Aliyeuawa na Mumewe 2019 kuagwa leo

Aliyeuawa na Mumewe 2019 kuagwa leo

Mwili wa marehemu Naomi Orest Marijani aliyeuawa na mume wake kisha kuchomwa moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ndani ya banda la kuku na mume wake Hamis Luwongo Mei 15, 2019 Maeneo ya Gezaulole Kigamboni Jijini Dar es Salaam, unaagwa kwa baba yake mdogo maeneo ya Mtoni Kijichi leo Ijumaa Machi 14, 2025 kwaajili ya kusafirishwa kwenye maziko nyumbani kwao Moshi Kilimanjaro.

Hii ni baada ya hukumu iliyotolewa Februari 26, 2025 na Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam na Jaji wa mahakama hiyo Hamidu Mwanga kunyongwa hadi kufa kwa aliyekuwa mume wake Hamis Luwongo kukutanika na hatia ya kumuua mke wake wa ndoa, Naomi Marijani.

hiki kisa nawaelewa sana kataa ndoa!!!!
 
Yani nikuoe unirudie nyumbani kwangu saa 7 usiku umelewa na maneno ya shombo.

Hata mie nakutoa kichwa.
 
Kimbia kwa Usalama wako, tena Hama nyumba kapange self container room moja chaaap.
Piga kazi mbwa inayokusumbua itapata akili baadae wewe ushapata mke mwingine
Ni moja ya njia nzuri kuepuka majanga makubwa baada ya ugomvi wa kimahusiano (bila kujali ni ME au KE anaamua kufanya hivi). Lkn pia inapotokea mtu anafanya hivi pia hulaumiwa sana.
 
Ni Heri nikimbie nyumba yangu,kinaanze upya kuliko kuua.

Sababu mwanamke anachotaka ni kukuumiza kihisia,sasa ukiwa haupo unaumiaje?

Kaa mbali tu,anza upya Utakua na amani.
Ona mtoto nasikia alianza kukaa Sawa darasani na kiakili wanamtonesha tena.

Mapenzi yakiisha zibaki akili jamani.
Yeah
 
Sema ndo ina mambo mengi sana na kila mtu akikwambia yaliyoko kwenye ndoa yake hutokuja kuamini.
Kuna watu wanamiaka 7 toka wafunge ndoa leo kila moja analala kitanda chake kwa muda wa mwaka sasa ukiuliza chanzo ni usaliti ndani ya ndoa.
Hata kifo cha naomi ni usaliti ndani ya ndoa
 
Sema ndo ina mambo mengi sana na kila mtu akikwambia yaliyoko kwenye ndoa yake hutokuja kuamini.
Kuna watu wanamiaka 7 toka wafunge ndoa leo kila moja analala kitanda chake kwa muda wa mwaka sasa ukiuliza chanzo ni usaliti ndani ya ndoa.
Hata kifo cha naomi ni usaliti ndani ya ndoa
 
Hamis uko alipoo Majuto ni makubwa mno anatamani ile siku Angempa talaka tuu yaishee.
Hamisi ni Muislam kwanini asinge ongeza mke na Dini ina ruhusu tena Wake wa nne, Yeye angel mke mwingine tu mbona Dar pisi kali zipo nyingi tu tena angeo mke wa pili na angeishi nao pamoja, Wazee wetu hawakufanya matukio ya kikatili kwasababu walikua wana oa wake wengi utakuta Mwanaume kaoa wake 6 au 4 kwahiyo Mke mmoja akizingua anaamia kwa wengine.
 
Back
Top Bottom