Alexander mkuu alivyotabiriwa na Biblia kwa usahihi

Wapi umejibu post #25 point by point?

Niwekee post number hapa niipitie tena labda sinaiona.
Kaanze toka mwanzo, nimejibu na kukuuliza maswali ambayo hukujibu Bali ukazalisha mada mpya kama kichaka

Na sasa hutaki kabisa kuyasikia hayo maswali 😂
 
NILIKUJIBU HAPA NA KUULIZA MASWALI

NI KWAMBA HUKUYAONA AU MAGUMU ?
 
Post# 25 Mkuu.

Anza kwa kuthibitisha Daniel alikuwapo kweli na si muhusika wa hadithi ya kutungwa tu.

Kwa sababu, kama huwezi kuthibitisha Daniel aliishi kweli, huwezi kuthibitisha alifanya utabiri wowote.
 
Post# 25 Mkuu.

Anza kwa kuthibitisha Daniel alikuwapo kweli na si muhusika wa hadithi ya kutungwa tu.

Kwa sababu, kama huwezi kuthibitisha Daniel aliishi kweli, huwezi kuthibitisha alifanya utabiri wowote.
Hiki kichaka nilikujibu na maswali juu ,

Kwasasa umerudia Tena ,kwamba unakubali Alexander Great alikuwepo ,ila hutaki kukubali Daniel alikuwepo ?😂

Kwamba hiki ndio Huwa kichaka chako cha mwisho kabisa

Daniel alikuwapo kweli kama unavyoamini alikuwepo Alexander Great .

Nitakujibu Tena ,Kihistoria, tunaweza kuangalia rekodi za Mesopotamia, ikiwa ni pamoja na Babylonian Chronicles, epigrafi za kilimela, na majina ya wafalme waliotawala katika kipindi hicho,hapa sitatumia biblia kabisa .

Nebukadneza (605-562 KK), Jehoiakimu wa Yuda (609-598 KK), na utawala wa Umedi na Uajemi baada ya kuanguka kwa Babeli (539 KK).


Muundo wa mlolongo wa wafalme unaendana na utabiri wa Danieli jambo lisiloweza kufanywa na mwandishi wa baadaye aliyeandika kama hadithi bila uelewa wa kina wa majukumu ya kifalme.


Tafiti za kiakiolojia na paleography, pamoja na Dead Sea Scrolls, zinaonyesha kuwa maandiko ya Daniel yalikuwa ni ya mapema zaidi ya karne ya 2 KK, kabla ya kufariki kwa Alexander, na hayajaanza kama uhariri wa matukio yaliyotokea.

Hii inathibitisha uwepo wa Daniel na msingi wa kihistoria wa kitabu hiki. Mlongo wa falme na majina ya wafalme waliotajwa,

Babeli (Nebukadneza, Belshazari), Umedi (Darius), na Uajemi (Koresi), unaendana na rekodi za kihistoria. ,hapa sigusi biblia kabisa

Hii inaashiria kuwa anayeeandika alijua matukio ya kifalme kwa kina,hivo alikuwepo
 
Kiranga

Je, hoja yako kwamba kitabu cha Daniel ni “forgery” kwa sababu kimeandikwa baada ya Alexander, inakabiliana vipi na ushahidi wa Dead Sea Scrolls na tafsiri za paleography zinazoonyesha maandiko ya Daniel yameanza mapema, kabla ya matukio ya Alexander?


HILI SWALI NA MENGINE UMEGOMA KABISA KUYAJIBU
 
Post# 25 Mkuu.

Anza kwa kuthibitisha Daniel alikuwapo kweli na si muhusika wa hadithi ya kutungwa tu.

Kwa sababu, kama huwezi kuthibitisha Daniel aliishi kweli, huwezi kuthibitisha alifanya utabiri wowote.
Juzi juzi hapa ,watafiti na Wana AKIOLOJIA wamegundua kuwa Dead sea scrolls ziliandikwa mapema zaidi na walivyodhani awali ,awali sababu ya teknolojia duni, walidhani ni 2K.K lakini kwasasa Inaonekana ni mapema zaidi ,


Mimi na swali kwako Tena la muhimu sana ,labda tu useme huiamini sayansi

Je, unakubali kwamba epigrafi za kilimela, Babylonian Chronicles, na tafsiri za Dead Sea Scrolls zinathibitisha mlolongo wa kifalme na majina ya wafalme waliotajwa katika Daniel?

Ikiwa hivyo, je, hoja yako kwamba Daniel ni “forgery” haiwezi kuangaliwa kama kukosa kuelewa au kupuuza ushahidi wa kihistoria uliothibitishwa kisayansi?
 

Rekodi za Mesopotamia zimemtaja Daniel?

In fact, kuna rekodi yoyote ya muda aliosemwa kuishi Daniel, nje ya Biblia, inayomtaja Daniel?

Unaelewa kuwa hapa hujathibitisha kuwa Daniel alikuwapo, unatapatapa na kurudia kutumia tabiri zinazodaiwa kuwa zilitolewa na Daniel, ili kuthibitisha kuwa Daniel alikuwapo?

Yani tumeanza na tabiri zinazodaiwa kuwa alizitoa Daniel.

Watu wakahoji kama hata huyo Daniel mwenyewe alikuwapo.

Wakasema "Hang on a minute, did this Daniel fellow even exist as an actual person, or is he just a mythological made up figure that cannot stand the test of historicity?"

Halafu wewe unataka kuthibitisha Daniel alikuwapo.

Kwa kuzirejea tabiri hizo hizo ambazo watu wanasema si za Daniel kwa sababu Daniel hakuwapo?

Hujaona circular logic hapo?
 
Dead Sea Scrolls ambazo umesema zimeandikwa au kuhaririwa takriban 2 centuries Before Common Era, zaidi ya miaka 100 baada ya kifo cha Alexander 323 BCE.

Sasa ukiandika utabiri leo wa mambo yaliyotokea mwaka 1900 utakuwa umeandika utabiri au historia?
 
Yaani mi hata sielewi chochote zaidi ya mahali nilisoma danieli alitupwa kwenye shimo la masimba dangote simba wakamuonea huruma wakatemana nae
 
Kwanza tushaona majina ya wafalme, pamoja na habari nyingine nyingi tu za muda huo, yaliyoandikwa katika kitabu cha Daniel yamekosewa, hayapo sawa na ukweli wa kihistoria.

Post #25 imeandika habari hizo in detail.

Mpaka namba za mikoa ya falme, mpaka musical instruments, mpaka lugha iliyotumika.

Sasa hata kama kitabu cha Daniel kinafanana na Dead Sea Scrolls, na vyote vinakosana na historia, hapo huoni kwamba historia ndiyo tuiangalie na hayo mambo ya Daniel na Dead Sea Scrolls ni mambo ya kuungaunga tu zamani huko?
 
Kwanza unachanganya mafile ,hakuna sehemu nimesema Dead sea scrolls zilihaririwa, labda kama huzijui ,hizo ni Magombo yameandikwa kwenye ngozi, yapo hapo Israel,unaruhusiwa kuyafanyia utafiti na wengi wameyafanyia research na juzi tu hapa imeonesha yaliandikwa mapema zaidi kuliko ilivyodhaniwa awali kuwa 2K.K

Halafu ni wazi hujui hata chronology ya kitabu cha Daniel na matukio yaliyotokea ,

Kama ningeketi leo na kuandika kitabu kinachotabiri matukio ya mwaka 1900, kama vita vya kwanza vya dunia, mapinduzi ya Urusi, au muungano wa Tanganyika na Zanzibar, si utabiri wa kweli, bali historia iliyoshuhudiwa ,Hii ni tofauti kabisa na unabii halisi wa Daniel, kwa kuwa Dead Sea Scrolls na tafsiri za kihistoria zinaonyesha maandiko hayo yalikuwepo kabla ya matukio ya Alexander, na yanalingana na mlolongo wa wafalme wa Babeli na Uajemi.

Kwa hivyo, kuchukulia maandiko ya Daniel kama utabiri wa matukio yaliyotokea ni kutoelewa msingi wa kihistoria na muda wa maandiko hayo.

Hivi wewe ni msomi kweli ?
 
Unarudi kule kule tu

Kwanza sijui kama unajua historia za Mesopotamia zimejikita hasa kwenye nini,

historia ya Mesopotamia, nyingi za maandiko yaliyohifadhiwa ni chronicles za kifalme, mashirika ya kidini, au maandiko ya kitaalam ya kifalme, ambayo hayakutaja kila mtu aliye na nafasi ya kisiasa au ya kifalme. ,Ukitaka zimtaje Daniel ,kesho utauliza zimtaje Yeremia ,Paulo au Isaya.

Hata hivyo, mlolongo wa wafalme na matukio yaliyotajwa katika Daniel unalingana sana na rekodi za kihistoria zilizopo:

Nebukadneza (605–562 KK), Jehoiakimu (609–598 KK), na uhamisho wa Uajemi.

Hii inaonyesha Daniel aliishi au alijua kwa kina majukumu ya kifalme, jambo ambalo huwezi kupata kwa mwandishi wa baadaye bila vyanzo sahihi.



Aidha, Dead Sea Scrolls zinaonyesha baadhi ya maandiko ya Daniel yalikuwa yameandikwa mapema zaidi ya karne ya 2 KK, yanathibitisha kuwa maandiko hayo hayakuandikwa baada ya matukio yote kutokea, bali tayari yaliokuwa yanapatikana mapema. Hivyo, hoja ya mpinzani kwamba Daniel ni hadithi iliyoundwa baadaye au kitabu cha Daniel kimeandikwa kama “forgery” ili kuonekana kama unabii ni dhaifu kwa sababu kuna ushahidi wa kihistoria unaoendana na maandiko hayo.

Je, ukikubali kuwa maandiko mapema ya Dead Sea Scrolls yanathibitisha kuwepo kwa Daniel, hoja yako ya “forgery” bado ina nguvu?

Je, mlolongo wa wafalme na matukio yaliyotajwa katika Daniel yalingana na historia halisi, je, huoni hii kama uthibitisho wa uhalisia wa Daniel?
 
Wayahudi wamekuwa wakihariri vitabu vyao kila mara ku fit utatuzi wa matatizo ya jamii yao.

Ukimsoma Kugel na wanazuoni wengi wa Biblia utaelewa hili.

Unawezaje kuhakikisha Dead Sea Scrolls hazijawahi kuhaririwa?
 
Umezitaja rekodi za Mesopotamia kama ushahidi wa kuwapo wa Daniel.

Nimekuuliza swali dogo tu, rekodi za Mesopotamia zimemtaja Daniel?

Hujajibu swali.

Hayo mambo mengine ya kutabiri wafalme na nini si hoja, kwa sababu hayo wahariri wa baadaye wanaweza kuja kuyaweka waki edit vitabu, na kusema Daniel alitabiri.

Mimi nilifikiri utanipa rekodi za Mespoptamia za muda alioishi Daniel, zilizo nje ya Biblia, zinazoonesha kulikuwa na mtu anaitwa Daniel, alitembea juu ya moto.

Hujaonesha rekodi hizi.

In fact hujaonesha rekodi yoyote iliyo nje ya Biblia ya kuonesha Daniel aliishi muda huo mnaodai aliishi.

Kifupi hujaweka ushahidi kuwa Daniel aliishi, na si muhusika wa hadithi ya kutungwa na watu na kuungwa ungwa tu.
 
Hii hoja yako mbona dhaifu sana ,Historia ya kale haikuhifadhi kila undani wa kila mkoa au kila kifaa cha muziki kilichotumika, na lugha zilizotumika zinapaswa kuchambuliwa kwa msamiati, sarufi, na muktadha wa kifalme., hebu leta hoja NZITO NZITO na ngumu, Mimi ndio nazipenda

Tafiti za paleography zinaonyesha kwamba maandiko ya Daniel yana muundo wa Kisemi, Aramaiki na Kiyahudi wa karne ya 6 KK, na haya yanalingana na rekodi zingine za kihistoria za Babeli.

Zaidi, Dead Sea Scrolls zinazothibitisha maandiko mapema ya Daniel haziungi mkono tu bali zinaonyesha kuwa maandiko hayo yalikuwepo mapema, hayakuandikwa kama kitabu cha baadaye cha kudanganya historia kama unavyodai .

Ushahidi wa kihistoria kutoka Mesopotamia, ikiwa ni pamoja na chronicles za kifalme, epigrafi, na matukio yaliyorekodiwa, unaendana kwa kiasi kikubwa na mlolongo wa Daniel, mlolongo wa wafalme, na matukio yanayoulizwa.

Kwa hivyo, hoja kwa Daniel au Dead Sea Scrolls ni “kuungaunga tu” inakufa kifo cha mende kwa sababu kuna uthibitisho wa kihistoria unaounganisha maandiko haya na matukio halisi.

Je, ukiangalia ushahidi wa kihistoria na akolojia, bado unaweza kudai kwamba Daniel ni “hadithi tu”?

Watu wa archeology hao wanakutana na vitu kama hivi ,halafu wewe unasema Daniel hakuwepo😂😂

Ndugu jiandae ubatizwe tu

 
Mkuu,

Miaka ya baadaye tukiona kitabu cha mtu anayedai aliishi Tanzania ya leo, akaandika akakosea kupanga marais, akaandika akakosea kutaja namba ya mikoa ya Tanzania, muda mabao Tanzania ina mikoa 31, yeye akasema ina mikoa 120, tutajua huyu mtu hakuishi katika hii Tanzania ya leo anayosema kaishi.

Hili ndilo limetokea katika kitabu cha Daniel.

Muandishi kakosea kupanga wafalme, kakosea hata namba ya mikoa katika ufalme mikoa takriban 30 kaisema 120, mpaka maneno aliyotumia wasomi wameyachambua na kujua huyu muandishi hajaishi zama hizi huyu ni wa baadaye ila anafoji kuwa ni wa kabla.

Tukiangalia haya yote, kwa ujumla wake, pamoja na ukweli kuwa mpaka sasa hakuna ushahidi wowote wa nje ya Biblia kuwa Daniel aliishi wakati huo mnaosema aliishi, ndiyo tunahitimisha kuwa huyu Daniel hakuwapo, na utabiri unaosemwa kuwa aliufanya, ni longolongo zilizoungwaungwa baadaye tu baada ya matukio kupita.
 
Kiranga, unao ushahidi pia kuwa Daniel nabii hakuwepo na kwamba ni character ya kutungwa tu?

Vv
 
Wayahudi wamekuwa wakihariri vitabu vyao kila mara ku fit utatuzi wa matatizo ya jamii yao.

Ukimsoma Kugel na wanazuoni wengi wa Biblia utaelewa hili.

Unawezaje kuhakikisha Dead Sea Scrolls hazijawahi kuhaririwa?
Je, unaweza kutoa uthibitisho wa kihistoria unaoonyesha kuwa Dead Sea Scrolls zimehaririwa kuanzia karne ya 2 KK?

Je, jinsi maandiko yanavyolingana na historia ya Babeli na Uajemi, unaweza kusema haya ni matokeo ya kutunga wa baadaye?

Je, ikiwa tafiti za paleography na ink analysis zinathibitisha toleo la mapema, je hoja yako haifi kifo cha mende?
 
Hoja ya mikoa ni dhaifu, maana sidhani kama una uthibitisho kulikuwa na mikoa mingapi, naona umekazania na mikoa ,unaacha hoja na point muhimu za msingi

Kwa mfano, rekodi za Babylonian Chronicles, epigrafi, na archives za kifalme za Mesopotamia zinathibitisha uwepo wa wafalme kama Nebukadneza II (605-562 KK), Jehoiakimu wa Yuda (609-598 KK), na Koresi wa Uajemi (539 KK), pamoja na nafasi ya Darius na Belshazari.

Hii inaonyesha kwamba muundo wa Daniel kuhusu mlolongo wa wafalme una msingi wa historia halisi, na si hadithi ya kubuniwa tu.,

Pili, kuhusu Dead Sea Scrolls na tafsiri za paleography, maandiko ya Daniel yamepatikana mapema zaidi ya karne ya 2 KK, yakithibitisha kuwa hayajaratibiwa au kuandikwa kama “utabiri baada ya matukio kutokea.”

Hii inapinga hoja yako kwamba kitabu kilijazwa na matukio ya kihistoria baadaye, kwani ushahidi wa archaeology unalingana na muda wa Daniel na falme zake., Hii hoja nakujibu zaidi ya mara 5 sasa ,ila cha ajabu wewe umegeuza ni tawi hutaki kuliachia😂😂

Mlolongo wa wafalme na matukio yaliyoandikwa unaendana na historia ya kifalme ya Babeli na Uajemi.

Hii inaonyesha kuwa muandishi alikuwa na ufahamu wa kifalme na matukio ya enzi yake, jambo lisiloweza kufanywa kama angeandika kama hadithi tu ya baadaye.

Je, unaweza kuonyesha rekodi yoyote za kihistoria kutoka Mesopotamia au epigrafi zinazopingana na hoja ya “Daniel hakuwapo”?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…