Kingine ambacho ni uongo tena mkubwa kabisa kwenye hii screenshot yako, kwa mujibu wa hiyo screenshot, kabla ya kupandishwa huko (ambapo ni uongo) inamaana afisa forodha msaidizi(diploma holder) na afisa forodha (bachelor holder) [kama nimekosea viwango vya elimu nisahihishe] it means wote walikuwa wanalipwa milioni moja, ndomaana uksasema huyo afisa forodha msaidizi akapanda kutoka 1mil mpaka 2mil, na afisa forodha naye akapanda kutoka 1mil mpaka 3 mil.
Yaani afisa forodha msaidizi na afisa forodha (ambavyo ni vyeo viwili tofauti) wote kabla ya kupanda walikuwa wanalipwa mshahara sawa Yaani milioni moja, inawezekanaje watu wenye cheo tofauti (probably mmoja ni degree mwingine ni diploma) walipwe mshahara sawa?
Huo si uongo wa mchana kabisa? Yaani hata hamjui kudanganya? Hapo hata mtoto mdogo anawashtukia, hata kama mmepanga kudanganya, itabidi uongo uendane na ukweli, siyo mnakopi screenshot za nyuzi za mitandaoni ndo mnatupestia hapa.
HITIMISHO.
Kwanza mishahara mliyopost ni ya uongo, ina ukakasi mwingi.
Pili hata ingekuwa ni mishahara ya kweli, bado siyo ya kutisha mtu, siyo kwa makamanda wala taasisi zingine zinazolipa, hata ukiidabo, rubani ndo humfikii kabisaa, na kwa namna hiyo, hata TPDC wamewapiga gap.