Ali Kamwe: Hatutacheza mchezo wa kombe la Shirikisho CRDB mpaka tulipwe pesa zetu za Msimu uliopita

Ali Kamwe: Hatutacheza mchezo wa kombe la Shirikisho CRDB mpaka tulipwe pesa zetu za Msimu uliopita

Mbumbumbu mmechoka
Mkuu, unless kwa maelekezo ya kisiasa ila kama sio hii vita hutamsikia Simba akiishupalia ataacha wauane waje na maamuzi. Baada ya kumsikia Ali kuwa kuna mwanasiasa aliagiza geti lifungwe sasa nimejua kwanini Simba anaendelea na mambo yake kama vile hayupo. Hii ni siasa 100% hakuna jingine.
 
Nakaribia kuelewa Mkuu
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Yanga ambae hajawahi kushinda kesi yoyote ile 😃 au Yanga ipi
Yanga inashinda makombe na kumfunga 5imba mara nne mfululizo kutia ndani kipigo cha mbwa mwizi cha goli 5
 
Press ya Yanga muda huu,

Pamoja na kuendelea kugomea mechi ya Derby ya Tar 15 June 2025, msemaji amesema hawatacheza mechi ya fainali iwapo hawatalipwa pesa za ushindi wa kombe la CRDB la msimu uliopita.

"Hatutacheza mchezo wa kombe la Shirikisho CRDB mpaka tulipwe pesa zetu za Msimu uliopita, maana tumechekeana sana na hizi taarifa zifike kwenye ofisi za Mtendaji Mkuu wa TFF"

Taarifa zaidi inakuja
Ikiwa timu kubwa kama Yanga inakopwa,vipi timu hizi nyingine ndogo zinazo shiriki, vipi marefa wanao chezesha hizo mechi, vipi mfungaji bora, vipi mchezaji bora wa hiyo michuano? nk.

Mpira wa bongo unaongozwa na wahuni. CRDB lazima watatoka kuongea kulinda brand yao, ila nina uhakika hela ambayo Yanga wanadai, CRDB washawapa TFF, ila sasa TFF wahuni na hii hela CRDB unaweza ukakuta anaingiza ndani dk chache tu. Mpaka hapa ndio muone hawa TFF hawa muheshimu hata mdhamini na ndio maana hata April nane mechi walihailisha,sababu hawamjali mdhamini NBC,hawamjali Azam nk.Juzi tu Liver na Man Anified kulikuwa na barafu kibao, tena hii sababu ya hali ya hewa ni sababu ya msingi kabisa ya kuhairisha mechi, lkn watu wakaa chini na watalamu wa viwanja, wakaangalia wakasema hapa kinapigwa na kweli mechi ikapigwa. Sababu ukihailisha mechi wadhamini unawapa hasara, kwani wanategemea airtime kupitia hiyo mechi, yule mrusha matangazo nae umempa hasara sababu katumia gharama kubwa kuleta magari ya matangazo, kusafirisha watu, kufunga camera nk,bado mashabiki wamenunua tickets nk.

Ila ndio hivyo soka letu kivyetuvyetu, viongozi wahuni na hawataki kuwajibika, kanuni wanatunga wenyewe ila wakivuruga wanakimbilia hekima na busara.
 
Itakuwa, maana hadi leo vodacom anadaiwa pesa ya udhamini wa ligi kuu, naona crdb anapita mulemule
Vodacom watakuwa wanasingiziwa, hawana uhuni huo halafu kampuni ya wazungu haina ubabaishaji, hiyo hela anayo aliyo itumia kudhamini hii ligi lenu unaweza kuta haizidi hata asilimia moja ya mapato yake. Huu mzigo utakuwa umepigwa na wahuni wa TFF.Hizi kampuni binafsi, Reputation ya brand zao zinalindwa kwa gharama kubwa, hawawezi kufanya huo ujinga.
 
CRDB walipeni Yanga, aibu kabisa tokea msimu uliopita hadi sasa hamjawalipa.
Wameshafanya utafiti wao, na wakagundua hela tayari ilishatua TFF.
Yanga wana viongozi makini na wanaojielewa.
Klabu inaudhamini na CRDB, si rahisi kuwaaibisha wadhamini wao kama hawana uhakika na jambo hilo.
 
Vodacom watakuwa wanasingiziwa, hawana uhuni huo halafu kampuni ya wazungu haina ubabaishaji, hiyo hela anayo aliyo itumia kudhamini hii ligi lenu unaweza kuta haizidi hata asilimia moja ya mapato yake. Huu mzigo utakuwa umepigwa na wahuni wa TFF.Hizi kampuni binafsi, Reputation ya brand zao zinalindwa kwa gharama kubwa, hawawezi kufanya huo ujinga.
Kumbe sakata la vodacom lilikupita, voda alidaiwa pesa ya misimu mitatu mfululizo, alikuwa anatoa kidogo kidogo.
 
Back
Top Bottom