Aliyewaandaa Masanja na Nyerere kwenda kuzungumza Mbele ya viongozi wa Mataifa mbalimbali awajibishwe

Aliyewaandaa Masanja na Nyerere kwenda kuzungumza Mbele ya viongozi wa Mataifa mbalimbali awajibishwe

Kwahiyo ikakutachii ?
Nilishangaa hilo neno "unataka baba yako ndio asafiri?"

Sidhani hata mama Samia alishawahi kujibu hizo tuhuma kwa maneno kama ya Masanja!

Ile ni hadhara yenye watu wa kitaifa na kimataifa, hivyo sidhani kama ni vyema kuleta vichekesho kwa matusi!



Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Yaani sherehe haikua nzuri kabisa aise nafkiri kuna tatizo flan waandaji wametuletea kwaya za vijijini halaiki sio nzuri kama tulizo wahi kuona
Kwaya zenyewe wanaimba wamevaa ijabu na kukatika viuno na ija u zao wawalete na masister wakatike viuno Kama ni hivyo
 
Nilishangaa hilo neno "unataka baba yako ndio asafiri?"

Sidhani hata mama Samia alishawahi kujibu hizo tuhuma kwa maneno kama ya Masanja!

Ile ni hadhara yenye watu wa kitaifa na kimataifa, hivyo sidhani kama ni vyema kuleta vichekesho kwa matusi!



Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Mbona ya kawaida Sana hiyo....

tena hapo ungemkuta magufuli na vile vijembe na matani yake hahah ...

Jamani masanja alikua anafanya matani tu. Ni kama matani yale kwenye sherehe zetu na misiba Yetu tunavyotaniana, ndio alichokifanya masanja kama comedian . Sasa hapo masanja kafanya aibu gani kwa taifa ?

Yaani sioni hapo ishuu ya watu kukomalia na kuchefukukwa hapo. Jambo la burudani hilo. Sema matani yake Kama yamewagusa baadhi ya watu kumoyo 🤣🤣

Jamani muache unafiki.. msijikute mko serious Sana mkasahau kwamba masanja alikua ana entertain umati kwa njia ya matani.
 
Hebu wabadilishe style yao hiyo ya kuwaita hao sijui wachekeshaji kwenye matukio hayo

Ova
 
Taifa liko kwenye hatari kubwa Sana , rasilimali watu inapotumika vibaya mahali pasiko sahihi na muda / wakati usio sahihi inaweza kuleta balaa kubwa Sana katika mahusiano ya nchi na nchi au watu na watu wengine wasio na itikadi moja

Kwa kweli Masanja ameongea neno ambalo hatupaswi kuluangalia kwa udogo ,Ni hatari Sana,taifa aliloongelea watakaa kutathimini tukio ambalo Rais wao amehudhuria , unahisi Nini wakifima hicho kipengele alichoongea Masanja kuhusu nchi ya Rwanda?

Unadhani maafisa wa Rwanda wa Usalama hiyo kauli wataichukulia poa?

Vipi wakidhani hiyo kauli siyo ya uchekeshaji , wakidhani ni imelenga Jambo fulani? Na hasa ukiunganisha matukio yaliyopita kuhusu nchi yetu na Rwanda?

Je wakidhani labda ametumwa kupitia uchekeshaji wake kutuma ujumbe kwa nchi nyingine , je ikitokea hapo mbeleni maana hatujui kesho yetu na migogoro haina ahadi , ikawa Tanzania na Rwanda tukaingia mgogoro watahisi Nini ?

Je , wakijiuliza kwa Nini aitaje Rwanda wakati dunia Ina mataifa mengi Sana?

Nina maswali kama 200 kujiuliza kuhusu maneno aliyosema Masanja

In the speech , do not mention the names that you think your speech will be ambiguous in later days
 
Katika hafla kubwa ya Kitaifa kama iliyofanyika Le ambayo camera za mataifa Mbalimbali zinaelekezwa Kwetu tumeshindwaje kuleta watu wenye akili wanaoweza kuitangaza nchi tunaleta watu Wanafoka na kuongea vitu visivyoeleweka. Mtu huyu anaongea as if yupo kwenye mkutano wa Kijiji. Bora tungewapa Maliasili hizo dakika watuonyeshe rasilimali zetu za kitalii.

Kama tuliona Masanja ana umuhimu tulishindwa kumuuliza anakwenda kusema nini? Aliyempa tenda Masanja anafanya nini Ofisini?
Screenshot_20211209-181649.jpg
 
Back
Top Bottom