Al-Barzakh: Haya ndio Maisha ya Kaburini baada ya kufa

Nani kwakwambia kuwa lengo la kufanya mapenzi ni kuzaliana tu? Hivi kuna starehe gani katika kiwiliwili cha mwanadamu kushinda kufanya mapenzi?

Ni hivi Paradise (peponi) ni ulimwengu wa raha na starehe.Na starehe kubwa kwa maisha ya mwanadamu ni kula(unachokitaka) ,kunywa (unachokitaka) na kufanya mapenzi!! Hivyo vingine ni vya ziada tu.

Ulimwengu huu tunaoishi ndio ulimwengu wa shida ila baada ya kufa kuna sehemu mbili Shida za milele na raha za milele. Na hayo yote ni matokeo ya machaguzi utakayoyachagua hapa duniani.
 
Wewe endelea kuwaza mambo ya mwilini wakati utaoza na Mungu ni Roho na wamwabudua wapaswa kumwabudu katika roho na kweli! Endelea kusubiria mabikra 72 wenye macho ya mviringo!
 
Wewe endelea kuwaza mambo ya mwilini wakati utaoza na Mungu ni Roho na wamwabudua wapaswa kumwabudu katika roho na kweli! Endelea kusubiria mabikra 72 wenye macho ya mviringo!
Quran 75:

(1) Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!
Ninaapa na natilia mkazo kiapo hichi kwa Siku ya Kiyama, na hiyo ni kweli iliyo thibiti;

(2) Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu!
Na ninaapa na natilia mkazo kiapo hichi kwa nafsi inayo mlaumu mtu kwa dhambi zake na upungufu wake, ya kwamba bila ya shaka yoyote mtafufuliwa baada ya kukusanywa mafupa yenu yaliyo tawanyika.

(3) Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
Hivyo mtu anadhani baada ya kuwa Sisi tulimuumba naye hakuwa kitu chochote, tutakuja shindwa kuyakusanya mafupa yake yaliyooza na yakatapanyika?

(4) Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!
Hasha! Sisi tuna uweza wa kuviweka sawa hata vifupa vya vidole vyake vilivyo vurugika, wachilia mbali mafupa yake makubwa makubwa ya mwili wake.

(5) Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake.
Hivyo mtu anakanya kufufuliwa? Anataka abakie katika uasi wake katika siku zote zilizo mbakilia katika umri wake ulio salia?

(6) Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?
Anauliza kwa kuona haiwezi kutokea saa ya Kiyama: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?

(7) Basi jicho litapo dawaa!
Jicho litapo tahayari kwa kufazaika na kushtuka,

(8) Na mwezi utapo patwa!
Na mwangaza wa mwezi ukapotea,

(9) Na likakusanywa jua na mwezi!
Na jua likakusanyika na mwezi kuchomoza magharibi,

(10) Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?
Mtu hapo atasema: Yako wapi makimbilio kuikimbia hii adhabu?

(11) La! Hapana pa kukimbilia!
Huachi, ewe mtu, kutafuta makimbilio? Leo huna pa kukimbilia wewe,

(12) Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.
ila kwa Mola wako Mlezi peke yake, ndipo penye matulivu ya waja, Peponi au Motoni.

(13) Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha.
Siku hiyo mtu ataambiwa vitendo vyake alivyo vitanguliza na alivyo viakhirisha.

(14) Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.
Bali mtu yeye mwenyewe ni hoja iliyo wazi juu ya nafsi yake inayo mkazania kwa anayo yatenda na anayo yaacha.

(15) Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.
Na ijapo kuwa atajitolea chungu nzima ya udhuru na akazieneza, hawezi kabisa kuepukana na hoja hizo
 
Ikiwa mwili utaoza ni kipi Kinachomfanya Firauni aliyejiita MUNGU asioze hadi leo karne na karne?
Mkuu farao walikuwa wanakausha watu.Na wamekausha wengi tu sio firaun tu. Zamani niliamini firaun alifia majini kumbe mafarao walikuwa na utanaduni wa kukausha ndio wazike ndio maana kuna farao wengi tu hawajaoza.
Ukifuatilia egyptology uragundua mengi.
 
ALLAH anamshangaa sana mtu anaekanusha kuwa akishakufa na kuvurugika mifupa yake kuwa hataweza kurudi katika umbile lake la sasa!!

Anawajibu kwa kuwaambia kuwa anaweza kurudisha hadi ncha za vidole vyako baada ya mwili wako ushakuwa mavumbi.

Mtume (s.a.w) anasema Siku ya Qiyama wanaume tutafufuliwa tukiwa uncircumcised (tuna magovi) yaani hadi kipande chako cha nyama ya uume kilichokatwa na kutupwa ,ALLAH atakirudisha.
 
Acha usanii wako wewe, kaburini hakuna maisha, mwili unaoza fahamu zinaondoka unakuwa sawa na mtu aliyelala usingizi "fo fo fo"
Hahaha…

kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.
Mhu 9:5‭-‬6 SUV
 
Allah hana mshirika hii ''SISI'' tena vipi!
 
Bible imenyooka haiana kona kona
 
Livor morts blood settle to certain part due to gravity
 
Enyi waamini, inueni vichwa vyenu muijue kweli


Baraja 2:8
 
Hebu kwanza tuambie roho ni kitu gani?5
 
1. Naomba utuambie nafsi ni kitu gani?
2. Wewe ni Quaranist?
 
1) Kwa ufupi, Nafs ni wewe binafsi bila kiwiliwili.

2) Sielewi ni nini "quaranist". Mimi ni FaizaFoxy wa JF.
1. Nawezaje kuwa mini bila kiwiliwili? Naomba ufafanuzi zaidi....

2. Quranist ni wale wasioamini kabisa hadithi za mtume
 
1. Nawezaje kuwa mini bila kiwiliwili? Naomba ufafanuzi zaidi....

2. Quranist ni wale wasioamini kabisa hadithi za mtume
Wewe ni Nafs yenye kiwiliwili, Nafs huitwa roho (spirit) pia.

Nafs inabeba himaya yako ya mwili na ya kiroho. Unachoona, unachosikia, unachofanya, unachonusa, unachoonja. Vyote hivyo vinabaki kwenye himaya (arsh) ya Nafs yako. Na nafs zinazokuwa kwenye kiwiliwili chako ni tatu tofauti (soma kuhusu Qareen), moja ni yako mahsusi na moja ni ile ya kishetani na moja ni ile ya mema. Hizi mbili daima zinaishawishi nafs yako, moja kutenda mema, moja kutenda ya kishetani. Wale wenye self control ndio huishinda nafs ya kishetani, inaposalim amri na kuwa njema basi hapo umevuka darja la majaribio ya Shetani na unakuwa mtu mwema sana.

Ukiisoma Qur'an kwa kina inaelezea hayo, pia kuna Hadith ya Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi Wasalaam imeeelea Qareen, alielezea kuhusu Qareen wake kuwa amesilim.

Kuna bwege mmoja aliulizia hapo juu, aliisoma aya, akona kuna "wawili wametajwa" akauliza "hao wawili ni nani", haielewi Qur'am na haelewi kuhusu Qareen, nikaona ni poyoyo hata nikimuelezea hatoelewa kwa kuwa Hamuamini Allah, Haiamini Qur'an na hamuamini wala kumjuwa Mtume Muhammad salaa Allahu alayhi Wasalaam ni nani. Anafikiri alikuja kwa ajili ya Waislaam tu, haelewi kuwa Mtume Muhammad ni Rahma kwa walimwengu wote. Na yeye akiwemo, angemsoma tu amuelewe, angempenda akitaka asitake.

2) Mimi sio hao. Mimi Naamini Qur'an, naamini na Hadith zile ambazo hazipingani na Qur'an. Siiamini kila inayoitwa "hadith" kuwa ni ya kweli, kwa kuwa zingine ni uzushi tu.
 
Vingi sina hakika, ila kitu ambacho nina hakika hao mababu zako walioleta hii dini walikamata baadhi ya mababu zangu wakawapoka uhuru wao, wakawafunga minyororo, wakawahasi na kuwauza kama watumwa. hivyo kungekuwa na ukweli wasingethubutu kufanya huo upuuzi basi hiyo bazarkh yako iwakumbushe msingi ambao leo unawapa kiburi wengine kujiona sahihi zaidi ya wengine ulijengwa juu ya mafuvu ya watu ambao walikufa kwa mateso makubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…