Pre GE2025 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM

Pre GE2025 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mch. Peter Msigwa katimkia CCM kutoka CHADEMA.
Rai yangu ni kwamba, pande zote mbili zijizuie kurushiana maneno au kulaumiana.
Yaani, Msigwa ajizuie kulaumu chama alichotoka na wafuasi wa CHADEMA wajizuie kumlaumu Msigwa.

Sumaye na Lowassa walikuwa mawaziri wakuu wastaafu lakini walihama CCM wakahamia CHADEMA na maisha yakaendelea. Kwa hiyo mimi sioni kama kuna la pekee sana linalohitaji kulaumiana kati ya hizi pande mbili.
Chadema yote ilijua Msigwa atahamia ccm, wamlaumu kwa lipi?
 
Kakaa nje ya Bunge msimu mmoja tu, njaa ikahamia kichwani ubongo ukaenda tumboni. Sijui kapewa ngapi, maana Boni yai aliwahi kusema hata yeye alifuatwa na kupigiwa simu sana na Magufuli na mamilioni akakataa, huyu kaisha hawezi kugombea hata udiwani.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila Wanasiasa wa Bongo, woiiiiiih
Hatariiii tupuu
 
Naanza kuwaelewa ambao huwa wanakataa kwenda kupiga kura , kumbe huwa wako sahihi . Siasa ni ujinga ujinga tu .
 
Mkuu, nilikuwa namuunga Msigwa mkono hadi hii leo. Hapa naunga mkono yeye kuukosa ule uwenyekiti dhidi ya Sugu, kukosa nafasi ya uongozi sio sababu ya kukihama chama.
Ameniacha na tafakuri, lakini zaidi ni mtu asiyefaa.
Anaamini hakutendewa HAKI.

Yeye alisema mapema

Lissu alisema pia
 
Kama Naibu Katibu Mkuu Chadema bara anasema eti mke wake wa ndoa (one of COVID-19) hakumshirikisha suala la kwenda kuapishwa na Ndugai gereji bungeni [emoji1]

Lakini posho za mkewe anakula
 
Shalom,

Ya Mungu mengi ila ya binadamu nayo si haba ndivyo unaweza sema kama nakshi ya kituko cha mchungaji Msigwa kuhamia CCM.
Akihojiwa huku akiwa na kihotuba chake, na papo hapo anaweweseka hawezi kusoma na kutamka vizuri maneno aliyoyandaa mwenyewe ni ishara ya mkurupuko na mfadhaiko wa kitoto na kishamba.
Mch. Msigwa lugha yake ya mwili na matamshi ni ishara ya mkurupuko and a failed calculation.

Pole sana ndugu Peter Msigwa kuchagua pia ni matokeo.

Ni hayo tu

Wadiz nipo. Kanyabayonga
 
Ktk dunia hii baada ya mwanamke mwengine wa kuogopwa ni mwanasiasa.

Huwa nawaona wanavyoongea mpaka mishipa ya shingo kuwatoka kwa kigezo wanamtetea mwananchi maskini lakini ukweli ni kwamba huwa wanapambania matumbo yao na familia zao.
 
Mkuu muache Mchungaji Msigwa aishi maisha yake. Wewe baki na maisha yako,amini katika chama unachoamini. Wapo wengine wengi wataondoka Chadema,huyu sio wa mwisho. Endeleeni kujifunza mnakosea wapi na nini mfanye kunasuka hapo mlipo sababu kiukuaji mnarudi kinyumenyume.
 
Kuna namna Msigwa hata yeye mwenyewe anajishangaa, ni kama haamini vile.
Amepoteza credibility yake kirahisi na kwa haraka sana.
Msigwa anaenda kupata teuzi,mshahara mnono,mamlaka na mengi ambayo kamwe asingepata huko Chadema. Kitila mkumbo anajuta? Joshua Nasari anajuta? Kafulila anajuta? Msigwa anaenda kuungana na hao kula keki ya taifa.
 
Mkuu muache Mchungaji Msigwa aishi maisha yake. Wewe baki na maisha yako,amini katika chama unachoamini. Wapo wengine wengi wataondoka Chadema,huyu sio wa mwisho. Endeleeni kujifunza mnakosea wapi na nini mfanye kunasuka hapo mlipo sababu kiukuaji mnarudi kinyumenyume.
Ukweli mchungu
 
Hahahaa kwahio Chadema mdundiko au sio ye baba.🏂🏂🏂
 
Kuna namna Msigwa hata yeye mwenyewe anajishangaa, ni kama haamini vile.
Amepoteza credibility yake kirahisi na kwa haraka sana.
Mimi sio shabiki wa haya mambo ya kisiasa,ila huyu jamaa inaonekana kabisa kua amechukua maamuzi kwa hasira aliyokua nayo,

Anyway hiyo ndio demokrasia,all the best for him.
 
Back
Top Bottom