Toxic Concotion
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 5,760
- 20,837
Mwaka 2007 nilienda na bus za Falcon Harare. Kuna mdada alikuja kusindikizwa na mumewe na vilio tele kuwa watamisiana.Ukikaa na mdada mpaka mfike mshaoana
Alikaa siti ya mbele kabisa ukiingia mlangoni. Nilikuwa namsikia conductor anamtongoza dada. Dada alikuwa anakaza kusema ni mke wa mtu.
Kufika Tunduma kila mtu alikuwa anatafuta ustaarabu wake wa kulala kuanza safari asubuhi.
Baadhi ikiwemo conductor na yule dada tulienda kuchukua vyumba lodge.
Kulipombazuka mke wa mtu alitokea chumbani kwa conductor kuashiria walilala wote. Na baada ya hapo mpaka tunafika Harare walikuwa kama wapenzi wa kitambo.