Aliyeamua kuchukua hii Route ya Johannesburg to Dar Es Salaam ni Mtanzania Kweli?

Safi sana,

Hivi zile Falcon sijui ziliishiaga wapi?
 
Hakuna Route ya Zambia,Malawi harafu utokee Tunduma...Route za SA ni SA,Zimbabwe mnapita msumbiji Tete harafu Malawi Desza au Mwanza Border unakuja kutokea Songwe border nyingine ni Zimbabwe,Zambia chirundu au Livingstone au Kariba dam harafu Lusaka,Mpika Chinsali unakuja kutokea Tunduma...nyingine ukitaka utokee Sumbawanga unapita mpika unakata kushoto kuelekea Kasama utatokea Ziwani kidogo harafu Sumbawanga hapo sijaitaja ya Msumbiji kwa kuwa bus au magari mengi hayapiti huko kutokea Ruvuma na hii ingine ni ndefu bus huwa zinatumia kutoka Zambia kwenda SA kupitia Botswana harafu SA hii wanapita Kazungura border na ndio bara bara wanayotumia magari madogo na makubwa kutoka SA kuja Tanzania haina usumbufu ila ni kipande cha 1100 Km kutoka border to border...
 
Nilitaka nikuta-tag mkuu kwa sababu najua wewe hizi route una uzoefu nazo.
 
hapo msumbiji hapo msipokuwa makini mnachinjwa shingo na alshabab.. kama inapita msumbiji sishauri tumieni ndege tu..
 
Tulienda mwaka jana mwanzoni, Enzi za Covid-19 mipakaninkulikuwa na complications sana

Dar-Tunduma,
Nakonde-Kapiri,
Kapiri-Lusaka,
Lusaka-Livingstone
Livingstone-Kazungura(Zambia)
Kazungur(Botswana)-Palapye
Palapye-Gaborone
Gaborone-Joz

Ni safari ndefu sana,back route ilibidi tuingie kwa mwewe tuu.
 
Duuuh noma sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…