Hizi ngonjera mliitwa ? Acheni ngonjera kujiona wa muhimu kuliko walimu na madaktari ..Mnapigana vita kila siku ? Acheni zenu ...Watu mnatoka mpaka vitambi kwa uhai upi unaoweka rehani ..Wenzenu madaktari ni muhimu kuliko nyie zaidi ya kutumika kisiasa.
Dogo acha dharau na dharau zitakuponza.
Kwenye hii nchi kila taasisi zina umuhimu wake ila kuna taasisi zina umuhimu zaidi.
Hii nchi bila kulindwa unadhani pangekalika kweli hata hao madaktari wangediriki kutibu watu kweli unajua usiongee utumbo kufurahisha watu tu humu.
Wanaume hawalali wapo mipakani wanakulinda wewe halafu unachukulia poa hivi unajua hata kinachoendelea mipaka ya Mtwara na Msumbiji wanaume wamekufa kwa ajili yako wewe uliye kwa shemeji yako.
Emu vuta picha nchi hii yani hkuna Jeshi na tunaishi na majirani kama Akina Rwanda, DRC, Msumbiji na n.k vipi hapo pangekuaje hapo.
Taasisi pekee ambayo hata Rais hawezi Kuja kuiongelea utumbo ni Jeshi na hutaweza kuuona huo ujinga kama unabisha mwambieni Rais afanye hivyo.
Marehemu Rais Magufuli alipofariki nchi ilikuwa chini ya udhibiti wa Jeshi yaani CDF Mabeyo mpaka Rais alivyoapishwa hivi unadhani Mabeyo angeamua kukataa uapisho wa Rais na kupitisha utawala wa kijeshi kuna mtu angeinua pua yake pale?
Hao madaktari waligoma kipindi cha Rais mstaafu Kikwete uliza kilichofanyika mpaka Leo sidhani kama watarudia na hao hao wanajeshi ndio walikuwa wanaenda kutibu watu badala ya madaktari na hakuna daktari aliye bembelezwa na waliufyata wenyewe na wakarudi kazini wenyewe halafu unakuja kuongea pumba hapa.
Alikuwa sijui ni Waziri yule kama sikosei alishiba kama wewe hivyo hivyo makande akawa anaongea pumba kama zako masaa kadhaa kupita hana kazi halafu jobless mmoja unapata ujasiri wa kuongea shit kama hizo.
Unasema wanapata vitambi wewe ulitaka wote waende mipakani sio?? Acha uzwazwa