Aliyekutwa na Fuvu, Sehemu za Siri 5 za Binadamu afutiwa kesi

Aliyekutwa na Fuvu, Sehemu za Siri 5 za Binadamu afutiwa kesi

Alafu

Alafu kuna watu wanasema uchawi haupo..

We ulisikia wapi kesi ya jinai inakuwa ya uhujumu uchumi ghafla

Mshtakiwa amekutwa na vielelezo vya waziwazi ila anaachiwa kwa kukosekana ushahidi.
Kuna Chali yangu aliombwa amwangalizie mtu begi huyo mtu akaingia sokoni, baada ya muda chalii kadakwa begi kupekuliwa limejaa bangi em jiulize tusingesimama kidede na kua tayari kwenda kutoa ushahidi mahakamani si angepotezwa?
 
Kwani mimi ndo nimesema ni viungo vya binadamu au mtoa mada?!!!

Besides, siyo kazi ya hakimu wala mwanasheria kuthibitisha kama hivyo viungo ni vya binadamu ama la. Kwa teknolojia ya sasa, hiyo ni kazi nyepesi tu kwenye maabara za kitaalamu kama Muhimbili, nk. Mahakama inapelekewa ripoti tu.

Kama wataalamu wanaweza kuthibitisha kuwa wameokota fuvu la binadamu aliyeishi zaidi ya miaka milioni moja iliyopita huko Olduvai, nk, watashindwaje leo kutambua uke na fuvu la binadamu?!!!

Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegunduliwa sehemu nyengine yeyote.
Si ndio hakimu kawaambia upande wa mashtaka wapeleke hivyo vielelezo ambavyo hawakupeleka au nimesoma vibaya
 
Sivyo..

Yaani ukutwe na viungo vya mtu halafu ulete stori kuwa hujui?!!!

Wanaokamatwa na vitu kama meno ya tembo wasingekuwa wanafungwa basi, wangesema hawayajui tu!

Kisheria, kutojua siyo utetezi.

In law, ignorantia juris non excusat, (or ignorantia legis neminem excusat), is a legal principle holding that a person who is unaware of a law may not escape liability for violating that law merely by being unaware of its content.
Sema kwenye kesi Kuna mambo mengi sana naweza kukuambia nithibitishie kwamba hili ni fuvu la kichwa Cha binadamu ukashindwa kunithibitishia
 
Sema kwenye kesi Kuna mambo mengi sana naweza kukuambia nithibitishie kwamba hili ni fuvu la kichwa Cha binadamu ukashindwa kunithibitishia
Uthibitishiwe kivipi, hapo kinachotakiwa ni kuwasilisha mahakamani autopsy au
post-mortem report ya hivyo vitu.

Usisahau kwamba hao wapelelezI na waendesha mashtaka Kwa makusudi tu wanaweza kuacha kupeleka vielelezo muhimu kama hizo ripoti ikiwa rushwa imehusika
 
Huenda imethibitishwa hivyo viungo sio vya binadamu na si vingenevyo. La sivyo ingetakiwa abinywe korodani mpaka awataje na wenzake.
 
Duuh[emoji849]
Hapo ni either kazi ya mpunga au ndumba..
Anaachiwa huru kivipi kama vielelezo ambavyo ni viungo vya binadamu vipo?!!!
Wana hakika hatoenda kuvuna vingine?!
Unataka sema hujasoma habari na kuielewa?
 
sishabikii kuwa na viungo vya binadamu lkn mitazamo yenu si sahihi wapi jamaa kaonekana aliua, viungo vya binadamu ukienda makaburini kwenye makaburi ya watu waliozikwa jana, juzi unapata viungo vyote unavyotaka vikiwa vibichi

Mtu akifariki unaruhusiwa kumtoa viungo kiholela makaburini?

Huu ujinga ulisomea wapi?
 
Hilo litakuwa amecheza na watunza mochwary siyo jmbo jepesi kupata viungo vya binadamu itakuwa kawaonga watunza maiti
 
sishabikii kuwa na viungo vya binadamu lkn mitazamo yenu si sahihi wapi jamaa kaonekana aliua, viungo vya binadamu ukienda makaburini kwenye makaburi ya watu waliozikwa jana, juzi unapata viungo vyote unavyotaka vikiwa vibichi
Je hilo unalosema wwe la kwenda makaburini na kuchukua viungo vya wafuu si kosa kisheria!!??
 
Sikiliza kesi hii ukiwa na Milion 20 imeisha

mil 5 polisi (dpp)
mil 5 HAKIMu


10 hizi za mawasiliano na upande wa wakili upande wa pili
DCI na DPP ndiyo wagawane hiyo M5!? Mbona hiyo pesa ni ndogo sana, watu wanafanya plea bargain ya over Biliones kwa DPP na bado wengine anawapiga chini na pesa zao!!
 
Mahakama haitoi hukumu kwa kusikia. Hata ukienda na kichwa cha mtu hiki hapa kinatoa damu, hakimu hasemi ni kichwa cha mtu. Daktari mwenye taaluma yake ndio aseme kile ni kitu gani. Sasa hakimu kashasema mpaka wapeleke vielelezo ambavyo ina maana hawajapeleka, kwahiyo hakimu hajui vile vinavyosemekana ni viungo vya mtu na fuvu ni vitu gani
Kwa hiyo unataka kusema police wamepeleka viungo Mahakamani lakini wameshindwa kupeleka report ya Dr aliyethibitisha kua kweli hivyo ni viungo vya Binaadamu!!?? Na ndiyo maana Hakimu akaitupa kesi nje!!?
 
Back
Top Bottom