Ali Kiba anadai kila mtu kazaliwa Muislamu na kwamba Wakristo wote ni watu waliobadili dini

Ukristu na Uislamu upi ulitangulia?

Hizi mbili ni dini za kurithi
Kila mtu huzaliwa bila dini ( Ali Kiba acha uzushi)

Ninyi wawili oops mko watatu ni wa dini sana

Kwa Mungu hakuna dini msipotoshe na kuwapotezea watu muda

Maisha yako na matendo yako ndio dini yako

Ufuska umalaya ujambazi uchawi nazo ni dini za watu kwani ni Imani ujue....

Huyu anayetangatanga mara mksristo mara kasababisha kifo cha nani yake mara msaidia yatima nk ndio wakumjadili kweli???
 
Hii angetamka domo, Mange hili angelivalia njuga plus la kuchumpa.

Kwa mtu kama Kiba kwa brand yake hakutakiwa kusema hivyo,mimi naamini maswala ya imani ni utashi wa mtu, Mungu alimpa binadamu utashi achague lilojema, huku tukiongozwa na mitume na manabii wa Mungu.

Ila mwisho wa siku hamna dini nzuri kama ya UPENDO, mpenda Mungu wako,majirani na pamoja maadui zako.

Uwe Muislamu au mkristo kama huna upendo ni kazi bure.
 
Logicaly ni kwamba dini ni ubunifu wa mtu

Alianza mtu ndio zikaja dini

Mtu ndio aliyeanzisha dini

Dini haijaanzisha mtu

Mpaka hapo utaona atheist ni default position ambayo kila mtu kaipitia
 
Muislam hata awe Profesa,dini Kwake ina ushawishi mkubwa!sasa fikiria mtu anaamini huu upuuzi,kwamba mtu anazaliwa akiwa na dini!!
Ujinga mtupu.
 
Dini ni moja tu toka Adam mpaka Muhammad wote walihubiri uislam
 
Hawezi kucha kusimamia dini kisa eti brand yeye anamwamini mungu wake.
 

Apeleke matumizi kwa mke wake mengine tutajadili
 
Haya uliyoyaandika wewe labda ulaya sio tz mzee, huku watu wapowapo tu. Kuhusu kauli ya ali nadhani yupo sahihi kwa mujibu wa imani yake
 
Mkuu msamehe tu maana ukifuatilia vitendo vingi vya kiba utajua kuwa ana level ndogo ya maturity and intellectual capacity
Na bado anajiona ni special. Kumbe ni kiazi.

Hajui anajifanya anajua.

Watu wetu wanakua public figures bila kujua values and what it takes kuwa public figure. Ama meneja wake naye ana matatizo kwa kushindwa kumtengeneza msanii wake, au ni ubishi na ujuaji wake.
 
Kimsingi mtu anazaliwa bila dini ndio maana baadhi ya imani / madhehebu ya kikristo mtu anabatizwa.

There is no way ukasema mtu anaziliwa muislamu wakati familia anayozaliwa ndio inayoenda kumuamulia imani yake.

Yaani mtu akizaliwa familia ya kiislamu anakuwa muislamu, akizaliwa familia ya kiyahudi anakuwa myahudi mpaka pale atakapokuja kubadilisha mwenyewe.

Hii hoja ya ally ni ya mtu ambaye hatumii kichwa chake vizuri kuung'amua ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…