japo hadithi imekaa kama uongo.
Faragha gani inahitajika hospitalini. Hapo watu si wanakuja kutoa pole tu. Huyo jamaasio sehemu ya familia ndio maana akaambiwa aende nje. Meanaume unatakiwa kuanzisha familia yako, sio kudandia kwenye familia ambayo tayari ishaanxishwa na mwanaume mwingine
Ofcourse kwenye kundi hilo huvai kofia ya familia, ndo maana unawapisha.
Tatizo halisi ni hofu ya kugongewa. We uliza tu, hapo kinachoogopwa ni nini? Wanaume huru ni wale wasio na hofu juu ya mwanamke ila wanawake zao ndo wenye hofu juu yao.
Hii ni point ya muhimu.Kwamba anamtu mwingine anaye share naye maisha yake.
Hii ni point ya muhimu.
Ndo maana wengine wanataka mhusika awe amekufa.
Binafsi naamini single mother anaweza kuwa Loyal kwa nafsi yake hata kabla ya kuwa na mume kwa kuweka mipaka na mzazi mwenzake, mipaka migumu kuvunjika.
Binti yangu yoyote akizalishwa akakimbiwa ushauri ntakaompa ni kuiheshimu nafsi yake kwa kutokuwa mrahisi kwa mzazi asiyemhitaji kama mke, akifanikiwa hilo hata jamii yake itamheshimu.
Mkuu, upo sahihi kabisa, changamoto ni kwamba tunajipumulisha kwa single mother sababu walibeba mimba. Hawakunywa P2, Hawakutoa mimba, waliamua wazae.Mkuu
Unajua hizi ndoa zina mambo mengi sana.
Kwenye ndoa kuna vipindi vigumu kwa kiuchumi na kiafya.
Kuna vipindi vigumu ambavyo wanandoa wanakuwa kama hawajaliani tena kihisia kama zamani.
Wanaume hawawajali wake zao kihisia. Hawawapi Wake zao attentiion. Wanawake wanajikuta wanajikuta wanarudisha mawasiliano ya siri na Ex zao hasa waliowazalisha kwa sababu wanakiunganisha(mtoto).
Nikuhakikishie kuwa mwanamke kama hapewi attention na hajaliwi kihisia huyo lazima awasiliane na Mzazi mwenzake kufidia hilo gap.
Hilo gap halizibwi kwa kula wala kwa pesa.
Atampigia kwa kigezo cha mtoto lakini hilo hata linaweza lisiwe lengo kuum yule mzazi mwenzake akiwa anampa maneno mazuri, anampa moyo, anamjali hata asipomtumia hata 10 atamsifu tofauti na mumewe aliyemuoa ambaye hampi attention