Akimbia Hospitali baada ya mkewe ‘singo maza’ kutembelewa na mzazi mwenzie

Akimbia Hospitali baada ya mkewe ‘singo maza’ kutembelewa na mzazi mwenzie

Kaka mmoja hapa mtaani alioa mwanamke mwenye Watoto Wawili wa Baba Mmoja, huyo mwanamke Aliachana Na MUME Wake kipindi Watoto Wakiwa Wakubwa tayari wameanza shule, baada ya kuachana na mume wake Akaolewa Na huyu kaka wa hapa mtaani, kaka ana pesa Kiasi.

Jana Mke Kaumwa Sana ikapekea akalazwa Hospital , akiwa hospital Akampa Taarifa Mzazi Mwenzake (yule waliyeachana) Kisha Mzazi mwenzake Akaenda Na Watoto Hospital Kumjulia Hali pale hospital.

Mume Wake Alijiskia Vibaya Sana kuona Yule Mwanaume anamtembelea mke wake, Mke Akamwambia Mume Wake Naomba Utupishe Kidogo Nina Maongezi Na Mzazi Mwenzangu, kaka Alitoka Nje na Hakurudi Tena Pale Hospital, Hadi Leo na inasemekana kaka Kaenda Dar es Salaam na Hana mpango WA kurudi Tena mana hapa mtaani haonekani tena.

My Take
Chambueni
Fictional story japo umeiweka kama somo ambapo mtu yoyote yanaweza kumkuta.
 
Kuoa mwanamke ambaye sio bikra n uvumilivu tosha, ukiongeza na n single mother ndo balaa kabisa, huo uvumilivu n God made.
Mkuu, Binafsi nimeshuhudia baadhi ya mahusiano mpaka ndoa, and trust me, mwanaume mwenye amani ni anayebahatisha mwanamke mwenye msimamo bila kujali msimamo wake umesababishwa na nini.
Wengine woooote hakuna mwenye afadhali.
 
Kuna ubaya gani mume akiwepo? Yeye akiona kuwa mazungumzo yanayoendelea hayamhusu ajisikie kuondoka sio kuambiwa 'Tunaomba utupishe'
Kitendo cha kuombwa atoke it means ni mtu ambaye mkewe yupo in control. Mke hana hofu ya kumpoteza. Na tatizo lipo hapo, si kwenye usingle mother wa huyo mkewe.

Kwani nikuulize mkuu, umezaa na mwanamke, mimi nikamuoa, ameugua, ukaja hospitali na mtoto wenu kuja kumsabahi, kwanini napaswa kukuhofia?

kwa sababu umekuja hospitali sasa unaweza mshawishi akurudie?

au kwa sababu mke wangu akikutana na wewe lazima akutanulie miguu?
 
Kama ni scenario ya kweli hakupaswa hata kuombwa, ilitakiwa awapishe kabla ya kuombwa, awape faragha ya mazungumzo sababu na watoto walikuwepo.
Livae hilo koti la hiyo stori uwe ni wewe hapo, ungelimpisha mkeo aongee na dear x wake?

Au kwa sababu issue ni ya mwingine ndiyo unairahisisha na kuifanya ndogo sana kama pilton?
 
Livae hilo koti la hiyo stori uwe ni wewe hapo, ungelimpisha mkeo aongee na dear x wake?

Au kwa sababu issue ni ya mwingine ndiyo unsirahisisha na kuifanya ndogo sana kama pilton?
Kama nina wasiwasi na X wake basi sikutakiwa kusubiri mpaka aumwe ndo nifanye maamuzi.

Fact tu kwamba natakiwa kumlinda ili asirudi kwa X wake hilo ni tatizo kubwa zaidi ya kumpa nafasi akiwa hospitali na watoto wao.
 
Kama nina wasiwasi na X wake basi sikutakiwa kusubiri mpaka aumwe ndo nifanye maamuzi.

Fact tu kwamba natakiwa kumlinda ili asirudi kwa X wake hilo ni tatizo kubwa zaidi ya kumpa nafasi akiwa hospitali na watoto wao.
Scenario imeletwa kipande kidogo sana cha maisha ya hiyo ndoa!
Naona issue ni ya kushitukiza, kaumwa kamuita X wake.
Tuchukulie hivyo, unamlindaje hapo bila kujaa jazba kwanza na kufura kama kifutu?
 
Back
Top Bottom