TANZIA Aliyekuwa Askofu Mkuu wa TAG, Prof. Rainwell Mwenesongole wa Upanga CCC ametwaliwa na Bwana!

TANZIA Aliyekuwa Askofu Mkuu wa TAG, Prof. Rainwell Mwenesongole wa Upanga CCC ametwaliwa na Bwana!

Hawa maaskofu hawanaga faida, wapiga dili tu sikuwahi kumsikia akihubiri haki
Huu ujinga kabisa kanisani sio sehemu ya kuhubiri siasa kiufupi yapo kambo mengi ambayo bado hayajafundishwa kanisani siasa wapatieni maaskofu wanasiasa
 
Neno hayati linatumiwa kwa wanajeshi na amir jeshi mkuu na wasaidizi wake wawili yaani makamu na waziri mkuu.

Wengine wote ni marehemu kwa heshima zao hapa duniani
Ufafanuzi huu ni wako au wakiswahili?
 
Neno hayati linatumiwa kwa wanajeshi na amir jeshi mkuu na wasaidizi wake wawili yaani makamu na waziri mkuu.

Wengine wote ni marehemu kwa heshima zao hapa duniani
Huu sasa ni upotoshaji. Maneno haya asili yake ni ya kiaarabu. Hayati kwa kiaarabu inamaanisha enzi za uhai wake. Linatumika unapokumbuka au kuogelea mambo/matendo mema ya enzi za uhai wake.

Marehemu linatokana na neno la kiaarabu la rehemu/ rehema au dua. Hivyo linatumika unapomwombea dua kwa Mwenyezi Mungu amurehemu aka RIP.
 
اِنَّ الَّذِيۡنَ كَفَرُوۡا وَمَاتُوۡا وَهُمۡ كُفَّارٌ اُولٰٓٮِٕكَ عَلَيۡهِمۡ لَعۡنَةُ اللّٰهِ وَالۡمَلٰٓٮِٕكَةِ وَالنَّاسِ اَجۡمَعِيۡنَۙ‏

Hakika walio kufuru na wakafa hali ni makafiri, hao iko juu yao laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote.

خٰلِدِيۡنَ فِيۡهَا ۚ لَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمُ الۡعَذَابُ وَلَا هُمۡ يُنۡظَرُوۡنَ

Watadumu humo. Hawata-punguziwa adhabu wala hawatapewa muda wa kupumzika.
 
Huyu alikuwa ameshastaafu ukuu wa TAG miaka mingi nyuma. Zaidi ya miaka 10 iliyopita, kuna Askofu Mkuu mwingine na si huyu aliyetwaliwa na Bwana. Tuzo aliyopewa Hayati JPM, ilikuwa ni baada ya kupambana vizuri sana na janga la Corona awamu ya kwanza. Haya mengine uliyoyasema humu unaweza kuyathibitisha, just in case?
Kakurupuka kwa ubinasi wake.
Rip Prof Mwenisongole
 
Nafahamu kuwa alishastaafu hicho cheo cha uaskofu mkuu wa TAG, lakini hakuwahi kustaafu cheo cha uaskofu na wala hakuwahi kuacha kazi yake ya kuhubiri au kulisemea kanisa lake la TAG pale City Christian Centre. Hivyo maovu yaliyofanyika nchi hii na yeye akiwa anayaona lakini akaogopa na kukaa kimya yanamhusu kwa 100%.

Swali kuu, kwa miaka mitano ya utawala wa ukandamizaji wa Magufuli, yeye alikuwa anasema nini?
Ule uchafu uliokuwa unafanywa na wapontekoste wenzake (TAG ikiwa ni kinara) wa kumsifia na kumpamba Magufuli, yeye aliweza kuchukua hatua gani?

Ule ubunge wa wizi ambao mtoto wake alizawadiwa na CCM kule Songwe ilikuwaje akaubariki?
Watumishi wa Mungu wanautendaji wao wa kazi sio lazima wewe Zanziba asp uyaone kwa macho yako ya kuangalia ugali.Rip Mchungaji kiongozi.
 
RIP askofu.
Huyu ni miongoni mwa maaskofu wa kipentekoste aliyekuwa muadilifu sana katika masuala ya imani.
Kanisani kwake upanga miaka hiyo ya 1991 ndipo palipokuwa na ibaada mbili kwa jumapili yaani ya kiingerza na ya kiswahili.
Wengi wa maofisa wa balozi nyingi nchini waliokuwa walokole walisali kanisani kwake.
Poleni wafiwa.
 
Acha upumbafu wewe..manabii na mitume walikemea wazi wazi watawala wabovu na wala hawakuogopa..unadhani kichwa cha yohana mbatizaji kilikatwa kwasababu gani?.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Enzi zile kiongozi wa dini ndie alikuwa anachagua Nani awe mfalme alikuwa juu ya wafalme sababu ndie aliwaweka madarakani

Yohana mbatizaji alijitia kumkemea Herode ambaye hakumuweka madarakani Herode alamshangaa huyu Yohana ananikemea kama Nani akamkata kichwa Akamuua

Usilinganishe wa zamani na wa sasa
 
Usihangaike naye huyo halijui Kanisa Katoliki kwa hoja zake wote waliopo kazini walikuwa majobles Kanisa Katoliki huanza kuandaa mapadri tangu kidato cha kwanza kwenye shule zao zinazoitwa seminari ndogo wapo wachache sana wanaopata wito wa upadri ambao hawakupitia seminari ndogo lakini lazima wapitie seminari kusomea falsafa na teolojia upadri haupatikani kwa kujitangaza mwenyewe
Sawa Katoliki huandaa wakiwa wadogo kuwa mapadre issue ni kuwa huwachukua vijana wadogo jobless kuwaanda a kuwa mapdre wenye job ya upadri
 
Pamoja na mambo yote aliyowahi kuyafanya, huyu Askofu hakuwa muadilifu kwa jamii kwa kipindi chote cha utawala wa Magufuli.

Huyu Askofu, yeye binafsi na kanisa lake la TAG waligeuka kuwa waongo na wanafiki ili kujipendekeza kwa Magufuli. Hawa maaskofu wa TAG na wapentekoste wengine ndio walifikia hatua ya juu ya unafiki ya kumuita na kumpa tuzo ya uadilifu Magufuli!

Wakati watanzania wakiuwawa, wakiteswa, kudhulumiwa na kufanyiwa kila ubaya na utawala wa Magufuli, huyu askofu na wenzake walikuwa kimya au kumimina pongezi kwa Magufuli.

Kwangu binafsi ninapenda kusema huyu Marehemu hakuwa tena na mchango wowote kwa jamii ya watanzania labda kwa dini yake.

Ninatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu, lakini ninasikitika kusema hapa kuwa, Marehemu hakuwa tena na faida yoyote kwetu kijamii, na bora amepumzika.
Wakati wa JPM huyu hakuwa askofu mkuu wa TAG.
 
Manzi wangu aliwahi nishawishi niwe nahudhuria 1st Sunday service, yaan ibada ya kwanza JP kwa kimombo, ee bhanae nilienjoy sana praise n worship session kuna vijana wanaimba vizuri mnoo asikwambie mtu.U guys brought me close to God through music. Niliacha kuhudhuria baada ya kuhamia mikoani. RIP Bishop Mwenisongore
 
Katoliki huajiri jobless wanamchukua kijana jobless wanamsomesha upadri halafu wanampa kazi ya upadri

Wako kibao wanasoma seminary za Katoliki majobless

Mapadri wengi unaowaona walkuwa majobless ajira yao ya kwanza ni upadri
Hujui unachokieleza. Waachie wanaojua wakwambie
 
Watumishi wa Mungu wanautendaji wao wa kazi sio lazima wewe Zanziba asp uyaone kwa macho yako ya kuangalia ugali.Rip Mchungaji kiongozi.
Acha uzembe ndugu yangu.
Mtumishi wa Mungu ni binadamu wa kawaida kabisa, anaishi na wanadamu, na amejaa udhaifu mwingi kama walivyo binadamu wengine, hana kitu kingine cha ziada kuliko mwanadamu mwingine yoyote, lakini amepewa nafasi ya kuwatumikia watu chini ya utaratibu wa Mungu.

Kama kuna mambo mtumishi wa Mungu anayafanya sirini basi hayo atajuana na Mungu wake lakini yale anayoyafanya hadharani ni mambo yetu na tuna haki ya kuyapima na kuyahukumu. Hiyo ni kazi yetu sisi wanadamu.

Biblia inasema, watumishi halisi wa Mungu tutawapima (tutawahukumu) kwa matunda (matendo) yao. Hivyo sisi hapa tunayo haki kwa 100% kumhukumu Askofu Mwanisongole kwa matendo yake. Kwenye suala la kutetea haki za watanzania waliokuwa wanaonewa vikali na serikali ya Magufuli, bila shaka Askofu Mwanisongole aliamua kukaa kimya au kuungana na watawala kwa kuwapongeza. Askofu Mwanisongole hawezi kulikwepa hili, na huko aliko litamfuata.
 
Ucdhihirishe ubwege wako hadharan,N zuzu tu ambaye anaweza kutofautisha maisha na siasa
Huu ujinga kabisa kanisani sio sehemu ya kuhubiri siasa kiufupi yapo kambo mengi ambayo bado hayajafundishwa kanisani siasa wapatieni maaskofu wanasiasa
 
Ukwel mchungu huu
اِنَّ الَّذِيۡنَ كَفَرُوۡا وَمَاتُوۡا وَهُمۡ كُفَّارٌ اُولٰٓٮِٕكَ عَلَيۡهِمۡ لَعۡنَةُ اللّٰهِ وَالۡمَلٰٓٮِٕكَةِ وَالنَّاسِ اَجۡمَعِيۡنَۙ‏

Hakika walio kufuru na wakafa hali ni makafiri, hao iko juu yao laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote.

خٰلِدِيۡنَ فِيۡهَا ۚ لَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمُ الۡعَذَابُ وَلَا هُمۡ يُنۡظَرُوۡنَ

Watadumu humo. Hawata-punguziwa adhabu wala hawatapewa muda wa kupumzika.
 
Acha uzembe ndugu yangu.
Mtumishi wa Mungu ni binadamu wa kawaida kabisa, anaishi na wanadamu, na amejaa udhaifu mwingi kama walivyo binadamu wengine, hana kitu kingine cha ziada kuliko mwanadamu mwingine yoyote, lakini amepewa nafasi ya kuwatumikia watu chini ya utaratibu wa Mungu.

Kama kuna mambo mtumishi wa Mungu anayafanya sirini basi hayo atajuana na Mungu wake lakini yale anayoyafanya hadharani ni mambo yetu na tuna haki ya kuyapima na kuyahukumu. Hiyo ni kazi yetu sisi wanadamu.

Biblia inasema, watumishi halisi wa Mungu tutawapima (tutawahukumu) kwa matunda (matendo) yao. Hivyo sisi hapa tunayo haki kwa 100% kumhukumu Askofu Mwanisongole kwa matendo yake. Kwenye suala la kutetea haki za watanzania waliokuwa wanaonewa vikali na serikali ya Magufuli, bila shaka Askofu Mwanisongole aliamua kukaa kimya au kuungana na watawala kwa kuwapongeza. Askofu Mwanisongole hawezi kulikwepa hili, na huko aliko litamfuata.
Unamuhukumu akiwa hana. Uwezo wa kujitetea? Kama hukuweza kusema muda wote nyamaza mzee apumzike imetosha , maneno makalimakali kama mtu mwenye njaa si viziri , watumishi wa Mungu ni wa kiroho zaidi na kama wewe si wa kiroho ndio maana unapima kwa macho yako ya kutafutia ugali , ndio maana unamgombeza hata marehemu.
 
Back
Top Bottom