Afadhali umekubaliana na karibu kila tuzo hulalamikiwa. Sasa sababu ya kulalamikiwa ndizo hizo sarakasi zilizomo kwenye hizo tuzo. Na ndicho nilichokisema, kwa maana ya kwamba Adele aliweka rekodi ya tuzo nyingi, lakini Nicki Minaj akauza sana album. Kama Davido kupata tuzo nyingi, lakini 2 Face Idibia akauza nakala nyingi za album.
Nijuavyo, maana ya mifano mfu ni ile ambayo haipo, lakini mimi nimekuwa mifano ya historia ya maisha ya muziki, kwani kiazi chetu tunajifunza kufuatana na historia kwa maana ya kumbukumbu, ndio maana leo tuna vitabu vitakatifu ambavyo vina miongozo ya matukio na maisha ya zamani.
Sasa kama mfano wa historia ya yaliyopita kwenye maisha ya muziki unaita mfu, unahitaji nini zaidi? Sijui kama unajua kama vitabu vinavyouzwa sana ukiondoa vya novel, ni vile vya kumbukumbu za watawala na watu mashuhuri waliopita kwa ajili ya watu kutaka kujifunza kupitia kwao.
Mifano niliyotoa ina maana kwamba unaweza ukawa mkali lakini bado usipate tuzo. Sikuwahi kutoa mfano wa asiyestahili kupata tuzo, kila anayefanya sanaa anaweza kupata tuzo au akakosa, lakini tuzo ni tofauti na matokeo ya darasani kwa maana ya uwezo halisi.
Katika tuzo ni tofauti, watu mtapiga kura nyingi muwezavyo lakini zinapewa asilimia 10 tu katika ushindi, kisha kuna kundi la watu watajifungia ndani na kuamua kwa muono wao kuwa huyu na huyu ndio washindi, kama unavyojua kila binadamu ana utashi wake.
Ndio maana tunaona Casper Nyovest kapata tuzo nyingi kwa wimbo wake wa Doc Shebeleza, lakini katika kufuata hisia za wapenzi wa muziki, huo wimbo wa Doc Shebeleza umeweza kuupoteza Y Tjukutja wa Uhuru alioimba na akina Professor, Oskido na Dj Bucks? Umeupoteza Khona wa Mafikizolo?
Ova