Huyo Tanganian kakimbia baada ya kuona kapotosha screenshot zake, sisi tulikuwa tunajadili kuwa madaktari hela zao ni ndogo cha ajabu unanichanganyia na mambo ya taasisi kana kwamba hujui tulikuwa tunajadili nini, na screenshot ya take home ilitumwa huku na pia pesa wanazopokea specialist nimetaja, yote hayo huelewi hadi utumiwe waraka?- Kama scales hazizajwi hauna base ya kusimamia, itakuwa ni story za Vijiwe vya kahawa tu, na ndio maana hata Tanganian alionekana kakushinda kwa hoja kwa sababu yeye alikuwa analeta hadi salary scale za mashirika ya umma, akakuambia kuwa TCAA salary scale ni 4m, per diem ni 200,000/, pia Wana extraduty 900,000/-, housing 800,000/-
-oncall allowance inalipwa kwa appearance au kwa flat rate?
- weka huo waraka unaosema hivyo,au source ya hiyo taarifa, kwa sababu hata per diem, extraduty zilivyopanda haikuwa siri ilitangazwa
- btw Kingine hizo posho unazozifanya siri wala sio pesa nyingi, taasisi per diem ndio Zina weBoost mwenzio anapata safari za siku 20-15 Kila mwenzi ukifanya hesabu hapo utakuta analipwa per diem za 4m, akijumlisha salary, extraduty, housing, transport, anazaidi ya 8m, wakati wewe ukipata safari ya kikazi per diem yako ni 100,000/-
On call allowance kwa siku waraka unasema ni 50K, kwa mwezi mtu anaweza akawa na call kumi so ni total 500K, sasa cha ajabu hazilipwi hizo, watu wanalipwa 100K kwa tamisenga na 250K kwa wizarani, waraka wenyewe unasema, pesa italipwa kulingana na bajeti ya mwajiri, inaonekana mkurugenzi anatumia hicho kipengele kulipa watu hela ndogo.
Ni kweli watu wa afya kazi yao ni ya muhimu ila hawana hela.