Alichoandika MwanaHistoria Mohamed Said, Baada Tamko La Askofu Rais Wa TEC

Ni kweli mambo ya dini hayana inshu?
Maana uhuru ulipiganiwa na watu na watu hao walikuwa na dini. Je ni kosa kusema watu wa dini fulani walipigania uhuru? Au itumike misamiati gani ili walau kuepuka kutaja dini?
Naomba tujadili hili.
Tofauti na mnavyotaka kutuaminisha ni waislamu wachache walipigania uhuru kwa ajili ya waislamu peke yao. Waliofanya hivyo hawakufanikiwa kabisa. Aidha, hamna mmisheni aliyepigania uhuru kwa ajili ya wamisheni wenzake peke yao.

Hatukatai watu kutajwa dini zao, sisi tunakataa kuwatambulisha zaidi na dini zao kuliko utanganyika wao. Waislamu na wakristu wa Lindi hawakwenda kumsikiliza Mwalimu kwa ajili ya dini yake. Walienda kwa sababu ya utanganyika wake. Ilikuwa hivyo hivyo kwa watu wa Mbeya na kwengine kulikosheheni wakristu.

Kusema kuwa mkatoliki Julius alihitaji ulinzi wa waislamu dhidi ya wakristu wenzake alipoenda kusali kanisani kwake ni uongo uliopitiliza. Badala ya kuwa simulizi ya jinsi watanganyika wa Lindi walivyomuunga mkono kiongozi wao katika kudai uhuru mmeigeuza kuwa simulizi ya jinsi waislamu wa Lindi walivyounga mkono juhudi hizo.
Kwa kweli haipendezi kabisa.

Amandla...
 
Huyu mzee ndie aliyeongoza waislamu wa magomeni kwenda kuvamia na kubomoa mabucha ya nguruwe pale magomeni,sijui sahivi anajiskiaje akiona magomeni watu wanavyo kula kitimoto bila hiyana,what a shame.
 
Uhuru na historia yake aliiua mwalimu nyerere na watu wake.
Mtu asiyejua historia yake ni sawa sawa na mti uso na mizizi. Ndiyo maana hata mapapai makubwa tuliyopanda wenyewe mashambani mwetu tunayaita ya " KIZUNGU"
 
Asante Pasco
Aione mzee wangu Mohamed Said
 
Ni kweli kabisa hata Mkuu Alamaa Mohamed Said , amesoma shule ya mission!. Waislamu mliofanikiwa kwa Elimu ya Shule za Mission badala ya Madrasa kuweni na Shukrani kwa Wakristo waliowafikisha hapo mlipo

P
 
Anasema lindi ulikua mji wawaislam anasahau huo uislam wenyewe uliletwa nawawaarab lindi ulikua mji wamababu zetu ukiwa naiman zakiafrika
Lindi ... ulio na jina lisilo kama 'Dar es Salaam' ambalo si la ki-Mzizima. Wavuvi wenyeji wameishi pale na historia ya pale haikuanzia ujio wa dini yoyote iloletwa na wageni.
 
Huyu angekuwa kijana angeshajiunga na wale wa somalia walioingia kibiti😁
Wakiristo kuandika hamuwezi iliobaki kuwachukia wanaoandika ukweli. Mumezoea kujinasibu nyie wasomi, akitokea wa kukuzidi akili na maarifa mnamchukia
 
Ukizifuta utakosa kujua hata maeneo amboyo unakosea wewe kama kiongozi au watendaji wako. Hayo matamko yanasaidia pia.
 
Shule za mission na hospital za mission zimejengwa kwa fedha za sadaka za Wakristu. MOU ni kwa
Hospital za mission, hata Bakwata walikuwa na hospital na ziligharimiwa na serikali.
P
Shule za mission na hospital za mission zimejengwa kwa fedha za sadaka za Wakristu. MOU ni kwa
Hospital za mission, hata Bakwata walikuwa na hospital na ziligharimiwa na serikali.
P
Mkuu hata wewe? Unatudanganya?
 
Watu wa aina hii, kama wangekuwa wao tu hapa nchini, wangeikabidhi hii nchi kwa Waarabu wa Saudi Arabia:

Na hata hawajiulizi kabisa:
Kuwa wao wanathaminiwaje huko kwa Waarabu ambako hata vyeo vya kiserikali tu huwa hawapewi watu weusi hata kama ni wa dini yao:

Hakuna Kiongozi Mwafrika Mweusi hata mmoja huko kwenye nchi za Kiislamu:

Ni kwamba watu wetu weusi wameridhia kuwa watumwa wa Mwarabu:

Huyo Mzee anayejiita Msomi amepewa dhamana gani huko Uarabuni ?

Na hata akienda kuishi huko hapewi hata ujumbe wa serikali ya mtaa:

Kwakweli inasikitisha sana:
Babu zetu wamesahaulika kabisa na anakumbukwa Mwarabu tu:

Ukiitwa jina la Kiarabu ndio unaheshimika:
Msomi mzima unakuwa mtumwa wa Fikra
 
Sijasoma...
Kwanini mambo mazito kiteknolojia wanagundua sana wazungu na wengi ni wakristo?? Alafu mtu anakupigia kelele eti makafiri wanakula nguruwe haya waarabu wasiokula wamegundua Nini??
Wewe umegundua nini hadi sasa? Hujuj hii dunia mungu kila kiumbe kimepewa jinsi ya kuishi siyo lazima wewe ufanye kama anachofanya mwenzako, huwezi ukategemea kuku akupe maziwa hiyo ni kazi ya ngombe, ndio maana mchina yeye ndio most industrilized nation on earth, huku muarabu akitumia maliasili zake vizuri na watu wake kuishi maisha mazuri kuliko mataifa mengi ya ulaya na marekani
Libya tu hapo gaddafi aliigeuza ikawa inakopesha hela karibia africa nzima hadi wazungu wakamgeuza adui,
Wewe soma usomavyo mwisho wa siku huwezi kushindana na bakhressa au gsm, wewe ni working class mungu kakuumba hivyo ukimaliza upeleke bahasha uajiriwe na gsm ambaye hakusoma ndio maisha yalivyo
 
Wakiristo kuandika hamuwezi iliobaki kuwachukia wanaoandika ukweli. Mumezoea kujinasibu nyie wasomi, akitokea wa kukuzidi akili na maarifa mnamchukia
Mm ni shekh buana

Anyway goodnight fela usiku umeingia sasa hapa nilipo
 
Mantiki yake ni nini?!
Inside10,
Sikutegemea hata kidogo kama post hii yangu itagusa watu wengi kiasi hiki.

Nimeamua In Shaa Allah kukuelezeni historia yote vipi TANU iliingia Lindi na Southern Province yote kama nilivyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes (1998):

TAA mjini Lindi ilikuwa chini ya uongozi wa Suleiman Masudi Mnonji aliyekuwa Rais na Katibu wake alikuwa Mohamed Waziri. Mnonji alikuwa fundi cherahani na Waziri alikuwa mchoraji wa ramani za nyumba. TAA ilichelewa kuanza mjini Lindi. TAA ilianzishwa Lindi mwaka 1953 wakati uongozi wa TAA mjini Dar es Salaam si tu ulikuwa unaigeuza TAA kuwa chama cha siasa bali ulikuwa ukifanya mipango kumpeleka mjumbe wake Umoja wa Mataifa kudai uhuru.

Masudi Mnonji alikuwa na uzoefu wa kutosha katika siasa. Baada ya Vita Kuu ya Pili alikuwa amejaribu kuanzisha vyama vya wafanyakazi katika mashamba mbalimbali ya mkonge kusini mwa Tanganyika. Vilevile aliwakusanya wapishi na madobi mjini Lindi waanzishe umoja wao. Ilikuwa kupitia juhudi zake binafsi TAA ijapokuwa ilichelewa, ilikuja kuanzishwa mjini Lindi na Mnonji alijitolea nyumba yake katika mtaa wa Makonde kama ofisi ya chama.

Mnonji kwa kutambua umuhimu wa kuwa na uongozi ulioelimika vizuri, alimleta Nangwanda Sijaona kutoka Nachingwea aje aishauri TAA jinsi ya kufanya mambo kwa utaalamu. Wakati huo mjini Lindi kulikuwa na chama cha wafanyakazi bandarini Dockworkersí Union chini ya uongozi wa Mussa Athumani Lukundu, chama ambacho kwa kiasi chake kilianzisha vuguvugu la siasa za vyama vya wafanyakazi. Ingawa vyama hivi viwili, yaani TAA na Dockworkersí Union vilikuwepo katika mji mmoja, siasa za hiki chama cha pili cha wafanyakazi bandarini hazikupitia TAA kama ilivyokuwa mjini Dar es Salaam. Hii kidogo ilidhoofisha mwamamko wa siasa kwa wananchi.

Jimbo la Kusini lilikuwa katika usingizi mzito wakati sehemu nyingine Tanganyika zilikuwa zikipiga hatua kwenda mbele zikiandaa vita dhidi ya utawala wa kikoloni. Chanzo cha usingizi huu mzito huko kusini ulikuwa na asili yake katika historia ya Tanganyika.

Vita vya Maji Maji vilipoanza kusini ya Tanganyika mwaka 1905 kwa nia ya kuwafukuza Wajerumani kutoka Tanganyika, zile sehemu zenye Wakristo wengi zilikataa kujiunga na vita na badala yake wakajiunga na majeshi ya Wajerumani na kupigana bega kwa bega na dhidi ya wazalendo.

Hii ilitokana na sababu ya kuwa uasi dhidi ya dhulma wa Wajerumani ulianza katika maeneo yenye Waislam wengi na vita vikachukua sura ya vita vya Kiislamu dhidi ya Wazungu ambao dini yao ni Ukristo. Kwa kuwa wamishonari walikuwa washirika wa wakoloni, walichukuliwa kama maadui na hivyo ikawa vituo vyao vinashambuliwa na wapiganaji wa Maji Maji.

Kutokana mashambulizi haya, Wakristo walivichukua Vita Vya Maji Maji kama vita dhidi ya Ukristo. Harakati za Maji Maji zilishindwa na Wajerumani walifanya ufisadi kubwa dhidi ya wananchi na viongozi wao. Jambo hili liliacha kovu kubwa katika fikra za wananchi na kwa upande wa Wakristo ambao walinusurika na ghadhabu ya Wajerumani, wengi wao wakajiweka mbali na aina yoyote ya kupinga ukoloni.

Kufuatia historia hii Waafrika waliokuwa kusini ya Tanganyika sasa wakiwa chini ya utawala wa Waingereza na kuwa chini ya himaya ya wamishonari walipumbazwa kiasi kiasi kwamba waliogopa siasa. Baada ya Waafrika kushindwa vita kwa silaha kali za Wazungu sasa Kanisa likaona ndani ya fadhaa ile fursa yao kutawala sehemu hiyo kwa kutoa vishawishi kama vile shule na hospitali.

Kwa hiyo Wamishionari na Waingereza walionekana kama mabwana wema wenye kuwajali raia zao kinyume na serikali katili na ya kidhalimu ya Wajerumani. Vuguvugu la siasa kama ilivyokuwa Vita vya Maji Maji, lilianza katika maeneo ya Waislam kufuatia mfumo ule ule kama ilivyokuwa katika upinzani wa ukoloni wa Wajerumani. Wakristo katika Jimbo la Kusini waliiona TANU kama walivyoviona Vita Vya Maji Maji, kama harakati nyingine za Waislam zilizokuwa zinakuja tena kwa mara ya pili kuvuruga amani na utulivu.

TANU ilipoanza ikawa inavuma kuwa safari hii Waislam walikuwa wamemua kuanzisha vita dhidi ya Waingereza kama walivyoanzisha vita na Wajerumani.


Tafsiri hii ya Kiswahili ya kwanza imechapwa na Phoenix Publishers, Nairobi 2002.

(Itaendelea...)
 
Fundi...
Wewe huipendi historia hii lakini wengi wameipenda na kunipa tuzo zinafika tano:



Tafsiri ya kwanza ya Kiswahili haikuchukua muda vitabu vyote vilivyokuwa
sokoni vikamalizika ikabidi vichapwe vitabu vingine India.

Angalia hapo chini:

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…