Aliingilia Msafara wa Mwenge na hicho ndicho Polisi waliamua kumfanyia. Je, ni haki?

Aliingilia Msafara wa Mwenge na hicho ndicho Polisi waliamua kumfanyia. Je, ni haki?

Acha kuwa na hisia za ajabu.
Mambo mengine tumia akili ya kawaida tu, we unavoona kaonewa..?

Sometimes hilo kama funzo tu, kwani wanajeshi ujaskia mara ngapi wanakamata watu wana wambia wagale gale hilo sula unazungumziaje..?
Hiyo ndiyo adhabu aliyostahili ?
Je ungefanyiwa wewe hivyo au kuambiwa ugalegale kwenye tope ungefurahia na kuridhia ufanyiwe hivyo.?
 
Acha kuwa na hisia za ajabu.
Mambo mengine tumia akili ya kawaida tu, we unavoona kaonewa..?

Sometimes hilo kama funzo tu, kwani wanajeshi ujaskia mara ngapi wanakamata watu wana wambia wagale gale hilo sula unazungumziaje..?
Sheria zetu hazijasema mtu akitenda kosa mzigo wake utupwe mtaroni.

Sheria zetu hazisemi mtu akifanya kosa agalegale kwenye tope na vumbi.

Ungefanyiwa wewe hivyo ingekuwa sawa ?
 
Sasa huyo jamaa alikuwa hajuwi kuwa hahusiki kwenye huo msafara??

Anaingia wakati hahusiki alitegemea nini?
Ikitokea kwa bahati mbaya hajafajamu, basi anakamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi mpaka mwenge upite halafu anapelekwa kituoni na mizigo yake anafanyiwa uchunguzi kama hakuwa na dhamira ya uhalifu basi anaonywa na kuachiwa na siyo kumwaga chakula kwenye mtaro. Haya, hebu tupe logic ya polisi kumwaga chakula kwenye mtaro!
 

Jamaa aliingilia msafara wa Mwenge huko Bariadi, Simiyu, Kijiji cha Nkololo. Hivi ndugu zetu baadhi ya askari na mgambo, mbona mna roho ngumu hivi? Haya maisha hamuwazi kwamba nafasi zenu zitaisha?

Kama alingilia msafara wa Mwenge, si kuna sheria zinazoweza kufuatwa? Huenda bwana huyu alikuwa amebeba maharage yake akienda kutafuta riziki ya watoto wake, lakini mnafanya hivi.

Kumbukeni hili kabla ya kuumiza maisha ya mtu; fikirieni kwanza watu wanaomtegemea nyuma yake.

Katika hii dunia ya Mungu, hebu tutende wema kuliko ubaya. Tuwekeze zaidi katika matendo ya huruma, utu na upendo kwa wengine.

Hata ukiwa kwenye nafasi ya cheo au mamlaka, kumbuka kuwa madaraka ni ya muda, lakini wema unaowatendea watu hubaki kwenye kumbukumbu zao.

UPDATES

ANAANDIKA TWAHA MWAIPAYA

TAARIFA KAMILI YA KIJANA ALIEPIGWA NA POLISI KWENYE MSAFARA WA MWENGE.

Tukio hili limetokea Kijiji cha Nkololo Kata ya NKOLOLO Wilaya ya BARIADI, Kijana mwendesha bodaboda aliepakia alizeti kwenye pikipiki yake aliingia barabarani kutoka barabara za mitaa inamaana alikuwa HAJUI kinachoendea njia Kuu alivyotokeza ghafla Polisi walimsimamisha kwa Kasi ikawa ngumu kusimama kwa haraka kama unavyojua vyombo vya Moto.

Baada ya kusimama Polisi na mgambo wakaanza kumpiga hapo mchukua video amechukuwa wakati Kijana huyu ameshapigwa, Baada ya kipigo wakamwaga alizeti zake mtaroni kama inavyoonekana kwenye video.

Kisa cha yote haya ni MSAFARA wa MWENGE kama unavyoona mwisho wa video hii inaonekana MSAFARA wa MWENGE unapita.

Baada ya hapo Kijana huyu alikamatwa Mpaka sasa yupo kituo cha Polisi Nkololo.

Kwa SASA nimempata MTU aliechukuwa video ya tukio nikamuomba video za ziada amenitumia.

Baada ya tukio hili kusambaza mtandaoni Polisi wamemfuata mtu aliechukuwa video na kusema watamkomesha kwa SASA Kijana aliechukuwa video yupo katika mashaka makubwa, anahitaji Masada wetu aweze kuondoka kijijini hapo kuokoa maisha yake.

Amenipatia namba yake kwaajili ya Msada wa dharula nimeshindwa kuiweka hapa Namba kwaajili ya usalama wake, kama kuna MTU anahitaji kumpa msaada wa haraka aje inbox.

Pia tunaomba wanasheria wafuatilie ili dereva BODABODA aachiliwe huru

Naomba tupate sauti Vijana hawa wawe salama.


Soma Taarifa ya Polisi kuhusu Tukio hili
Sawa kafanya kosa. Je, sababu ya polisi kumwaga chakula ni ipi?
 
Mamlaka yakizidi akili, matokeo yake ndio haya tunayoyaona Simiyu.
 
Amenipatia namba yake kwaajili ya Msada wa dharula nimeshindwa kuiweka hapa Namba kwaajili ya usalama wake, kama kuna MTU anahitaji kumpa msaada wa haraka aje inbox.​
Hii n akili au matope?
Sasa vp wanaotaka kumkamata jamaa wakitumia hii nafasi ili waipate namba ya jamaa ili watimize kumkamata?
 
Tukio linalodaiwa kutokea katika Kijiji cha Nkololo, wilayani Bariadi, mkoani Simiyu, limezua mjadala mkubwa baada ya video/Picha inayomuonesha dereva wa bodaboda akiwa amebeba gunia la maharagwe yenye uzito wa zaidi ya kilo 100 kusambaa mitandaoni.

Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa, dereva huyo anadaiwa kuingilia msafara wa Mwenge wa Uhuru, hali iliyosababisha askari polisi kumzui

Katika video hiyo, baadhi ya askari wanaonekana kulifungua gunia la maharagwe, huku mmoja wao akidaiwa kulisukumia mtaroni. Gunia hilo lilidaiwa kutoboka na kusababisha maharagwe kumwagika chin

Tukio hilo limeibua maoni tofauti, huku baadhi ya wananchi wakisema kuwa iwapo dereva huyo alivunja sheria, hatua za kisheria zinapaswa kuchukuliwa kwa mujibu wa taratibu. Wengine wamehoji namna ambavyo mali yake ilishughulikiwa, wakisisitiza kuwa utekelezaji wa sheria unapaswa kuzingatia utu, uwajibikaji na matumizi sahihi ya mamlak

Wito umetolewa kwa vyombo husika kuchunguza mazingira ya tukio hilo na kutoa ufafanuzi, pamoja na kuchukua hatua stahiki endapo kutabainika kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria au matumizi mabaya ya mamlak
a
1786003538755.jpg
 
Back
Top Bottom