Alexander Mnyeti amepata wapi utajiri wa kuinunua TCC CLUB ya Chang'ombe?

Acha "wivu" ndugu. Mambo ya kuuliza Mwanaume mwenzako amepata wapi pesa hayana mashiko. Wewe fanyakazi , pambana kivyako na wewe utazipata.

By the way, mbona huulizi Mbowe kapata wapi pesa za kumiliki majumba ya kifahari Dubai na South Africa?
 
Mquate rais ajue la kufanya
 
Nakubaliana na wewe 100%
 
Inasemekama huyu jamaa anahela toka zamani, kabla hajaingia kwenye siasa kama alivyo yule mbunge msukuma...hela za madini kama sijakosea. Ukumbuke ndie anaemiliki team ya Gwambina Fc.
 
Hawa wote hukumu inawahusu
Warudishe pesa za walipa kodi
Mali zao zitaifishwe zote
Haiwezekani hospitali zikose madawa watoto wakose mikopo kwa ulafi wa wachache
 
Yaan nyumba 10 ndio utajiri wa kutisha?.wabongo mnamambo kweli.watu wanamiliki nyumba 100 wewe unasema 10 ndio utajiri wa kutisha.
Tatizo katoa wapi hizo pesa za kujenga nyumba 10 wakati yeye ni mtumishi wa umma.
 
Kipato ni mshahara tu? Watu wanaandika write-up mahela yanamwagika tu.endelea tu na akili zero.
Unaandika write up ya wizi?
Usilinganishe Riz 1 na mnyeti.....Riz 1 ni mtoto wa Rais mstaafu
 
hapo kwenye bold ndo umezingua. hujui kama kodi ni pesa ya kunihudumia mimi?
Nimeandika hivyo kama kejeli kwa wazushi , huyu bwana amekuwa tajiri hata kabla hajaingia kwenye siasa, sio kwamba wanasiasa wote ni masikini au utajiri wao wamepata kwenye utumishi, mwishowe hata akina Msukuma,Kishimba nao mtasema wameiba ,mnasahau kuwa hawa ni Wasukuma wamepata pes akitambo sana wengi wao ni wakulima wakubwa, wafugaji wakubwa na wamiliki wa machimbo ya vito vya thamani kama dhahabu na almasi.
 
Unaandika write up ya wizi?

Usilinganishe Riz 1 na mnyeti.....Riz 1 ni mtoto wa Rais mstaafu
Na Mnyeti ni mfanyabiashara mkubwa wa siku nyingi kabla hata huyo Riz1 yuko chuo, na utajiri wake haujapatia kwenye utumishi wa serikali, sasa kuwa mtoto wa mstaafu ndio asingiziwe kila kitu.
 
Kila utawala wa ccm lazima uje na mafisadi wake na wa dikteta Magufuli ndio hao akina Mnyeti.
 
Kawadanganye majuha wenzako.
 
Kumbe ile trilioni 1.5 aliyohoji AG wa zamani ndiyo inaliwa na hawa makanjanja
 
ndio shida yetu watz, kwa kuwa unafahamu alikuwa mwalimu,unataka kwa hiyo miaka sitailiyofuata awe vile vile, fursa na akili zinabadilika kwa mtu asiyekuwa na mawazo mgando, kwa nafasi alizopitiwa na aliyonayo anakuwa na fursa nyingi tu mikopo, kilimo, ufugaji hata biashara tu za kawaida. ulitakiwa uje na hoja zenye ushahidi kwa mfano 1. kuna ufisadi huu kaufanya, kamwibia huyu, kakwepa kodi kweli hiki, n.k. lakini kusema kwa nini ana pesa za kuwa na miradi mikubwa na ninamjua alikuwa ticha......aaaahh vibaya hivyo acha ufitina...ndugu acha chuki....think big kila kukicha sio sababu alikuwa ticha unataka kumwona akiwa palepale
 
Anachimba madini misungwi
 
huyu ana visa binafsi, hii mada ifungwe...anachukia mwenzake kuwekeza tanzania bila sababu...alafu anadanganya kanunua na sio kweli, kuwekeza kukodisha bar hata milioni 20 nyingi....ukizama Access bank au vikoba unapata
 
Kuna baadhi ya watanzania wachache walifaidika mno na utawala wa mwendazake!! Walifanya watakavyo huku mzee huyo akiwachekea na kuwapandisha vyeo na kuwakingia kifua
 
huyu ana visa binafsi, hii mada ifungwe...anachukia mwenzake kuwekeza tanzania bila sababu...alafu anadanganya kanunua na sio kweli, kuwekeza kukodisha bar hata milioni 20 nyingi....ukizama Access bank au vikoba unapata
Alipata wapi mihela ya kuwekeza ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…