TANZIA Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar, Willson Kabwe afariki dunia

TANZIA Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar, Willson Kabwe afariki dunia

Status
Not open for further replies.
Sio kweli kuwa marehemu aliugua kutokana na shock... Kwa Maelezo yake mwenyewe ni kuwa tangu mwaka jana afya yake haiko sawa na alishaandika barua ya kuomba kustaafu kwa sababu za kiafya.
Tuondoe upotoshaji...
mkuu kwa jinsi ulivyoandika ni kama marehemu amekanusha habari wakati tayari ameshafariki.
 
maweeeeeee mbona kaondoka mapema hivyo hata hajajibu mashtaka ya ile mikataba aliyosaini??i
Hajajibu mashtaka yapi? Maneno ya Makonda ndio criminal charge sheet?

Tujifunze kuwapa watu due process of law. Ungempeleka akajitetee angeweza labda kukupa majina makubwa zaidi. RAS is a lightweight kwenye utawala na maamuzi ya jiji. Rais kashtukizwa hadharani na maneno ya Makonda akataka kufurahisha umati kwa kum fire RAS. Mbona kamuacha RC Sadick, alikuwa wapi wakati hii mikataba inapitishwa? Kwa nini AG nae hakuihakiki? Pesa iliyoingiwa mkataba ilikuwa north of the threshold which triggers Attorney General mandatory review. Inakuaje mtu mmoja ajiamulie peke yake kuingia mkataba wa mabilioni bila kufuata sheria? Haiwezekani. Basi angeweza kuuza Uwanja wa Taifa peke yake. Your problem here is bigger than just one individual.
 
Asee hivi we jamaa umeambiwa Mkurugenzi wa jiji kwa kiingereza ndo RAS au? Acha kuchanganya habari aisee.
 
RC Makonda alisema hawezi kufanya kazi na Mr Kabwe, itashangaza wengi endapo ataudhuria msibani. Kwani utampendaje mtu baada ya kufariki? Huo utakuwa unafiki mkubwa sana.
 
Makonda alimuomba magu amuondolee huyo MTU kwakuwa hawezi kufanya naye kazi Magu naye akatii agizo la Dogo HV wataenda kwenye msiba wake kweli?
 
RC Makonda alisema hawezi kufanya kazi na Mr Kabwe, itashangaza wengi endapo ataudhuria msibani. Kwani utampendaje mtu baada ya kufariki? Huo utakuwa unafiki mkubwa sana.

Ninaomba tuache habari za uchochezi. Huyu mzee baada ya tangazo la kufukuzwa kazi, iliwekwa bayana kwamba alikuwa ameomba kustaafu kwa ajili ya afya yake. Iweje leo tusingizie watu wameua ikiwa likuwa dhaifu kwa muda mrefu kiasi hata cha kushindwa kufanya kazi?

Ni vyema tukamheshimu Mungu jamani.
Halafu pia, mtu akifanya makosa akaumiza watu au kuharibu hatima zao makusudi kwa jinsi isiyohalali, makosa hayo hayafutwi na kifo kwa sababu kufa kwake hakubadilishi automatically maumivu ya watu aliowatesa na wengine kuwapotezea maisha. Ndiyo sababu Biblia inasema kufa ni mara moja na baada ya kufa ni hukumu. Hakuna toba wala nini baada ya kufa bali matendo ya kila mtu yanamfuata.

Lakini huyu mzee wetu hajawahi kufanya jema lolote katika maisha yake? Katika kipindi hiki, ninaomba turejee ubindamu wote. Tujengemsiba wake katika heshima ya mazishi bora. Kwamba tuache kulaumiana kwa ushabiki wa kukomoana, lakini pia tutafakari kama kuna jema lolote alilowahi kutenda huyu ndugu, na hilo ndilo tulitaje. Ni binadamu huyu.

Maisha yake baada ya hapa sasa yanakuwa chini ya Hukumu ya Mungu kwa ajili ya roho yake, na sheria za nchi kwa ajili ya matumizi ya mamlaka aliyokuwa nayo.

Ninashukuru kwa walionielewa.
 
wilson%2Bkabwe.JPG

Inadaiwa amefariki dunia akiwa nchini India alikokuwa kwa matibabu.

Aidha, inasemekana tangu siku ile wamtumbue jipu ktk Daraja la Kigamboni (Nyerere Bridge) alikuwa shocked sana alikuwa kalazwa India akipatiwa matibabu.

=====
UPDATE: Naithibitisha taarifa hii

RIP Bw. W. Kabwe, Poleni Wafiwa.
 
Labda jamaa alijua mapema akaamua kubalance stori kwa kumtumbua mzee wa Lugumi Kitwanga ili asubuhi watu wahamishe stori toka msiba na madhara ya utumbuaji hadharani kwenda kwa Kitwanga....
 
Labda jamaa alijua mapema akaamua kubalance stori kwa kumtumbua mzee wa Lugumi Kitwanga ili asubuhi watu wahamishe stori toka msiba na madhara ya utumbuaji hadharani kwenda kwa Kitwanga....
Mkuu mbona umeniibia wazo aseee, so itabd ipi iwe hot hapo maana zote za moto si unajua tunaendeshwa na matukio
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom