Aliyekutwa na Fuvu, Sehemu za Siri 5 za Binadamu afutiwa kesi

Aliyekutwa na Fuvu, Sehemu za Siri 5 za Binadamu afutiwa kesi

Kwa maana hiyo kukutwa na viungo vya binadam sio kosa kisheria?
Mtu anaweza kataa tu akasema yeye hajui kama fuvu ni la binadamu.

Kesi kama hiyo mtu anaikataa tu,kazi inabaki kwenu mnaoshkia bango kumuaminisha HAKIMU kuwa mwamba ana HATIA,otherwise hakimu anamtema!
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemfutia kesi na kumwachia huru mshtakiwa Salum Nkonja (23) maarufu kama Emmanuel Nkonja, aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka 11 yakiwemo ya kukutwa na vipande viwili vya mafuvu ya kichwa cha binadamu pamoja na sehemu za siri tano za mwanamke baada ya kesi hiyo kuahirishwa kwa zaidi ya mara tano bila kuendelea na ushahidi.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu, April 17, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Ramadhani Rugemalira wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 32/2022 ilipoitwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.

Mbali na kumfutia mashtaka na kumwachia huru, mshtakiwa hiyo, Mahakama hiyo imeamuru mshtakiwa asikamatwe mpaka upande wa mashtaka watakapowasilisha vielelezo mahakamani.

MWANANCHI
utakuta MAJAMBAZI YALIYOAJIRIWA[emoji61]yalimbambikia raia mwaminifu {Salum Mkonja} ili wamtoe mtu wao
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemfutia kesi na kumwachia huru mshtakiwa Salum Nkonja (23) maarufu kama Emmanuel Nkonja, aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka 11 yakiwemo ya kukutwa na vipande viwili vya mafuvu ya kichwa cha binadamu pamoja na sehemu za siri tano za mwanamke baada ya kesi hiyo kuahirishwa kwa zaidi ya mara tano bila kuendelea na ushahidi.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu, April 17, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Ramadhani Rugemalira wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 32/2022 ilipoitwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.

Mbali na kumfutia mashtaka na kumwachia huru, mshtakiwa hiyo, Mahakama hiyo imeamuru mshtakiwa asikamatwe mpaka upande wa mashtaka watakapowasilisha vielelezo mahakamani.

MWANANCHI
Kasome sheria kwanza utaelewa kwanini kesi imefutwa. Sheria ni sayansi ina kanuni zake, usipozifuata hata km una haki hutaipata. Ndio maana mnaambiwa mtafuteni sana elimu angalia msimwache akaenda zake.
 
Mtu anaweza kataa tu akasema yeye hajui kama fuvu ni la binadamu.

Kesi kama hiyo mtu anaikataa tu,kazi inabaki kwenu mnaoshkia bango kumuaminisha HAKIMU kuwa mwamba ana HATIA,otherwise hakimu anamtema!
Mbona rahis sana, wanaodakwa na Nyara za serikali mbona mambo inamalizika kwa mvua? Nakwambia tena hawa watu hawastahil kuish na binadam..
 
Sikiliza kesi hii ukiwa na Milion 20 imeisha

mil 5 polisi (dpp)
mil 5 HAKIMu

10 hizi za mawasiliano na upande wa wakili upande wa pili
 
Someni maelezo vizuri. Upande wa Mashitaka haukuwa na Vielelezo. Na ndiyo maana Mahakama imesema asikamatwe mpaka upande wa Mashitaka uwe na VIELELEZO na uviwasilishe kwanza Mahakamani!!
 
Kwa maana hiyo kukutwa na viungo vya binadam sio kosa kisheria?
Mahakama haitoi hukumu kwa kusikia. Hata ukienda na kichwa cha mtu hiki hapa kinatoa damu, hakimu hasemi ni kichwa cha mtu. Daktari mwenye taaluma yake ndio aseme kile ni kitu gani. Sasa hakimu kashasema mpaka wapeleke vielelezo ambavyo ina maana hawajapeleka, kwahiyo hakimu hajui vile vinavyosemekana ni viungo vya mtu na fuvu ni vitu gani
 
Hakuna cha ndumba wala nn huyu dogo napajua hadi kwao kijijini kwetu Mwamitumai nimemaliza f4 2012 nikamuacha f1 kwao hawana kitu kwanza Baba yake alifariki kwa pressure baada ya dogo kukamatwa na hakuna hata mmoja aliyekuwa anamshughulikia atoke bahati tu imemuangukia
Hakuna kitu kinachoitwa bahati. Always you let things happen. Lazima Kuna kitu, suala la ndumba linaweza kuwa limechukua nafasi kubwa, kwanza kushughulika na biashara hiyo siyo kitu Cha kawaida Kwa akili hizi na bila ndumba.
 
ukienda makaburini usiku ukachimba maiti bado mbichi imezikwa jana haupati, msiangalie upande wa kuua tu hata wewe ukienda makaburini kwa waliozikwa jana, juzi unavupata

Nakuelewa BOFREE
Makubari mengine vimezikwa vitu na sio miili ya watu japo wazikaji wanaona wamezika mtu
 
Hakuna cha ndumba wala nn huyu dogo napajua hadi kwao kijijini kwetu Mwamitumai nimemaliza f4 2012 nikamuacha f1 kwao hawana kitu kwanza Baba yake alifariki kwa pressure baada ya dogo kukamatwa na hakuna hata mmoja aliyekuwa anamshughulikia atoke bahati tu imemuangukia
Asee..
Kumbe unamjua. Hayo mafuvu na mbususu za watu huwa anatumia kwa kazi gani?!
 
Toa Ushahidi kuwa fuvu ni la binadamu? Thibitisha!

Toa Ushahidi kiungo cha sehemu ya siri ni cha mwanamke,Thibitisha!

Kuna kesi ukiziangalia ni rahisi ila ukipewa uiendeshe Hata kama wewe ni hakimu Utafuta kesi au kumuachia Huru mshtakiwa.
Kwani mimi ndo nimesema ni viungo vya binadamu au mtoa mada?!!!

Besides, siyo kazi ya hakimu wala mwanasheria kuthibitisha kama hivyo viungo ni vya binadamu ama la. Kwa teknolojia ya sasa, hiyo ni kazi nyepesi tu kwenye maabara za kitaalamu kama Muhimbili, nk. Mahakama inapelekewa ripoti tu.

Kama wataalamu wanaweza kuthibitisha kuwa wameokota fuvu la binadamu aliyeishi zaidi ya miaka milioni moja iliyopita huko Olduvai, nk, watashindwaje leo kutambua uke na fuvu la binadamu?!!!

Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegunduliwa sehemu nyengine yeyote.
 
Mtu anaweza kataa tu akasema yeye hajui kama fuvu ni la binadamu.

Kesi kama hiyo mtu anaikataa tu,kazi inabaki kwenu mnaoshkia bango kumuaminisha HAKIMU kuwa mwamba ana HATIA,otherwise hakimu anamtema!
Sivyo..

Yaani ukutwe na viungo vya mtu halafu ulete stori kuwa hujui?!!!

Wanaokamatwa na vitu kama meno ya tembo wasingekuwa wanafungwa basi, wangesema hawayajui tu!

Kisheria, kutojua siyo utetezi.

In law, ignorantia juris non excusat, (or ignorantia legis neminem excusat), is a legal principle holding that a person who is unaware of a law may not escape liability for violating that law merely by being unaware of its content.
 
Duuh🙄
Hapo ni either kazi ya mpunga au ndumba..
Anaachiwa huru kivipi kama vielelezo ambavyo ni viungo vya binadamu vipo?!!!
Wana hakika hatoenda kuvuna vingine?!
Sasa vingekuwepo mahakama ingesema mpaka ushahidi uje?
 
Duuh[emoji849]
Hapo ni either kazi ya mpunga au ndumba..
Anaachiwa huru kivipi kama vielelezo ambavyo ni viungo vya binadamu vipo?!!!
Wana hakika hatoenda kuvuna vingine?!
Sasa umenishtaki, huleti ushahidi mahakamani unatarajia nini
 
Apo ndipo wananchi wanajichukulia sheria mkononi
Mfano tumekamatwa mwizi, tumempeleka polisi then kesi ikaenda mahakamani, sasa tunaambiwa tukatoe ushahidi tunakula Kona, Kuna ile tabia tunasema sitaki kua shahidi hapo unatarajia hakimu afanye nini
 
Babu ni Tanzania tuu.

Utaambiwa, Ushahidi haujitoshelezi.

Kama J4 alipiga watu Risasi na baadae ameachiwa.

Sembuse Hilo ??

Tanzania hamna kinachoshindikana, tena Kwa aina ya utawala kama huu
Acheni kulalamika mambo ya kisheria Yana taratibu zake vipi kama huyo mtuhumiwa alibambikizwa?
 
watu wengi wanaangalia jamaa lbda aliua mtu kumbe alivitoa tu makaburini kwenye makaburi ya wafu
Lakini upande wa pili nahisi kuna sheria inayo kataza kuzitendea mambo ya ovyo maiti.
Kwa namna yeyote ile asingehukumiwa kesi ya mauaji, uhuju uchumi basi angehukumiwa kwa makosa ya kuidhalilisha au kuitendea ndivyo sivyo maiti.
Hakupaswa kuachiwa huru kama amekutwa na viungo hivyo kinyume cha sheria,
 
Back
Top Bottom