View attachment 3643423
Jamaa aliingilia msafara wa Mwenge huko Bariadi, Simiyu, Kijiji cha Nkololo. Hivi ndugu zetu baadhi ya askari na mgambo, mbona mna roho ngumu hivi? Haya maisha hamuwazi kwamba nafasi zenu zitaisha?
Kama alingilia msafara wa Mwenge, si kuna sheria zinazoweza kufuatwa? Huenda bwana huyu alikuwa amebeba maharage yake akienda kutafuta riziki ya watoto wake, lakini mnafanya hivi.
Kumbukeni hili kabla ya kuumiza maisha ya mtu; fikirieni kwanza watu wanaomtegemea nyuma yake.
Katika hii dunia ya Mungu, hebu tutende wema kuliko ubaya. Tuwekeze zaidi katika matendo ya huruma, utu na upendo kwa wengine.
Hata ukiwa kwenye nafasi ya cheo au mamlaka, kumbuka kuwa madaraka ni ya muda, lakini wema unaowatendea watu hubaki kwenye kumbukumbu zao.