Aliniacha kisa ex wake tena anataka kurudi kwangu

Ok nimekuelewa ukweli alinambia kua alikua na bwana wakazinguana harafu mi nilimkuta wakati yupo na depression baada ya hapo ndo kamrudia tena ila ninahasira nae sana nataka nimfanyie kitu ambacho hata sahau kwa sababu aliniachia maumivu nikasahau tena jana kaanzisha mengine

Hii mission mbona kama nmeielewa, au ni kwamba nawaza kwa sauti.😁🤔
 
Atakuwa mtu sahihi kwako mpe nafasi Tena.
Mtu anaejirudi kwako ni Bora zaidi amekuthamini
 
Wakuu kwanza nikili nimetumia ID nyingine tofauti na ninayotumia.

Kuna dada ambaye nilikutana nae na tukawa katika mahusiano kumbe kipindi nimetoka kumtafuta alikua ameachana na huyo ex wake.

Sasa katika mahusiano yetu tulipendana sana yeye alionyesha kunijali japo sijui rohoni alikua ananiwazia nini, tumekaa katika uhusiano zaidi ya miezi sita bila ugomvi wowote.

Ila baada ya hapo nikaanza kuona tofauti nikamuuliza mbona unakuwa kama mbali shida nini akasema hapana na bahati mbaya baada ya siku kama nne mbeleni mimi ( wezi waliingia nako kaa waliruka fensi na kukaa ndani wakawa wananisubiri nirudi sababu walikua wanajua nafanya kazi za mobile money) na yeye siku nne hizo alikua na safari ya mikoani, nikampa taarifa kuwa nimeibiwa na wameniumiza .

Sasa kipindi naendelea kuuguza jeraha kama wiki tatu mbele nikakuta mesji,
yeye: upo poa
Mimi: nipo poa nambie
Yeye: safi nikwambie kitu ila usinune
Mimi: sawa nakusikiliza
Yeye: i m sorry naona kwangu mda wa kuolewa umefika so nataka kuolewa naomba nisameheme
Mimi:💔

Jana kanitafuta nikachati nae kumbe karudi alikokua yupo nyumbani kwao ambapo pia ni karibu na kazini kwangu, akaja maeneo ya kazi akawasalimia majirani wa pale kwangu hakuja alivotoka jana kanitumia meseji akaa kidogo akapiga simu naomba nisamehe turudiane nilikosea nimejifunza nisamehe sana mi nikamjibu nitakupigia, sasa wakuu nimwambiaje maana nina hasira sana japo alipiniacha sikuonyesha kama nina hasira nae sana nikawa namjibu kawaida sana ila ukweli niliumia sana.Baadhi ya meseji za nyuma na janaView attachment 2707339View attachment 2707335View attachment 2707337
Mkuu wewe si ni wakala? Huyo binti ni kama wale matapeli wanaopiga simu kutaka kukuibia tu.

Ukiwagundua ni unakata simu na kuwaripoti polisi.
 
Kurudiana na ex ni kosa kubwa sana kwenye maisha
 
Kama una upwiru mpelekee moto tu, ila ukitaka habari za kumpenda sijui sikua watarudiana tena na ex wake
 
Wengi huwa wanarudi baada ya kupigwa matukio walikoenda. Watu wa hivi mara nyingi hawana nia njema.
Wametambua makosa Yao kwa kuumwa na nyoka,shida ni kuishi kwa kutofuta Yale waliyotutendea utumia Nia hio kuwalipizia kisasi au kuwashusha thamani
 
Wakuu kwanza nikili nimetumia ID nyingine tofauti na ninayotumia.

Kuna dada ambaye nilikutana nae na tukawa katika mahusiano kumbe kipindi nimetoka kumtafuta alikua ameachana na huyo ex wake.

Sasa katika mahusiano yetu tulipendana sana yeye alionyesha kunijali japo sijui rohoni alikua ananiwazia nini, tumekaa katika uhusiano zaidi ya miezi sita bila ugomvi wowote.

Ila baada ya hapo nikaanza kuona tofauti nikamuuliza mbona unakuwa kama mbali shida nini akasema hapana na bahati mbaya baada ya siku kama nne mbeleni mimi ( wezi waliingia nako kaa waliruka fensi na kukaa ndani wakawa wananisubiri nirudi sababu walikua wanajua nafanya kazi za mobile money) na yeye siku nne hizo alikua na safari ya mikoani, nikampa taarifa kuwa nimeibiwa na wameniumiza .

Sasa kipindi naendelea kuuguza jeraha kama wiki tatu mbele nikakuta mesji,
yeye: upo poa
Mimi: nipo poa nambie
Yeye: safi nikwambie kitu ila usinune
Mimi: sawa nakusikiliza
Yeye: i m sorry naona kwangu mda wa kuolewa umefika so nataka kuolewa naomba nisameheme
Mimi:💔

Jana kanitafuta nikachati nae kumbe karudi alikokua yupo nyumbani kwao ambapo pia ni karibu na kazini kwangu, akaja maeneo ya kazi akawasalimia majirani wa pale kwangu hakuja alivotoka jana kanitumia meseji akaa kidogo akapiga simu naomba nisamehe turudiane nilikosea nimejifunza nisamehe sana mi nikamjibu nitakupigia, sasa wakuu nimwambiaje maana nina hasira sana japo alipiniacha sikuonyesha kama nina hasira nae sana nikawa namjibu kawaida sana ila ukweli niliumia sana.Baadhi ya meseji za nyuma na janaView attachment 2707339View attachment 2707335View attachment 2707337
Mrudishe,fumua ndogo kwa fujo then mtimue
 
Mtu hana hisia na wewe bado unakomaaa kubeba mchanga kwenda nao beach https://jamii.app/JFUserGuide u [emoji19]
 
Kwa hili nalo unasubiri ushauri kijana? Ama kweli mapenzi ni upofu.
 
Back
Top Bottom