View attachment 1058576"watu kama wakina Pierre sijui,watu wa hovyo hovyo ndio wanakua maarufu watu wa maana hawajulikani,tunajenga jamii ya watu gani?"
Haya ndio maneno ya Makonda wakati anahutubia kwenye tamasha la tokomeza zero Kisarawe,lililofanyika jana Mlimani City,ambalo pia Pierre alikuwa moja kati ya watu waliohudhuria.
Hivi mtu kama Pierre kuwa maarufu yeye inamuuma nini? anaposema ni mtu wa hovyo katika lipi? kati ya Pierre na hao wasanii wake ambao daily wanshinda makahamani kwa kesi za hovyo hovyo,wanatukanana mitandaoni live,wanavujisha picha za ngono mitandaoni,wanabadili wanawake/mabwana kila uchwao na bado anawahusudu na kuwaona wa maana nani ni wa hovyo sasa?
Muache mzee wa watu aingize kipato chake kihalali,ilimradi havunji sheria za nchi.