Nimekupa hoja hapo ya kuonesha mazingira gani yanaweza kusababisha ushindwe kumjua mbunifu
Sio kila mtu anapenda kuwekwa public
Sio kila neno lilitotungwa linaweza kunulikana na wote
Chukulia mfano wa hapa hapa bongo kuna maneno recently mangapi ambayo yanabuniwa na watu na yanatumika kila siku ila haijulikani mtunzi?
Neno demu, msela, mrume, vishoka, kudanga nk.
Maeno hayo bila shaka ushawahi yasikia na unaelewa yakitajwa yana maanisha nini na si ajabu miongoni mwa maneno hayo hata wewe unayatumia
Vipi unabisha kwamba maneno hayo hayajabuniwa na watu?
Bila shaka huwezi kubisha
Vipi unawajua waliobuni hayo maneno ni kina nani?
Huwajui eeh?
Sasa kama utashindwa kujua mbunifu wa maneno ya miaka ya karibuni utawezaje kujua maneno ambayo yana miaka elfu?
Sasa kama utataka kulazimisha hapa kwamba kila neno lazima liwe na muundaji na asipo julikana basi neno hilo lilikuwepo na halina chanzo itabidi uniambie nani mtunzi wa neno Mziki, Kilimo, nk. Kitu ambacho najua huwezi
Kama huwezi kujua inventors wa hayo maneno basi huna authority ya kupinga hoja yangu kwa kigezo cha kutomjua mbunifu wa neno DINI