Aliyemshauri Mbowe agombee alidhamiria kumdhalilisha na kukiua Chama

Aliyemshauri Mbowe agombee alidhamiria kumdhalilisha na kukiua Chama

Mtu imara anapimwa kwenye vigezo gani? Kwa hapa taasisi ilipofikia unafikiri ilikosa uongozi imara. Taasisi imara ni ile yenye collective responsibility kwa uongozi mzima na sio kiongozi.
Ndio maana kuna kamati tendaji ambayo ndio inafanya maamuzi ya kiutendaji. Otherwise tuelezwe kuwa kamati tendaji haina viongozi imara.

Mkuu uimara wa CHADEMA kwa sasa upo wapi?
Kwa zamani inajulikana CHADEMA ilikuwa imara kwenye eneo la kukemea ufisadi, Rushwa na kupigania HAKI za Watanzania ambao wewe unauita uanaharakati.

Hata umaarufu wa CHADEMA ulijikita katika kitengo hicho.
 
Kwani huu ushauri una shida gani!!
20241227_143435.jpg
 
Haki ndio inamfanya mwenyekiti wa sasa kuomba ridhaa tena. Maamuzi yako mikononi mwa wajumbe na si wanaharakati.

Nafikiri hujui Maana ya HAKI.

Kama umkristo kasome Kisa cha Mfalme Sauli Vs Daudi utaelewa kipi ambacho kinaendelea kwa watu wenye Akili na HEKIMA.

Katiba inaweza kukupa Haki ya kugombea kitu Fulani lakini mazingira na wakati vikakunyima haki hiyo
Au Elimu yako ya kukariri unashindwa kuelewa mambo madogo kama hayo?
 
Siasa ni mipango mkuu. Binafsi naamini kuna mipango. Kwa historia yao Bado siamini FAM na TAL ni maadui kwa kiwango cha kutokukaa chini na kukubaliana kuhusu hii vita.

Mpango unaweza kuwa ni:

1. Mbowe anashindwa, Lissu anashinda, Mbowe anakubali matokeo na kuahidi kutoa ushirikiano.

2. Panatokea mdahalo wa FAM v/s TAL, Lissu anajenga hoja zake vizuri, Mbowe anaitisha Press anaamua kujiengua na sababu ni Lissu kamshawishi kwa hoja.

3. Lissu anashindwa, Mbowe anashinda, Lissu anamuunga mkono Mbowe.
(Kwa maoni yangu hii somehow ni mbaya kwa CHADEMA na nzuri kwa CCM maana baada ya hapo CCM wataanza kuimba wimbo wa mbowe kung'ang'ania madaraka, kupenda pesa za ruzuku, chama cha wachaga n.k)

Kama hivi ni vita visivyo na ushirikiano baina yao, uwezekano ni TAL atachana na chama na sio nzuri kwa CHADEMA.
Unasemaje?
20241227_143435.jpg
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Vijijini ndio hawataki hata kusikia jina lake wanaona kama msaliti yaani chawa wa ccm au political entrepreneur
 
Kumbe Mbowe alikuwa mvurugaji toka kitambo sana. Ni vile tu hatukujua
Mbowe hakuwa mvurugaji ila sasa ndiyo ameamua kuvuruga, Mbowe alijitahidi sana kukijenga hiki chama Ila dakikaa za mwishooo kabisa roho ya usaliti ikamwingia, Shetani anamwingiavmtu mda wowote, Roho ya usaliti ilipo mwingia, akaenza kwenda kinyume na agano aliloliweka na wanaCHADEMA akaona ili, madhambi yake ya usaliti yasije kujulikana lazima amkabidhi kijiti Mtu anaye, mwamini kwahiyo, Akaamua kugombea na mwaka huu na Lisu alivyojua kuwa Mbowe anagombea kipindi hiki tena, naye hakuwa na shida, akatangaza kugombea umakamu, Akashtukia wenje naye Anatangaza kuwania umakamu, Washauri walisu wakamtonya kuwa Huyo ni Mshirika wa Mbowe na mkakati wao nikung'oa umakamu kwasabu Msure kashaonjeshwa asali na Wamekubaliana na Mama yeye agombee Urais ili mama asipate Competition is ya maana kwahiyo wewe livumbulue, Hata ukishindwa huna cha kupoteza. Ndiyo hapo Lisu akaanzisha huu mtanange kutibua deal la watu. Sasa mambo mshike mshike kila kona, mwizii huyo mwizi huyoo, wengine, mchonya asali, mchonya asali mishale kila kona ila yeye anajifanya Nyegere ata ang'atweje, Kwani mchonya asali achonyi mara moja. Pamoja na mishale yote ya nyuki, yeye yumo tu.Pia kulikuwa na minong'ono ya serikali ya Nusu mkate ambayo Baadhi ya viongozi waandamizi wangepata ubenge na uwaziri, Mmm lakini hizi Porojo zangu tu msizitilie Maanani.
 
Kwema Kabisa!

Mbowe itampasa amkumbuke aliyemshauri aendelee kugombea.
Familia yake ilimshauri apumzike, kwa mujibu wa maelezo yake. Ni kwa sababu inampenda na kutaka heshima yake idumu.

Lakini kuna kundi jingine ambalo likamshauri vibaya agombee ili adhalilishwe, heshima yake kushuka, na chama kumfia Mikononi.

Embu fikiria Miaka zaidi ya 30 Mbowe amepigana kufa na kupona kujenga jina na heshima ya brand yake.

Leo hii Mbowe ni wakuitwa Nkurunzinza,
Leo hii Mbowe ni wakuitwa Ayatollah, kweli?

Haya Leo hii Yule Mbowe mwenye jina Kubwa anakuwa kama underground, au underdog kumkabili Lisu mtu aliyemlea Mwenyewe kisiasa? KWELI!

Leo hii Mbowe ni wakushindwa ushawishi kwenye jamii kwa zaidi ya asilimia 80% kila polls zikiitishwa. KWELI?

Heshima iliyojengwa kwa miaka nenda Rudi Leo inavurugika na kupotea kwa Siku chache tuu. Kisa uchaguzi?

Leo hii Mbowe ni wakukataliwa na Robo tatu ya Jamii Forum ambao ni mtandao wa ndani katika nchi yetu. Mtandao unaojitambulisha kama home of Great thinker. KWELI?

Nini kina thamani zaidi ya Heshima? Kitu gani hicho.
Kama ni pesa tayari Mbowe anazo. Nani alimshauri aiweke rehani Heshima yake.

Nani huyo aliyemshauri Mbowe ashindane na Wakati?
Tangu lini mtu akashindana na wakati akashinda zaidi ya kudhalilika na heshima yake kudondoka?

Mfalme Sauli naye heshima yake ilianguka, kwa kushindwa kutambua matumizi ya wakati.
Akawa anapambana na Daudi, kijana mdogo.
Heshima yake yote ikadondoka. Hata Yale mazuri yote aliyoyafanya Sauli Akiwa mfalme yakafutika.

Nawatakia siku njema
Tatzo kura anaweza kupata uchaguzi ukiwa wa kifisi
 
Mbowe hakuwa mvurugaji ila sasa ndiyo ameamua kuvuruga, Mbowe alijitahidi sana kukijenga hiki chama Ila dakikaa za mwishooo kabisa roho ya usaliti ikamwingia, Shetani anamwingiavmtu mda wowote, Roho ya usaliti ilipo mwingia, akaenza kwenda kinyume na agano aliloliweka na wanaCHADEMA akaona ili, madhambi yake ya usaliti yasije kujulikana lazima amkabidhi kijiti Mtu anaye, mwamini kwahiyo, Akaamua kugombea na mwaka huu na Lisu alivyojua kuwa Mbowe anagombea kipindi hiki tena, naye hakuwa na shida, akatangaza kugombea umakamu, Akashtukia wenje naye Anatangaza kuwania umakamu, Washauri walisu wakamtonya kuwa Huyo ni Mshirika wa Mbowe na mkakati wao nikung'oa umakamu kwasabu Msure kashaonjeshwa asali na Wamekubaliana na Mama yeye agombee Urais ili mama asipate Competition is ya maana kwahiyo wewe livumbulue, Hata ukishindwa huna cha kupoteza. Ndiyo hapo Lisu akaanzisha huu mtanange kutibua deal la watu. Sasa mambo mshike mshike kila kona, mwizii huyo mwizi huyoo, wengine, mchonya asali, mchonya asali mishale kila kona ila yeye anajifanya Nyegere ata ang'atweje, Kwani mchonya asali achonyi mara moja. Pamoja na mishale yote ya nyuki, yeye yumo tu.
Aiseee si aweke silaha chini
 
Nafikiri hujui Maana ya HAKI.

Kama umkristo kasome Kisa cha Mfalme Sauli Vs Daudi utaelewa kipi ambacho kinaendelea kwa watu wenye Akili na HEKIMA.

Katiba inaweza kukupa Haki ya kugombea kitu Fulani lakini mazingira na wakati vikakunyima haki hiyo
Au Elimu yako ya kukariri unashindwa kuelewa mambo madogo kama hayo?
Mifano yako ni irrelevant.
Tuwaache wajumbe na wenye chama chao wachague wanayemtaka. Nyie wanaharakati subirini atakayepata kura nyingi mfanye naye kazi.
Nawahakikishia wanaharakati bila vyama vya siasa hamna mtalachofanya, yaani mtakosa kazi za kufanya.
Malema wa Afrika Kusini unaweza kumfananisha na TAL ingawa kuna maeneo wanatofautiana. Sasa angalia Malema ameishia kwenye harakati wakati wenzie wanafanya siasa na kupitia uchaguzi uliopita unaweza kuona matunda ya kila chama.
 
Mbowe angepata fursa ya kutawala Tanzania angekuwa ni Dikteta wa hatari na angemteua Yericko awe ndiye Malyamungu wake wa kushughulikia Critics wake trust me na angefia Ikulu na Jeshi angejaza watu wake ili lisimpindue.

Huenda nikajiunga na ATC wazalendo siku za usoni au nikabaki kwenye Jukwaa la Sauti ya Watanzania.
 
Mbowe angepata fursa ya kutawala Tanzania angekuwa ni Dikteta wa hatari na angemteua Yericko awe ndiye Malyamungu wake wa kushughulikia Critics wake trust me na angefia Ikulu na Jeshi angejaza watu wake ili lisimpindue.

Huenda nikajiunga na ATC wazalendo siku za usoni au nikabaki kwenye Jukwaa la Sauti ya Watanzania.
Mbowe ameonekana vile alivyo
 
Pambaneni mnavyoweza ila mkumbuke anayetaka kuwa mwenyekiti wa CHADEMA lazima agombee na apate kura kuwazidi wengine.

Nilikuwa namkubali Lissu kuliko hata Mbowe, ila baada ya Lissu kuleta tuhuma zisizi na ushahidi nimemwona hafai hata kuwa mjumbe.
 
Pambaneni mnavyoweza ila mkumbuke anayetaka kuwa mwenyekiti wa CHADEMA lazima agombee na apate kura kuwazidi wengine.

Nilikuwa namkubali Lissu kuliko hata Mbowe, ila baada ya Lissu kuleta tuhuma zisizi na ushahidi nimemwona hafai hata kuwa mjumbe.
Wote wamejivua nguo kwa kutanguliza tamaa zao binafsi huku wakikibomoa chama chao, they're all playing dirty games out of greediness.
Kinachomsaidia Lissu ni kuwa na chawa wengi ambao wako very vocal, all in all pomoja na kwamba Lissu fuses nyingi za kichwani kwake zimeungua ndiye anayeweza kuipa kashkash CCM jambo ambalo Mbowe kwa sasa haliwezi.
Yale maneno yake anayotiririkaga na uchambuzi wake wa namna anavyokosoa mikataba ya 'kihuni' itarudisha amsha amsha kwenye upinzani, ila honestly uwezo wa kuongoza institution hana. Yupo sampuli za late Mtikila.
 
Back
Top Bottom