Aliyemshauri Mbowe agombee alidhamiria kumdhalilisha na kukiua Chama


Mkuu uimara wa CHADEMA kwa sasa upo wapi?
Kwa zamani inajulikana CHADEMA ilikuwa imara kwenye eneo la kukemea ufisadi, Rushwa na kupigania HAKI za Watanzania ambao wewe unauita uanaharakati.

Hata umaarufu wa CHADEMA ulijikita katika kitengo hicho.
 
Haki ndio inamfanya mwenyekiti wa sasa kuomba ridhaa tena. Maamuzi yako mikononi mwa wajumbe na si wanaharakati.

Nafikiri hujui Maana ya HAKI.

Kama umkristo kasome Kisa cha Mfalme Sauli Vs Daudi utaelewa kipi ambacho kinaendelea kwa watu wenye Akili na HEKIMA.

Katiba inaweza kukupa Haki ya kugombea kitu Fulani lakini mazingira na wakati vikakunyima haki hiyo
Au Elimu yako ya kukariri unashindwa kuelewa mambo madogo kama hayo?
 
Unasemaje?
 
Reactions: Tsh
Vijijini ndio hawataki hata kusikia jina lake wanaona kama msaliti yaani chawa wa ccm au political entrepreneur
 
Kumbe Mbowe alikuwa mvurugaji toka kitambo sana. Ni vile tu hatukujua
Mbowe hakuwa mvurugaji ila sasa ndiyo ameamua kuvuruga, Mbowe alijitahidi sana kukijenga hiki chama Ila dakikaa za mwishooo kabisa roho ya usaliti ikamwingia, Shetani anamwingiavmtu mda wowote, Roho ya usaliti ilipo mwingia, akaenza kwenda kinyume na agano aliloliweka na wanaCHADEMA akaona ili, madhambi yake ya usaliti yasije kujulikana lazima amkabidhi kijiti Mtu anaye, mwamini kwahiyo, Akaamua kugombea na mwaka huu na Lisu alivyojua kuwa Mbowe anagombea kipindi hiki tena, naye hakuwa na shida, akatangaza kugombea umakamu, Akashtukia wenje naye Anatangaza kuwania umakamu, Washauri walisu wakamtonya kuwa Huyo ni Mshirika wa Mbowe na mkakati wao nikung'oa umakamu kwasabu Msure kashaonjeshwa asali na Wamekubaliana na Mama yeye agombee Urais ili mama asipate Competition is ya maana kwahiyo wewe livumbulue, Hata ukishindwa huna cha kupoteza. Ndiyo hapo Lisu akaanzisha huu mtanange kutibua deal la watu. Sasa mambo mshike mshike kila kona, mwizii huyo mwizi huyoo, wengine, mchonya asali, mchonya asali mishale kila kona ila yeye anajifanya Nyegere ata ang'atweje, Kwani mchonya asali achonyi mara moja. Pamoja na mishale yote ya nyuki, yeye yumo tu.Pia kulikuwa na minong'ono ya serikali ya Nusu mkate ambayo Baadhi ya viongozi waandamizi wangepata ubenge na uwaziri, Mmm lakini hizi Porojo zangu tu msizitilie Maanani.
 
Tatzo kura anaweza kupata uchaguzi ukiwa wa kifisi
 
Aiseee si aweke silaha chini
 
Mifano yako ni irrelevant.
Tuwaache wajumbe na wenye chama chao wachague wanayemtaka. Nyie wanaharakati subirini atakayepata kura nyingi mfanye naye kazi.
Nawahakikishia wanaharakati bila vyama vya siasa hamna mtalachofanya, yaani mtakosa kazi za kufanya.
Malema wa Afrika Kusini unaweza kumfananisha na TAL ingawa kuna maeneo wanatofautiana. Sasa angalia Malema ameishia kwenye harakati wakati wenzie wanafanya siasa na kupitia uchaguzi uliopita unaweza kuona matunda ya kila chama.
 
Mbowe angepata fursa ya kutawala Tanzania angekuwa ni Dikteta wa hatari na angemteua Yericko awe ndiye Malyamungu wake wa kushughulikia Critics wake trust me na angefia Ikulu na Jeshi angejaza watu wake ili lisimpindue.

Huenda nikajiunga na ATC wazalendo siku za usoni au nikabaki kwenye Jukwaa la Sauti ya Watanzania.
 
Mbowe ameonekana vile alivyo
 
Pambaneni mnavyoweza ila mkumbuke anayetaka kuwa mwenyekiti wa CHADEMA lazima agombee na apate kura kuwazidi wengine.

Nilikuwa namkubali Lissu kuliko hata Mbowe, ila baada ya Lissu kuleta tuhuma zisizi na ushahidi nimemwona hafai hata kuwa mjumbe.
 
Mbowe ameshindwa kusoma alama za nyakati. Watu hawaamini aina za siasa anazofanya, siasa zisizoinyima CCM usingizi!
All politicians are crooks, wawe wa opposition au wa rulling party there is no difference.
Kuamini wanasiasa ni uzoba uliokithiri.
 
Pambaneni mnavyoweza ila mkumbuke anayetaka kuwa mwenyekiti wa CHADEMA lazima agombee na apate kura kuwazidi wengine.

Nilikuwa namkubali Lissu kuliko hata Mbowe, ila baada ya Lissu kuleta tuhuma zisizi na ushahidi nimemwona hafai hata kuwa mjumbe.
Wote wamejivua nguo kwa kutanguliza tamaa zao binafsi huku wakikibomoa chama chao, they're all playing dirty games out of greediness.
Kinachomsaidia Lissu ni kuwa na chawa wengi ambao wako very vocal, all in all pomoja na kwamba Lissu fuses nyingi za kichwani kwake zimeungua ndiye anayeweza kuipa kashkash CCM jambo ambalo Mbowe kwa sasa haliwezi.
Yale maneno yake anayotiririkaga na uchambuzi wake wa namna anavyokosoa mikataba ya 'kihuni' itarudisha amsha amsha kwenye upinzani, ila honestly uwezo wa kuongoza institution hana. Yupo sampuli za late Mtikila.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…